Nini Unacho Kifahamu Kuhusu Neonatal Jaundice Kwa Watoto Wachanga?

Nini Unacho Kifahamu Kuhusu Neonatal Jaundice Kwa Watoto Wachanga?

Jaundice is a common and usually harmless condition in newborn babies that causes yellowing of the skin and the whites of the eyes.

Neonatal jaundice kwa watoto wachanga ni jambo la kawaida. Hii ni hali inayo badilisha rangi ya ngozi na macho ya mtoto na kuwa njano, siku kadhaa baada ya kuzaliwa. Watoto hupatwa na kiasi kidogo cha ugonjwa huu siku kadhaa baada ya kuzaliwa. Kwa watoto waliozaliwa mapema ugonjwa huu inaweza jitokeza mapema na kukaa kwa muda mrefu kuliko watoto waliozaliwa baada ya miezi kamili kuisha.

Kiwango cha mtoto cha bilirubin kikizidi kupita kiwango cha kawaida, huenda mtoto akapata matatizo ya kimwili kama vile kuharibika kwa akili, kutosikia na cerebral palsy.

Nini kinacho sababisha neonatal jaundice kwa watoto wachanga

Nini Unacho Kifahamu Kuhusu Neonatal Jaundice Kwa Watoto Wachanga?Jaundice ina sababishwa na watoto wachanga kutoa kiwango cha juu cha bilirubin. Madaktari wanaita hali hii "physiological jaundice." Bilirubin ina rangi ya njano inayo tolewa punde mwili unapovunja seli nyekundu zinazo tengeneza damu. Kwa watoto wachanga, mwili inatoa bilirubin kwa kiwango cha juu zaidi na maini yanashindwa kuchakata.

Jaundice ya kifonologia inaonekana siku chache baada ya kuzaliwa na inatibika kwa muda wa wiki mbili. Kuna aina mbali mbali za jaundice za watoto wachanga na huenda zikawa ni juu ya kutokua. Matatizo yanayo husika na kunyonyesha, maambukizo, aina ya damu kuwa tofauti kati ya mama na mtoto, na matatizo mengine ya maini na damu.

Kwani wamama wengi na watoto hutoka hospitalini punde tu baada ya kujifungua, jaundice huenda isionekana hadi pale mtoto anapokuwa nyumbani. Ni muhimu sana kwa mtoto mchanga kuangaliwa na mtaalam wa watoto. Jambo hili linapaswa kutendeka siku chache baada ya kwenda nyumbani kuhakikisha kuwa mwanao hana jaundice.

Ni muhimu kumshughulisha daktari wako unapo ona ishara zozote za jaundice kwenye mtoto. Iwapo una shuku jaundice, hakikisha umemtembelea daktari wako siku hiyo. Huku jaundice ikiwa ni hali inayo weza kutibika, kwa kesi zilizo zidi, inaweza sababisha kuharibika kwa ubongo.

Habari nzuri ni kuwa katika visa vingi, jaundice ya watoto wachanga huisha bila matibabu yeyote. Inafanyika maini ya mtoto wako yanapo endelea kukua na mwanao anaanza kukula. Inasaidia bilirubin kupita mwilini.

Watoto walio katika hatari zaidi ya kupata jaundice kwa watoto wachanga ni:

Nini Unacho Kifahamu Kuhusu Neonatal Jaundice Kwa Watoto Wachanga?

 • Watoto walio zaliwa kabla ya wakati (kabla ya wiki 37 za gesti)
 • Wale ambao hawa nyonyi vya kutosha kwa sababu wana ugumu wa kunyonya ama maziwa ya mama hayatoshi
 • Wana ambao aina ya damu yao ni tofauti na ya mama yao

Kinacho sababisha neonatal jaundice kwa watoto wachanga ni kama vile:

 • Kuumia unapo jifungua ama kutoka damu kindani
 • Matatizo ya maini
 • Maambukizo yoyote
 • Ukosefu wa kimeng'enya
 • Shida za seli nyekundi za mtoto wako
Je, ni nini ishara za neonatal jaundice?

Dalili ya kwanza ni kubadilika kwa rangi ya ngozi na macho ya mtoto na kuwa njano. Rangi hii Unaeza anza kujitokeza Siku 2-4 baada ya kuzaliwa na inaweza kwa uso kisha kuenea katika sehemu zingine za mwili. Kiwango cha Bilirubin huanza kupanda Siku 3-7 baada ya kuzaliwa. Ukifinyilia kidole katika ngozi ya mtoto kisha uone rangi ya njano kumaanisha kuwa kuna uwezekano wa Jaundice.

Je, madaktari wanatumia mbinu ipi kupima neonatal jaundice?

Rangi ya njano inaonyesha kwamba ni Juandice lakini lazima wapime ili waweze kujua kiwango cha ugonjwa huo.Watoto wanaopata Jaundice masaa 24 baada ya kuzaliwa wanapaswa kupimwa viwango vya Biliburin kupitia kipimo cha ngozi au cha damu.Daktari watahitaji kufanya vipimo vingine ili kudhibitisha kuwa haisababishwi na shida zingine za kimwili. Vipimo hivi ni kama CBC(complete blood count), Rhesus factor(Rh), aina ya damu na vitu vinginezo.Kipimo cha coombs hufanywa kuangalia ongezeko la seli zinazo tengeneza damu.

Jinsi ya kutibu jaundice katika watoto

jaundice katika watoto wachanga

Tiba ya picha (phototherapy) Ni njia tmya kawaida na inayosaidia kutibu Jaundice kwa kutumia mwangaza ili kuvunjwa Bilirubin iliyo ndani ya mwili wa mtoto.Katika tiba hii ya mwangaza wataekelea mtoto wako kitandani chini ya mwangaza wa samawati bila nguo ila miwani ya kuzuia kuchomeka na mwangaza ule, mara zingine wanaeza ekelea blanketi.Kwa tukio zingine daktari hupendekeza mtoto aekwe damu nyingine kwa kiasi kidogo kidogo. Damu hii inabadilisha damu ile iliyomo ndani ya mtoto iliyoharibika.Hii inaongeza na kutengeneza seli mpya za kutengeza damu na na kupunguza kiwango cha bilirubin.

Je, unaeza kuzuia Jaundice kwa watoto wachanga?

jaundice kwa watoto wachanga

Hakuna njia haswa ya kuzuia ugonjwa huu. Unapokuwa na mimba, ni muhimu kuhakikisha unapata kipimo cha damu.

Baada ya kujifungua, madaktari watapima aina ya damu ya mtoto wako, iwapo kuna umuhimu. Hii ni kutoa uwezekano wa kutofanana kwa damu ya mama na mtoto ambayo inaweza sababisha jaundice kwa mtoto. Kuna njia za kuzuia isiwe hatari:

 • Hakikisha kuwa mtoto wako anapata lishe bora kupitia kunyonya. Kunyonyesha mtoto mara 8-12 kwa siku kunahakikisha kuwa mtoto wako hakosi maji mwilin. Inasaidia bilirubin kupitia mwilini kwa urahisi.
 • Kama hanyonyi hakikisha kwamba unampa fomula ya watoto. Mpe kipimo cha 1-2 katika kila Masaa 2-3 wiki ya kwanza ya kuzaliwa. Watoto waliozaliwa kabla ya muda watakunywa vipimo vidogo.
 • Ongelesha daktari wako kama mtoto wako anachukua kipimo kidogo ama zaidi sana cha fomula ya watoto ama wasipo amka mara nane kwa masaa 24.

Tathmini mtoto kwa makini kwa Siku tano baada ya kuzaliwa ili kujua kama ana ugonjwa wa Jaundice kama rangi ya njano kwa macho na ngozi.

Iwapo unaona ishara zozote za jaundice katika mtoto wako, mpigie daktari wako bila kukawia.

WebMD

Also read: Could jaundice protect newborns from sepsis? New research thinks so

Written by

Risper Nyakio