Kugundua uhusiano usio na afya sio jambo rahisi. Hasa pale ambapo haujaishi na wanandoa hawa na wanapokuwa nje ya nyumba wanaonekana kuwa wanajali wenzi wao. Lakini ishara zilizo wazi kama wanandoa kuhusika katika vita vya kifizikia ama matusi zinadhihirisha mahusiano yasiyo na afya. Lakini kwa wanandoa wanaoshikana mikono hadharani na kukosa kuongeleshana wanaporudi nyumbani, ni vigumu kutambua.
Kumbuka kuwa sio tabia zote za kujali zilizo na afya. Sio jambo geni kwa matendo hayo kuwa yanatumika kuficha matatizo ya undani. Huenda ikawa pia wanandoa hawa wamezoea kuonyeshana wanasikizana wanapokuwa miongoni mwa watu. Ni vyema kutafiti na kujua motisha ya matendo haya.
Ishara za uhusiano usio na afya

Sio lazima iwe ni ishara zilizo wazi, mbali ishara ndogo tunazopuuza katika uhusiano. Na zinapotokea, zinapaswa kuzungumziwa.
Usawa katika uhusiano. Uhusiano wenye mafanikio mara nyingi huwa pale ambapo kila mwanandoa anahisi kuwa anasikizwa na kila mtu anafanya jukumu lake. Lakini mambo yakibadilika na mwenzi mmoja aanze kufanya zaidi ya mlivyokubaliana na kutaka wakati wote mambo yaende anavyotaka, kuna tatizo. Jambo muhimu kufanya ni kuwa na mazungumzo ya kina kabla ya hali kuwa dharura.
Kukosa imani. Uhusiano ambapo wanandoa hawaaminiani sio wenye afya. Mwenzi mmoja anapoanza kuwa na shaka kuhusu vitendo vya mwingine, kuna tatizo. Na lisipojadiliwa, huibua masuala makubwa zaidi.

Hasira. Ni kawaida kukasirika mara kwa mara, hasa mnapokuwa mnaishi pamoja na mtu. Lakini iwapo mchumba mmoja anakasirika wakati wote na kukasirishwa na mambo machache. Ni vyema kwa wanandoa kuwa na mazungumzo ya kina. Uhusiano ni mahali ambapo wanandoa wanapaswa kuwa huru, lakini mmoja anapohisi kuwa lazima awe makini na anachosema wakati wote, uhusiano huo sio bora.
Kutumia mapenzi kufaidika. Sio kila mtu anayeingia katika uhusiano na nia nzuri. Kuna wanaoingia katika uhusiano na mtu wanayeona kuwa watafaidika. Hata hivyo, hamwelezi. Na kwa upande wake, ana nia nzuri. Mwishowe, anavunjwa roho. Sio vyema. Pia si vyema kwa wanandoa kutumia hisia zako kuchukua faida ya wanachotaka.
Soma Pia: Mambo 5 Usiyo Yafahamu Kuhusu Familia Ya Billionea Peter Obi