Ishara Za Uchungu Wa Uzazi

Ishara Za Uchungu Wa Uzazi

Ukishuku kuwa maji yako yame vuja ama kuanza kushuhudia ishara za uchungu wa uzazi tulizo angazia, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako.

Uchungu wa uzazi ni mchakato wa asili unaotendeka mwilini wa kujifungua mtoto. Huanza na kubanwa kwa asili kisha kuendelea na kuwa kujifungua kwa mtoto na placenta. Baadhi ya wanawake huwa na ishara za kipekee za uchungu wa uzazi, wakati ambapo wengine hawana. Wataalum bado wana fanya utafiti kudhihirisha kinacho fanya uchungu wa uzazi kuanza ama kinacho athiri wakati ambao utaanza. Kuna homoni nyingi na mabadiliko ya kifizikia yanayo saidia kuonyesha kuanza kwa uchungu wa uzazi.

Ishara Za Uchungu Wa Uzazi

ishara za uchungu wa uzazi

Kuanguka kwa mtoto (maarufu kama lightening kwa kimombo)

Mchakato wa mtoto kusonga kwenye sehemu ya chini ya pelvisi masaa machache kabla ya kuanza kwa uchungu wa uzazi kunajulikana kama lightening ama "kuanguka kwa mtoto."

 • Kunaweza fanyika wiki chache ama masaa machache kabla ya uchungu wa uzazi.
 • Kwa sababu uterasi inalalia kibofu cha mkojo zaidi baada ya mtoto kuanguka, huenda ukahisi haja zaidi ya kukimbia msalani kila mara.

Ongezeko la kamasi

Kiwango cha kamasi kinacho toka kutoka kwa kizazi kina zidi na kupitishwa kwenye uke. Kizazi kina anza kuwa kipana. Uchafu wa uke/kamasi huenda ukawa wa rangi nyeupe na wazi, ya pinki ama na kiasi kidogo cha damu. Huenda uchungu wa uzazi ukaanza masaa machache ama wiki chache baada ya hili.

Kubanwa

Mama mjamzito hushuhudia kubanwa misuli ya uterasi inapo kazwa. Tumbo huwa ngumu, na kati ya kubanwa huku, uterasi hutulia na tumbo kuwa laini. Jinsi mwanamke mmoja anavyo hisi katika kipindi hiki ni tofauti na mwingine ama hata tofauti kati ya ujauzito mmoja hadi mwingine.

 • Uchungu wa uzazi husababisha kuumwa mgongo ama upande wa chini wa tumbo na kushinikiza pelvisi
 • Uchungu huanza upande wa juu wa tumbo ukielekea sehemu ya chini
 • Kwa baadhi ya wanawake, uchungu huu ni sawa na uchungu wa hedhi
 • Tofauti na uchungu wa uzazi usio wa kweli, uchungu wa uzazi wa kweli haupungui ukibadilisha mtindo wa kuketi

Kuharisha

Huenda ukagundua kuwa haja yako ni ya majimaji ama imelegea. Huku kuna maana kuwa utaanza kushuhudia uchungu wako wa uzazi baada ya siku moja ama mbili.

Kukata uzani

Ukiwa mjamzito, huenda ikaonekana kana kwamba utazidi kuongeza uzito mpaka siku ya mwisho. Wanawake wengi huanza kupunguza uzito siku chache kabla ya kushuhudia uchungu wao wa uzazi.

Hisia za kujipanga

Wanawake wengine huhisi haja ya kujipanga na kuhakikisha kuwa mambo yote yako sawa kabla ya mtoto kufika. Baada ya kuhisi uchovu kwa muda mrefu, unaanza kuhisi una nishati. Unaanza kununua nguo zaidi za mtoto, vitu vya nyumba na kutayarisha chumba cha mtoto. Hakikisha kuwa hufanyi kazi sana kwani kujifungua kuta hitaji nishati nyingi.

Mtoto kutulia tumboni

Unapo karibia kujifungua, mtoto amekuwa mkubwa na hana nafasi nyingi ya kusonga tumboni. Wiki za mwisho kabla ya kujifungua, utapata kuwa mtoto ametulia na hasongi sana ikilinganishwa na hapo awali.

Kuumwa na tumbo na mgongo

Kwa mama wa mara ya kwanza, huenda ikawa vigumu kwake kutambua kubanwa kabla ya kujifungua. Kwani uchungu huu ni sawa na uchungu wa kipindi cha hedhi. Uchungu huu unaweza zidi ama kupungua, pamoja na maumivu ya upande wa chini wa mgongo unakuja na kuisha.

Kuvuja maji

Ishara Za Uchungu Wa Uzazi

Kutoboka kwa amniotic membrane inayo mzingira mtoto na kumlinda akiwa tumboni huenda kukafanyika kabla ya kuenda hospitalini.

ishara za kuvuja maji

 • Kiwango kingi kutoka mara moja ama kutiririka kiasi kidogo
 • Maji haya huwa hayana harufu wala rangi
 • Sio wanawake wote ambao huvuja maji wakiwa katika uchungu wa uzazi. Kwa wanawake wengine, madaktari hutoboa gunia hilo wenyewe
 • Unapo shuhudia kuvuja maji, andika unacho kishuhudia, wakati unapo shuhudia haya na rangi ya maji hayo kisha umjulishe daktari wako atakaye kushauri unacho stahili kufanya

Kukonda kwa kizazi

Unapo shuhudia uchungu wa uzazi, kizazi chako kita konda na kuwa kifupi (effacement) ili kinyooke na kufunguka karibu na kichwa cha mtoto wako. Daktari wako anapofanya kipimo cha pelviki atakuelezea iwapo kuna mabadiliko yanayo onekana ama la.

Kufunguka kwa kizazi

Kunyooka na kufunguka kwa kizazi (dilation). Mabadiliko haya yana pimwa kwa sentimita. Mama akiwa tayari, dilation yake ni sentimita 10. Effacement na dilation yana sababishwa na kubanwa kwa uterasi. Ili daktari adhibitishe maendeleo katika uchungu wa uzazi na iwapo mama ako karibu kujifungua, wanapima kiwango ambacho kizazi kime konda na kujifungua kukubalisha kupita kwa mtoto kupitia uke wake.

Tofauti kati ya uchungu wa uzazi wa kweli na usio wa kweli ni nini?

 • Uchungu usio kweli hauji mara kwa mara na haukaribiani, huku uchungu wa kweli ukiwa katika kwa mara hasa kama vile baada ya kila sekunde 30-70. Baada ya wakati, kubanwa huku kuna zidi na kukaribiana
 • Uchungu usio wa kweli huenda ukakoma unapo tembea ama kupumzika wakati ambapo uchungu wa kweli huendelea hata ukibadili mtindo wa kukaa ama kutembea
 • Uchungu wa uzazi usio kweli huwa mwepesi na hauongezeki. Ama ukawa mwingi kisha kupunguka. Uchungu wa kweli huzidi kuongezeka na kuwa na uchungu zaidi.
 • Usio wa kweli huhisiwa upande wa mbele wa tumbo na sehemu ya pelviki, huku uchungu wa kweli huanza sehemu ya chini ya mgongo na kuenda sehemu ya mbele ya tumbo.

Jaribu kupumzika

Ni vyema kupitia hatua ya kwanza ya uchungu wa uzazi ukiwa nyumbani mwako. Kufanya mambo haya kutakusaidia:

 • Tembea ndani ama nje ya nyumba
 • Jaribu kutizama sinema
 • Koga kwa maji ya vuguvugu kutuliza mwili
 • Pumzika, jaribu kulala

Ukishuku kuwa maji yako yame vuja ama kuanza kushuhudia ishara za uchungu wa uzazi tulizo angazia, hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako. Ata kushauri jambo unalo paswa kufanya ama hata kukwambia ufunge safari kuelekea hospitalini.

Soma Pia:Mambo Ya Kutarajia Maji Yanapo Vuja Kabla Ya Kushuhudia Uchungu Wa Uzazi

Written by

Risper Nyakio