Jangamizi La Virusi Vya Korona

Jangamizi La Virusi Vya Korona

Sherehe maarufu za likizo ya Luna New Year imeahirishwa kufuatia ibuko la virusi vya korona nchini Uchina. Inasemekana kuwa virusi hivi vilianza mji wa Wuhan na kusababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja (100) na nambari hii inaendelea kuongezeka. Watu walio ambukizwa ni zaidi ya elfu tatu (3,000). Madaktari huko Uchina wanahofia kuwa nambari hii itaongezeka na wanaji tayarisha vilivyo kukumbana na virusi hivi.

Virusi hivi vinasemekana kuwa katika familia kubwa ya virusi vinavyo adhiri wanyama kwa sana. Ila, virusi hivi viliweza kuwa adhiri wanadamu tofauti na inavyo aminika.

virusi vya korona

Nchi nyingi zinaendelea kudhihirisha iwapo virusi hivi vya korona vimefika waliko

Kulingana na Shirika la Afya Duniani kote WHO, inasemekana kuwa ingawa virusi hivi vinaendelea kutamba, ni mapema sana kusema kuwa hili ni janga linalo adhiri dunia yote.

Kenya

Kuna shaka kuwa huenda virusi hivi vikawa nchini ya Kenya tayari kufuatia kisa cha msafiri mmoja aliyerudi nchini baada ya safari kutoka Guangzhou aliye dhibitisha kuwa na ishara za homa na mafua. Msafiri huyu alitengwa na kuwekwa katika Hospitali Kuu ya Kenyatta. Na baadaye kuachiliwa baada ya vipimo mwafaka kufanywa na kudhibitisha kuwa hakuwa na virusi hivi. Balozi la Uchina nchini Kenya linafuatia kwa umakini wachina wanao ingia nchini ili kuhakikisha hawana virusi hivi.

Ethiopia

Nchi hii ina urafiki wa kikaribu na Uchina. Watu wanne wametengwa kufuatia shaka kuwa huenda wana virusi hivi. Watatu miongoni mwao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Wuhan. Hatua zimechukuliwa kuhakikisha kuwa kila mtu anayeingia nchini hiyo anakaguliwa kuhakikisha hawana virusi hivi vya korona.

Sri Lanka

Inasemekana kuwa mwanamke mmoja aliye enda matembezi huko Uchina na kurudi tarehe 25 mwezi wa kwanza, alisemekana kuwa na virusi hivi baada ya vipimo kufanywa.

Amerika

Kulingana na Kituo cha Magonjwa na Kujikinga (Centers for Disease Control and Prevention CDC), watu watano wameadhiriwa na virusi hivi na nambari hii inasemekana kuwa itaongezeka huko Amerika.

Cambodia

Kisa cha kwanza kilicho shuhudiwa cha ugonjwa huu ni cha mwanamme aliye tembea pwani mwa nchi hii na familia yake kutoka mji wa Uchina wa Wuhan. Ambapo virusi hivi vinasemekana vilianza. Mwanamme huyu alianza kuhisi joto jingi ila inasemekana kuwa hali yake iko salama kwa sasa.

South Korea

Watu wanne wame semekana kuwa na virusi hivi. Kisa cha mwisho kikiwa cha mzee wa miaka 55 aliye rudi kutoka matembezi mjini wa Wuhan.

Watu wanao tembea katika mji wa Wuhan huko Uchina wanashauriwa kufanyiwa vipimo vya kiafya mara kwa mara kuhakikisha kuwa wako salama na wala hawaugui virusi hivi.

Mambo muhimu ya kujua kuhusu virusi vya korona

Tangazo la dharura kutoka kwa wizara ya afya ni kuwa virusi hivi ni hatari sana. Na kuwa hakuna matibabu bayana yanayo julikana. Watu wanashauriwa kuhakikisha :

  • Kuwa koo zao hazijakauka. Kwani virusi hivi vitaingia mwilini mwako kabla ya muda wa dakika kumi kuisha.
  • Kunywa maji vuguvugu 50-80cc na 30-50 cc kwa watoto
  • Hakikisha kuwa unakunywa maji kwa wingi na wakati wote
  • Epuka kuenda kwa umati wa watu ama mahali kunako kuwa na watu wengi.
  • Epuka kula vyakula vilivyo na pilipili nyingi na ukijaze chakula chako na vitamini C.

Ishara za virusi hivi ni kama vile:

  • Jongo jingi mwilini
  • Kukohoa sana
  • Kuumwa na kichwa
  • Shida ya kupumua

Athari za virusi vya korona

Kufuatia habari za ugonjwa huu, soko ya za forex trade na stocks zimeendelea kudidimia na kuanguka kufuatia woga wa virusi hivi kutamba.

Bei ya dhahabu duniani kote imeongezeka. Utalii nchini hii umedidimia na hoteli na kampuni za kitalii zimeshuhudia hasara kubwa wichi chache zilizo pita kufuatia habari hizi.

Usafiri kuenda na kutoka nchini hii ume punguzwa ili kuhakikisha kuwa virusi hivi havienezwi kwa sana na kupunguza idadi ya watu walio athirika.

Nchi ambazo zina wananchi wanao ishi katika mji wa Wuhan, wameanza mazungumzo na serikali ya Uchina kuona watakavyo wahamisha wananchi wake na kuwapeleka miji iliyo salama.

Nchi zinazo karibiana na Uchina kama vile Mongolia vimefunga mipaka yake na kukataza watu na magari kupita mipaka wakielekea Uchina. Vyuo vimefungwa hadi Mechi tarahe 2 ambapo vitafunguliwa baada ya hatua zinazofaa kuchukuliwa kuhakikisha watu wake hawaambukizwi na virusi hivi vya korono. Serikali ya nchi hii inasema kuwa watu walio utembelea mji wa Wuhan watakatazwa kurudi nchini kabla ya kudhibitisha kuwa hawana virusi hivi vinavyo ua.

Huduma ya afya ya Uchina inasema kuwa imetenga dola bilioni 9 kukabiliana na jangamizi hili. Kulingana na serikali yake, hospitali itajengwa kwa muda wa siku tisa kukabiliana na janga la virusi hivi.

 

 

Written by

Risper Nyakio