Watu Mashuhuri Wanao Wasaidia Walio Athirika Na Covid-19

Watu Mashuhuri Wanao Wasaidia Walio Athirika Na Covid-19

Watu wengi wamejaribu kufanya kadri wawezavyo kusaidia watu walio athirika na janga la covid-19.

Janga la homa ya corona lime athiriwa maisha ya watu wengi duniani kote, na kufanya biashara ziwe na mapato madogo na zingine hata kufungwa. Ili kupunguza mzigo huu kwa watu, mwigizaji wa Nigeria Toyin Abraham anatoa msaada kwa wananchi kutoka sehemu tofauti huko Nigeria. Mwigizaji huyu ni mojawapo wa watu ambao wanatoa msaada katika janga la virusi vya Covid-19 kwa watu nchini kote.

Mshindi wa AMVCA ambaye pia amewaelimisha wafuasi wake kuhusu virusi vya homa ya corona; na wakati huo huo kutuma bidhaa za vyakula na vitakasio vya mikono kwa waliolemewa. Aliwatumia bidhaa watu katika pande za Ibadan, Ilorin, Abeokuta na miji mingine.

 

janga la virusi vya covid-19

"Habari zenu, natafuta watu waaminifu ambao ningependa wanisaidie na jambo hili. Nitakutumia hela, ila lazima akaunti yako iwe yafanya kazi na hizi zita angaziwa katika kila hatua ya safari hii. Tafadhali wacha ujumbe mfupi hapa," aliandika kwenye kurasa yake ya mtandao wa Instagramu.

Toyin Abraham ni mojawapo ya wana Nigeria wengi wanatoa msaada katika janga la virusi vya Covid-19

Mwigizaji huyu na mama wa mtoto mmoja aliongea na wauzaji wanao uza mchele na mitakasio ya mikono, ambao wangesaidia kuwapelekea watu katika miji ya Lagos, Ibadan, Akure, Ogun na Ilorin.

 

View this post on Instagram

 

#Repost @mansurah_isah with @make_repost ・・・ BLESS YOU AND YOUR FAMILY. WHAT A GESTURE. @toyin_abraham NOLLYWOOD Actress Donated 200k ( two hundred thousand naira ) to get some food items and detergent for Kano state less privilege. Thank you so much. More success and more happiness in your life. I think she spent more than a million today trying to support people across the #NATION STARTING FROM #IBADAN #KANO #ILORIN #LAGOS AND OTHER STATES. HER OWN GESTURE TO SUPPORT THE NATION AT LARGE ?? and help the GOVERNMENT IN CONTAINING THE #CORONAVIRUS #COVID_19 . AM SPEECHLESS RIGHT NOW. THANK YOU. We want more of you. Lets do this Inshaa Allah. #savethenation #stopcororna #akeelahthemovie #putasmileonthatface #peace #love #hope #support #futureassured #todayslifefoundation #notohunger #endhunger #coronapendamic #fateofalakada #who #unicef #unitednation #smile

A post shared by TOYIN ABRAHAM??????? (@toyin_abraham) on

Watu mashuhuri wanao wasaidia watu wakati huu wa janga la virusi vya Covid-19

janga la virusi vya covid-19

Baadhi ya watu wengine mashuhuri wa Nigeria walikuwa wanafanya wawezavyo kusaidia mwananchi wa kawaida katika nyakati hizi ngumu za kujitenga kufuatia virusi vya corona. Watu hawa mashuhuri wametuma pesa kwa wafuasi wao ili wanunue vyakula, wengine wao wali watumia watu vyakula ili wasitaabike kwenda kununua vyakula.

Mwimbaji mashuhuri anaye julikana kote Peruzzi ni mojawapo wa watu wanao ongoza katika wakati huu wa janga la virusi vya corona. Mkuu huyu amekuwa akiwapa wana Nigeria N10,000 za chamcha. Wengi wamepokea pesa hizi na bado mwimbaji huyu anaendelea kuwatumia wengine.

Mwimbaji mwingine mashuhuri aliye kuwa akiwapa watu pesa katika kipindi hiki cha corona na kujitenga ni mwimbaji wa Nigeria Douglas Agu maarufu kama Runtown. Nyota huu wa muziki amekuwa akitumia mtandao wake wa kijamii wa @iRuntown. Wafuasi wengi wake walimshukuru  baada ya wengi wao kupata kiwango cha pesa kutoka N25,000, N20,000, na N15,000.

Mashuhuri wa mtandao wa kijamii na mwigizaji Tunde Ednut pia alikuwa anapeana pesa kwa kurasa yake ya Twitter @tundeednut. Watu wengine wengi pia wanajaribu kadri iwezekanavyo kufanya wawezavyo katika wakati huu mgumu.

Kitendo cha kuwasaidia walio lemewa katika kipindi hiki ni jambo la kusifika.

Iwapo unaona kuwa una ishara za COVID-19, tafadhali piga nambari za wizara wa afya zifuatazo. 

  • Nambari ya kupiga bure: 0800 721 316
  • Whatsapp: +254-29- 471 414
  • Nambari ya ujumbe mfupi: +254-20-2717077/ 719

Hakikisha kuwa una zingatia umbali unao takikana na uwe salama. Je, una maswali yoyote? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mfupi hapa.

Legit NG

Soma pia: How To Prep Your Meals During COVID-19 Including 5 Sumptuous Recipes

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio