Wakati wa uja uzito, wazazi wengi, hutaki kujua iwapo mtoto watakao pata ni msichana ama mvulana. Iwapo hauna uhakika kamili atakua wa jinsia gani kabla ya wiki 20 , kuna imani tofauti zinazo zingatiwa na kuaminika kuwa za kweli. Ni haki kusema kuwa hupaswi kuziaminia kwa sana imani hizi. Unapata uhakika kweli kuhusu jinsia ya mtoto wako anapo zaliwa. Kupima jinsia ya mtoto kupitia mashine huenda ikawa kweli ila haina usawa wa asilimia mia moja. Ni muhimu kuelewa ishara za uja uzito. Je, nini ishara iwapo utapata mtoto wa kike ama wa kiume?
Ishara za uja uzito: Jinsi ya kugundua iwapo ni mtoto wa kike ama wa kiume
Imani za kutabiri zimegawanyika katika vikundi tofauti. Na katika kila kikundi ni ishara za kujua iwapo utajifungua mvulana ama msichana. Vikundi hivi ni:
- Ishara za kusema za kimwili
- Ishara za mhemko
- Imani za nyanya wazee
- Vipimo vya nyumbani
- Kupima
Ishara za kusema za kimwili

1. Umbo la tumbo
Miongoni mwa watu huwa na imani kuwa wanaweza kutabiri jinsia ya mtoto kufuatia umbo la tumbo ya mama mja mzito. Iwapo tumbo imo upande wa chini wa sehemu za siri za mama, unamtarajia mvulana. Ila tumbo inapo egemea upande wa matiti, unamtarajia msichana.
2. Ugonjwa wa asubuhi
Imani hii imedhibitishwa kuwa ya kisayansi. Ugonjwa wa asubuhi ulio ongezeka ni ishara kuwa unamtarajia mtoto msichana. Iwapo unamtarajia mtoto wa kike, kuna ongezeko la idadi ya oestrogen mwilini inayo sababisha ugonjwa wa asubuhi.
3. Unene wa matiti
Iwapo chuchu zako hazitoshani, huenda ikatumika kuashiria iwapo unatarajia kupata mtoto msichana ama mvulana. Chuchu kubwa ya upande wa kushoto huashiria kuwa unamtarajia mtoto wa kike. Iwapo kama chuchu ya kulia ndiyo kubwa, hivyo basi unamtarajia mtoto mvulana ama wa kiume.
Ishara za uja uzito: Ishara za kihemko

4. Kubadilika kwa hisia
Hii huwa ishara iwapo unamtarajia mtoto wa kike ama wa kiume. Kubadili kwa hisia kwa kiasi cha sana kuna maana kuwa unamtarajia mtoto msichana. Iwapo ni jambo la kawaida kwa wanawake wote kushuhudia mabadiliko haya.
5. Ndoto
Kuna imani ya kutumia ndoto kama ishara ya jinsia. Iwapo unapata ndoto kuhusu wasichana, kuna uwezekano mkubwa kuwa unamtarajia mtoto msichana. Iwapo ndoto zako ni kuhusu wavulana, huenda unamtarajia mtoto wa kiume.
Ishara za uja uzito: Imani za nyanya wazee
6. Unavyo lala
Jinsi unavyo lala huenda ikawa ishara ya jinsi ya mtoto unayo tarajia. Kukusaidia kujua jinsia unayo tarajia, unapo lala kwa upande wako wa kulia, una mtarajia mtoto msichana iwapo una lala kwa upande wako wa kushoto, una tarajia mtoto mvulana.
7. Kutamani vyakula
Miongoni mwa wanawake hutamani vyakula vitamu wanapo kuwa waja wazito iwapo wengine hutamani vyakula vya chumvi. Tofauti hii huenda ikatumika kuashiria jinsia unayo itarajia. Kutamani vyakula vitamu huenda ikawa ishara kuwa utapata mtoto wa kiume.
Ishara za uja uzito: Kipimo cha nyumbani

8. Kipimo kutumia mkate wa kuoka
Baadhi ya watu wana imani kuwa kipimo hiki huashiria jinsia ambayo mama mja mzito atapata. Kinacho dhibitisha ni tokeo baada ya mkojo kupatana na mkate huu wa kuoka iwapo kuna sauti inayo tolewa au la ni ishara ya jinsia unayo kusudia.
9. Kipimo cha mkono
Kuuwekelea mkono wako kwa kila upande wa tumbo huenda lika ashiria jinsia ya mtoto wako. Mkono wako utaviringika kwa tumbo iwapo ni mtoto msichana. Ila iwapo ni kijana, mkono wako utaingia ndani kidogo.
Njia nyingi kati ya hizi za kutabiri huwa za kufurahisha. Hakuna ubaya kutaka kujaribu baadhi ya njia hizi. Ila kuwa na uhakika, huenda ikakupasa kuwa mtulivu na kungoja.
Read also: Boy And Girl Baby Names That Carry Good Fortune
Source: Healthline