Katika siku za hapo awali, IVF iliongelelewa kwa sauti za chini ambazo hazingependa kusikika. Je, IVF ni nini? Hivi leo, mambo ni tofauti na IVF ni jina maarufu. Sio tu njia ya wazungu ya kupata mimba. Tuna angazia kwa kina maana ya IVF.
Je, IVF ni nini?

Ufupi wa In vitro fertilization, ni njia inayotumia teknolojia kumsaidia mwanamke kutunga mimba kwa kusaidia uwezo wake wa kuwa na rutuba, ukuaji wa fetusi na kujipandikiza kwa yai kwenye uterasi. Wanandoa wanapata mimba kwa urahisi.
IVF hufanyika kwa kutoa ovari za mwanamke na manii ya kiume kisha kuchanganywa kwenye maabara ya kimatibabu. Ili kukubalisha manii kurutubisha mayai. Mimba inapofanyika na fetusi kuchukua shepu, mtaalum ataipandikiza kwenye uterasi.
Kwa nini IVF inatumika?
Mbinu hii hutumika kwa sababu tofauti. Baadhi ya wanandoa huitumia kama njia ya mwisho, huku wengine wakiitumia kwasababu wangependa kupata mtoto zaidi ya mmoja.
Baadhi ya sababu kwa nini watu hutumia IVF:
- Kwa visa ambapo ovari inakosa kufanya kazi, kuwa na fibroids kwenye uterasi na matatizo ya kupevuka kwa yai
- Endometriosis
- Kuwa na fallopian tubes zisizo fanya kazi
- Mzazi mmoja ama wawili kuwa na tatizo la kijeni ambalo hawangependa kupitisha kwa kizazi chao
- Kwa visa ambapo mirija ya kizazi imetolewa kupitia kwa upasuaji
- Mchumba wa kiume ana tatizika na ugumba kama kuwa na idadi ya chini ya manii ama manii kukosa uwezo wa kusafiri
Ufanisi wa IVF

Watu wanao uliza swali, 'je, IVF ni nini' mara nyingi wanataka kujua nafasi za kufaulu kwa mbinu hii. Ni muhimu kufahamu kuwa asilimia ya kufaulu kwa mbinu hii kunategemea:
- Umri wa mama
- Mitindo ya maisha
- Historia ya uzalishaji
- Endometriosis
- Chanzo kikuu cha ugumba
Kulingana na utafiti, asilimia 33 ya mbinu za IVF hufaulu. Na kumaanisha kuwa asilimia 33 ya wanawake hupata mimba na kujifungua kwa ufanisi mara ya kwanza baada ya kujaribu IVF.
Kufuatia sababu fulani za hatari, mbili kati ya mimba tatu ya IVF huenda ikaharibika. Lakini kuna hatua ambazo wanawake wanaweza kuchukua kuongeza nafasi zao za kubeba mimba hadi ikomae.
- Pumzika vya kutosha
- Kupunguza mawazo mengi
- Kukoma mitindo kama kuvuta sigara na kunywa pombe
- Kula vyakula vyenye afya hasa matunda na mboga
- Kuchukua vitamini za prenatal inavyofaa
- Kunywa maji kwa wingi
- Kwenda kwa kliniki za antenatal
Ni vyema kwa wanawake kukumbuka kuwa, kujifungua kupitia kwa IVF hakukufanyi kuwa mama mchache ikilinganishwa na wengine. Furahi kuwa umepata baraka zako.
Kumbukumbu: NHS
IvfWorldwide.com
Soma Pia: Athari Hasi Za Kutumia Tembe Za Kupanga Uzazi