Nchi ya Kenya imeshuhudia mlipuko wa nzige wa jangwani ambao wamesababisha hasara kubwa hasa kwenye mimea. Ni wakati wenye shaka nyingi baada ya wadudu hawa wanao semekana kutoka Nchi inayokaribia ya Somalia kuingia Nchini Kenya. Wadudu hawa wanajulikana kwa hasara kubwa wanayo sababisha. Kwa kuiharibu mimea na kusababisha kupunguka kwa chakula.
Nzige hawa wameshuhudiwa katika idadi kubwa katika nchi za Somalia na Ethiopia. Inasemekana kuwa nzige hawa walitoka nchi la Yemen na Bahari la Shaba. Imekuwa zaidi ya miaka 70 kutoka nchi ya Kenya iliposhuhudia uwingi kiaisi hiki cha nzige wa jangwani. Katika nchi ya Somalia, inasemekana kuwa nzige hawa wameiharibu mimea na huenda nchi ikashuhudia uhaba wa chakula. Nzige wana uwezo wa kusafiri kwa umbali wa maili 93 ama kilomita 150 kila siku. Uwezo huu unawezesha kusafiri kwa kasi zaidi na kuadhiri sehemu tofauti za nchi.Wanakula chakula kingi kwa siku. Wakiwa kwa idadi kubwa, wana uwezo wa kuharibu mimea mingi sana.

Mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2019, Nchi ya Kenya ilishuhudia kiwango kikubwa cha mvua ambacho kinasemekana kilitengeneza mazingira mema ya kuhimiza uwepo wa wadudu hawa. Kadri siku zinavyo zidi kupita, ndivyo janga hili linavyo endelea kuongezeka na kuwa mbaya zaidi. Wadudu hawa wamesafiri katika sehemu tofauti za nchi ya Kenya, Isiolo, Meru, Ukambani na sehemu ya kati ya nchi.
Iwapo janga hili la wadudu hawa wa nzige nchini Kenya halitatatuliwa na kukabiliwa, kuna shaka kuwa huenda vikundi vya wadudu hawa kusambaa katika maeneo tofauti nchini Kenya na kusababisha madhara makubwa. Hasa katika uharibifu wa chakula na kupelekea katika uhaba wa chakula nchini. Nzige wa kike ana uwezo wa kutaga mayai hadi 158 kila mara na wana uwezo wa kutaga mara zisizo pungua tatu maishani mwao. Nzige wana uwezo wa kuishi kwa muda wa miezi mitatu hadi mitano kulingana na hali ya anga na kuwepo kwa chakula. Janga la nzige huenda likasumbua kwa zaidi ya karne moja kwani wana uwezo wa kutaga mayai mengi na kuzaana kwa wingi.

Iwapo wadudu hawa wana athari nyingi, hakuna ushuhuda wa wao kuathiri watu ama wanyama na wala hawasemekani kubeba maradhi mabaya. Kukubana na janga hili huwa bei ghali. Katika mwaka wa 2003-2005 dola ($) millioni 450 zilitumika kukabiliana na nzige wa jangwani ambao walisemekana kusababisha hasara ya mimea ya dola ($) bilioni 2.5. Mtaalum mmoja alisema kuwa janga la nzige ni kama moto, ukiligundua lingali change hivi ndo la anza una uwezo wa kuliangamiza hadi likaisha. Ila, ukiligunduwa likiwa limesambaa, ni vigumu kubaliana nalo. Wadudu hawa wataisha pale ambapo wanakikosa chakula.
Kulingana Shirika la Mataifa (UN), zaidi ya watu milioni 24 yanakumbana na uhaba wa chakula na janga hili la nzige. Huenda watu zaidi ya milioni nane wakahitaji msaada wa chakula. Hili limekuwa janga kuu kabisa la wadudu hawa ambalo limeshuhudiwa. Nchi ya Somalia ilitangaza janga la nchi. Na kuitisha msaada wa chakula kutoka kwa watu wa wema mzuri. Kama ilivyo kwa wasaa huu, Nchi ya Kenya ina tatizo la kukabiliana na tatizo hili. Kwa sababu hii, shirika la UN linajaribu kuingilia kati na kutatua tatizo hili, kabla ya maafa zaidi kusababishwa na wadudu hawa kusafiri katika maeneo mengineyo.

Mbali na nchi za Afrika Mashariki ambako janga hili limeshuhudiwa kwa wingi, makundi ya nzige wameshuhudiwa katika nchi zingine kama vile Pakistan, Iran, na pia India. Kuna shaka kuwa vikundi hivi vya nzige hawa wa jangwani wataingia sehemu za Uganda na Sudan ya kusini. Ni matumaini yetu kuwa janga hili la nzige Kenya litatatuliwa.