Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Je, Unajua Jinsi Ya Kupika Sima: Matayarisho Ya Ugali

2masomo ya dakika
Je, Unajua Jinsi Ya Kupika Sima: Matayarisho Ya UgaliJe, Unajua Jinsi Ya Kupika Sima: Matayarisho Ya Ugali

Chakula kinachosifika kwa sana hasa katika nchi za Afrika Mashariki. Sima inajulikana kwa majina tofauti kama vile ugali, sembe, ngunga, bondo ama nguna. Ugali huenda ukapikwa kwa kutumia mtama, uwele, muhogo, ama mahindi. Tuna angazia jinsi ya kupika sima.

kutayarisha ugali

Je, tunahitaji viungo gani kupika sima?

Sima ni mojawapo ya vyakula vilivyo rahisi zaidi kutayarisha. Unacho hitaji ni maji na unga wako utakao utumia. Kulingana na sembe unayo taka kutayarisha. Kama vile ugali wa unga wa mahindi, mtama ama muhogo. Aina ya ugali unayoitayarisha kwa kawaida inalingana na eneo unalo ishi. Kama vile, watu wanao ishi upande wa magharibi mwa nchi, wana utengeneza ugali wa mtama kwa mara nyingi. Watu wanao ishi eneo la katikati mwa nchi wanaipika sima yao kwa kutumia mahindi. Kwani mahindi yanapatikana kwa urahisi katika eneo hilo.

Pia kuna aina inayo julikana kama udaga ambao ni ugali unaotayarishwa kwa kuchanganya unga wa muhogo na ulezi. Unapatikana kw asana eneo la Musoma ambako jamii ya Wakuria inaishi.

Mahitaji:                                                                                    

Sufuria, Maji, Mwiko, Unga

sima

Kutayarisha:
  • Weka maji (kulingana na watu unao watayarishia) kwenye sufuria.
  • Yaekelee maji yako kwenye moto hadi yanapo chemka.
  • Ongeza unga wako kwenye maji haya.
  • Koroga ama usonge mchanganyiko huu kwa kutumia mwiko.
  • Kishe uupe mchanganyiko huu muda mdogo uive.
  • Endelea kusonga sima yako kwa dakika zisizo pungua 20.

Dude hili huliwa kwa vitoweo mbali mbali. Huenda ukakula sima kwa samaki ya kukaangwa ama kuchemshwa, omena, nyama ya ng’ombe, mbuzi, kuku, maharagwe ya nazi, ama mboga kama vile sukuma wiki, kabeji, kunde, mchicha ama mrenda.

Katika familia ya waswahili, dude hili linaliwa kwenye mkeka. Wanajamii wanauzunguka mkeka huu wakiwa wamekunja miguu kisha kukisherehekea chakula hiki.

 

Je, Unajua Jinsi Ya Kupika Sima: Matayarisho Ya Ugali

Sima kwa samaki

Kwa kawaida ugali huliwa kwa mikono, unalifinyanga ama kulibofya tonge la ugali na kutengeneza shimo katikati kisha kuchovya kwenye kitoweo chako. Ladha ya ugali ni kuila kwa mkono na ikiwa ingali moto. Baada ya kujua jinsi ya kupika sima, jaribu kuwatayarishia jamii na marafiki wako chakula hiki. Furahikia!

img
Yaliandikwa na

Risper Nyakio

  • Nyumbani
  • /
  • Meals
  • /
  • Je, Unajua Jinsi Ya Kupika Sima: Matayarisho Ya Ugali
Gawa:
  • Jinsi Ya Kutengeneza Dambu Nama

    Jinsi Ya Kutengeneza Dambu Nama

  • Jinsi Ya Kupika Wali Wa Nazi Kipwani!

    Jinsi Ya Kupika Wali Wa Nazi Kipwani!

  • Jinsi Ya Kupika Kitoweo Cha Nyama Ya Mbuzi

    Jinsi Ya Kupika Kitoweo Cha Nyama Ya Mbuzi

  • Jinsi Ya Kupika Supu Ya Konokono

    Jinsi Ya Kupika Supu Ya Konokono

  • Jinsi Ya Kutengeneza Dambu Nama

    Jinsi Ya Kutengeneza Dambu Nama

  • Jinsi Ya Kupika Wali Wa Nazi Kipwani!

    Jinsi Ya Kupika Wali Wa Nazi Kipwani!

  • Jinsi Ya Kupika Kitoweo Cha Nyama Ya Mbuzi

    Jinsi Ya Kupika Kitoweo Cha Nyama Ya Mbuzi

  • Jinsi Ya Kupika Supu Ya Konokono

    Jinsi Ya Kupika Supu Ya Konokono

Pata ushauri wa mara kwa mara kuhusu ujauzito wako na mtoto wako anayekua!
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • Zaidi
    • TAP Jamii
    • Tangaza Nasi
    • Wasiliana Nasi
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
Kutuhusu|Timu|Sera ya Faragha|Masharti ya kutumia |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it