Keto Kwa Watoto: Je, Lishe Ya Keto Ni Salama Kwa Watoto?

Keto Kwa Watoto: Je, Lishe Ya Keto Ni Salama Kwa Watoto?

Is keto safe for kids? Dietitians weigh in on the safety of keto for kids, including whether keto is a good choice for overweight kids and how many carbs a child needs.

Utaratibu maalum wa kula wa keto unahusisha kabohidrati kiasi kidogo ili kusaidia kusimamia na chakula chenye kiwango cha juu cha mafuta. Kwa miaka mingi ina faida nyingi za kiafya. Lakini keto ni salama kwa watoto wetu? Na ni suluhu kwa wazazi wanaojaribu kusaidia watoto wao ambao wamezidi kipimo cha kilo na wanajaribu kupunguza kilo kadhaa na kusitiri afya.

Miaka ya hivi karibuni, wataalam walitumia utaratibu huu wa kula wa keto kusaidia kusimamia hali zingine za kiafya kwa watoto. Hii inahusisha ugonjwa wa kifafa na saratani ya akilii. Ilhali utaratibu wa kula wa keto ni salama kwa watoto, lakini haihusishi watoto na vijana. Isipokuwa umeagizwa na daktaro na sababu za kiafya.

Keto ni salama kwa watoto wetu? Ujumbe huu unaangalia usalama wa utaratibu huu swa kula wa keto kwa watoto na vijana, na pia kuangazia matumizi na madhara yake.

je, keto ni salama kwa watoto

Utaratibu wa kula wa keto ni nini na keto ni salama kwa watoto wetu?

Utaratibu huu wa keto ulianzishwa katika mwaka wa 1920; kama dawa ya kifafa na ungetumiwa kwa kutathminiwa kwa kiafya kwa makini. Hivi karibuni, keto imejulikana kama utaratibu wa kula unaosaidia kabohidrati inayojumuisha kiwango cha kawaida cha protini.

Watoto wanaofuata utaratibu huu wa keto wanakula chakula ambacho kina kiwango cha juu cha mafuta lakini hawapunguzi kiwango cha protini. Mifano ya chakula zinazoliwa mtu anapofuata utaratibu huu wa kula ni kama samaki, mayai, njugu, jibini, soseji, avocado, krimu na mboga za rangi tofauti tofati.

Unapofuata utaratibu huu unahusisha kiwango kidogo cha mkate, wali, matunda, nafaka na switi.

Utaratibu huu wa kiwango cha chini cha kabohidrati na kiwango cha juu cha mafuta ina madhumuni ya kuweka mwili katika hali ya ketosis. Kwa kawaida kabohidrati tunazozila zinavunjika na kuwa vipengele vidogo vya sukari vinavyojulikana kama glukosi ambazo mwili hutumia kama nguvu. Lakini ikupunguza kabohydrati, mwili hautaweza kusaidia kutengeza sukari ya kutosha, na hii ikifanyika, mwili unabadilisha mafuta na kuwa shina la kutoa nguvu inayohitajika mwilini na kutoa kipengele kinachoitwa ketone. Wakati ambapo kuna kiwango cha juu cha ketone katika damu, mwili uko katika hali ya ketosis

Mwili kwa kawaida unafikiria kwamba umekosa chakula, kwa hivyo unabadilisha mafuta kama asili nyingine ya kutoa nguvu. Na hii ndio maana mtu hupunguza kilo.

Keto Kwa Watoto: Je, Lishe Ya Keto Ni Salama Kwa Watoto?

Kwa nini keto haipendekezwi kwa watoto na vijana

Wataalam hawapendekezi utaratibu huu kutumika na watoto na vijana kwa sababu kabohadrati. Na watoto wanahitaji kabohyadrati ili kukua kiakili na kimwili. Watoto ambao wanafuata utaratibu wa kiafya wa kula wanapaswa kula gramu 130 za kabohyadrati kwa siku. Hiki ni kipimo cha 45-65% cha kalori ilhali keto inapunguza kabohyadrati hadi gramu 20-30 kwa siku.

Chakula kilicho na kiwango cha juu cha kabohyadrati kinachoitwa nyuzi (fiber) zinakusaidia uskie umeshiba na kusaidia kudhibiti kilo zako au kupunguza kwa kilo. Nyuzi zinazopatikana katika mboga, matunda na nafaka husaidia ili kudumisha sukari ya damu na kuzuia kukaukiwa unapoenda msalani. Kabohyadrati zinatusaidia na nguvu na virutubisho vingine vinavyohitajika. Watoto wanahitaji kabohidrati ili kukua na kuweza kufanya kazi yao ya ziada na kuweza kucheza.

Madhara ya utaratibu wa kula wa keto kwa watoto

Keto Kwa Watoto: Je, Lishe Ya Keto Ni Salama Kwa Watoto?Wakati ambapo mwili unapitia ketosis, watoto na watu wazima wanaweza kuwa dalili fulani za:

 • Kuendesha
 • Uchovu
 • Kujikuna
 • Kuskia kusunzi
 • Kuhisi kutapika

Madhara haya yanafanyika sababu mwili unafikiria kwamba mtu hauna chakula, hii ina adhiri umakini wa mtu na kukosa kwa virutubisho vinavyosaidia mtu, na pia kusababisha kiwango cha juu cha cholesterol na triglycerides, mifupa isiyo na nguvu na shida ya figo.

Mbinu za kupunguza kilo badala ya kutumia utaratibu wa keto

Je, keto ni salama kwa watoto?

Kwa watoto na vijana wanao kusudia kuwa na uzito unaofaa, wataalamu wanashauri kuwa na utaratibu unao faa wa lishe bora. Wana shauri mbinu zifuatazo:

 1. Kula vyema na chakula bora

Ili kuwapa watoto chakula kingi ambacho kina virubutisho vingi, wape chakula bora. Ukitengeza sahani iliyo na chakula bora kila wakati utakuwa unafanya kazi njema. Kama kilo za mtoto wako zi juu au la, angalau unawapa virutubisho wanavyohitaji ilikukua.

 1. Punguza chakula cha dukani na chakula kilicho ongezwa sukari

Chakula kama hiki ni kama vile soda, kuki, vitindamlo na viazi karanga na bidhaa za kuokwa.

 1. Chagua vitafunio vyenye lishe

Hakikisha kwamba watoto wanakula vitafunio kwa wakati ambao unafaa, na uchague mbinu ambazo ni salama kiafya. Wape motisha wa kula chakula kwa viwango vidogo vidogo vinavyokuwa na vikundi viwili au zaidi ya chakula. Kwa mfano jaribu sandwichi ya njugu nusu na mkate kisha mboga

 1. Kuwa na maoni mazuri na umpe mtoto wako ujumbe

Elezea mtoto wako kuwa ni vyema kula chakula ambacho kitamsaidia kukua na kumpa nguvu siku yote siku mzima. Kwa mfano waambie ‘unataka kula mboga na matunda sababu zina fanya uwe makini shuleni, nguvu ya kucheza na kukufanya uskie vizuri.

 1. Usitilie maanani kilo za mtoto

Watoto wanakuja na njia tofauti wengine wakubwa wengine wadogo, kile ambacho ni muhimu jinsi ambavyo mwili wetu unafanya kazi, vile tunavyohisi au mtoto ako sawa kiafya au la

 1. Wape chakula kipya mara kwa mara

Hata kama mtoto hakupenda chakula Fulani mwaka mmoja uliopita wapatie tena kwani jinsi chakula huonja kwa watoto hubadilika wakikomaa.

 1. Wape motisha wa kuchagua jambo wanalolipenda

Kutembea, kukimbia, kuendesha baiskeli. Kama mtoto wako anapena michezo ya video watafutie ile ambayo inahitaji wawe hai. Tafuta mchezo wanaopenda. Washa muziki, piga densi.

 

Huffpost

Also read: 10 Cancer-Causing Foods You Probably Eat Every Day

Written by

Risper Nyakio