Baada ya yai kurutubishwa, huchukua muda wa siku sita kujipandikiza kwenye uterasi. Hapo mwanamke husemekana kuwa amebeba mimba. Lakini kujua kwa uhakika kama uko na ujauzito unafaa kupima aidha nyumbani ama kwenye hospitali. Makala haya yanaangazia jinsi ya kufanya kipimo cha mimba.
Jinsi Ya Kufanya Kipimo Cha Mimba

Mara baada ya yai na manii kukutana, maumbile mbalimbali yanaunganika kutengeneza seli mpya. Seli hii mpya inagawanyika haraka na kila seli mpya iliyoundwa kugawanyika tena kuwa kiini-tete. Baadhi ya seli mpya ndani ya kiini-tete hukua na kufanyika plasenta ya mtoto. Hii plasenta ya mtoto huanza kutengeneza homoni inayoitwa Human Chorionic Gonadotropin (HCG).
Mara tu kiini-tete kinapojipandikiza kwenye uterasi, ndipo mtu hujulikana kuwa mjamzito. Utengenezaji wa homoni HCG huongeza kwa wingi na hii homoni huamrisha mwili kuachisha hedhi. Kiwango cha HCG huzidi kuongezeka kadiri kiini-tete kinavyozidi kukua na plasenta yake inavyoendelea kukua.
Vipimo vya mimba hulenga kutambua uwepo wa hii homoni kwenye mkojo. Hili hutokea baada ya siku sita baada ya yai kurutubishwa. Hivyo kufanya kipimo mapema sana unaweza pata majibu yasiyo sahihi. Pamoja na kuwa kipimo hiki ni rahisi na cha faragha pia ni cha haraka.
Kuna Njia Mbili za Kupima:
- Weka mkojo wako kwenye kikopo safi kisicho na mafuta ama kemikali. Kisha weka sehemu ya kupimia kwenye mkojo wako
- Shika sehemu ya kupimia ya kipimo chako kisha ukiwa unakojoa kiweke kwenye mtiririko wa mkojo ili kilowane
Baada yake subiri kwa muda mchache ili kupata majibu. Haya huonekana kwa kutokea kwa mistari miwili yenye rangi au kwa alama ya chanya(+) au hasi (-). Vipimo vya kigiditali huonyesha neno (pregnant) ujauzito au (not pregnant) hakuna ujauzito. Unaweza kununua vipimo vya ujauzito bila kuelekezwa na daktari katika maduka ya dawa au mtandaoni.
Lini Nifanye Kipimo Cha Ujauzito?
Ni vyema kusubiri baada ya siku moja baada ya Kukosa siku zako za hedhi. Hivyo utaepuka majibu ya uongo. Ikiwa mzunguko wako wa hedhi haueleweki, usifanye kipimo hadi utakapopita mzunguko mrefu unaokuwaga nao. Kipindi chako cha hedhi kinapochelewa kwa wiki au wiki mbili utaweza kupata majibu sahihi.
Wakati Gani Wa Siku Ni Mzuri Kufanya Kipimo?
Majibu sahihi kabisa huweza kupatikana asubuhi. Kipimo cha nyumbani hufanya kazi kwa kutambua homoni HCG kwenye mkojo. Mkojo wako wa asubuhi utakuwa na viwango vikubwa vya hii homoni isipokuwa kama uliamka usiku kujisaidia ama ukanywa maji mengi.
Vipimo Vya Nyumbani Vina Uhakika?

Vipimo vya nyumbani vina uhakika kama utafuata maelekezo yalitolewa. Baadhi ya vipimo vina umakini wa kugundua haraka, rahisi kutumia na kutafsiri zaidi ya vingine. Umakini kugundua haraka katika kipimo ni mzuri zaidi maana unanyaka hata viwango vidogo vya HCG ndani ya mwili wako. Vipimo vya mimba vya kidigitali hutajwa kuwa na uhakika zaidi.
Utaelewa kuwa viwango vya HCG huripotiwa kwenye units za kamili(MIU) kwa milimita. Udogo wa namba katika kipimo ndio uharaka wa kipimo kugundua ujauzito. Hivyo basi kipimo kinachoonyesha 10mIU /ml ni makini zaidi kugundua ujauzito katika mkojo zaidi ya kipimo cha 40mIU /ml.
Vipimo vya ujauzito ni rahisi sana kupatikana na pia kusoma. Cha muhimu kabisa ni kuelewa jinsi ya kufanya kipimo cha mimba.
Soma Pia: Je, Manii Huenda Wapi Wakati Wa Ujauzito: Umuhimu Wa Ngono Katika Mimba