Jinsi Kulala Kunavyo Saidia Na Homa

Jinsi Kulala Kunavyo Saidia Na Homa

Baadhi ya ishara za homa ni kama vile kukohoa, koo inayo uma, kuchemua, joto mwilini, kuumwa na kichwa. Soma zaidi upate kufahamu jinsi ya kuzipunguza.

Homa ni ugonjwa unao sababishwa na virusi na ku athiri mfumo wako wa kupumua. Kwa hivyo virusi vina husishwa na homa baridi ambayo mfumo wako wa kinga huenda uka shindwa kuji kinga dhidi yake. Baadhi ya ishara za homa ni kama vile kukohoa, koo inayo uma, kuchemua, joto mwilini, kuumwa na kichwa na mapua yaliyo fungana. Baadhi ya watu huenda waka kosa kushuhudia ishara hizi. Hii ni kwa sababu kila mtu ana mfumo wa kinga tofauti. Makala haya yana kuelimisha zaidi kuhusu jinsi kulala kunasaidia homa.

Jinsi kulala kunasaidia na homa

Wakati wowote ule unapo ugua homa, una pata hamu ya kukimbia kwenye zahanati kununua dawa kuponya ugonjwa wako. Lakini sote twafahamu kuwa haiwezekani kununua usingizi, kwa hivyo tuna shauri juhudi zako ziwekwe kwa kutafuta usingizi. Ni suluhu bora kwa homa. Ujumbe unao egemezwa na utafiti.

jinsi kulala kunasaidia homa

Utafiti uliofanyika kwa Chuo Kikuu cha California huko San Francisco una onyesha umuhimu wa kulala kwa kuponya na kuepusha kuugua homa. Mwanasaikolojia Aric Prather alitumia watu 164 kufanya utafiti. Ali tathmini mtindo wa kulala wa kila mmoja wao kwa wiki, kabla ya kuwa nyunyuzia virusi vya baridi kwenye mapua yao. Tofauti kati walio lala zaidi na walio lala kwa muda mfupi ulikuwa wazi. Utafiti ulionyesha kuwa asilimia 39 ya watu wazima walio lala kwa masaa 5 ama 6 kila usiku waligonjeka. Walio lala kwa vipindi virefu kama masaa 7-8 kila usiku waligonjeka.

Camilo A. Ruiz ambaye ni mkurugenzi wa kimatibabu katika Choice Physicians Sleep Center huko South Florida anasema kuwa usingizi unasaidia mwili kupigana dhidi ya virusi baridi kwa kasi. Unataka virusi viishe mbio na upone mbio.

Unapo kuwa na homa, huenda ukagundua kuwa hata mwili wako unakuambia ulale. Hii ni kwa sababu mwili unafanya kazi sana kupigana dhidi ya virusi na inachosha. "Baadhi ya watu hata wata kwambia, ninapo pata homa, nahisi kulala zaidi, " Camilo alisema. "Tuna fahamu kuwa maambukizi yanaweza athiri sehemu fulani za ubongo zinazo husiana na kuamka na kutahadhari. Kwa hivyo mwili wako haupigani dhidi ya maambukizi tu, inayo chosha, mbali unahisi kulala zaidi kwa sababu una virusi.

Jinsi ya kulala vyema ukiwa na homa

Ikiwa baridi inakufanya usilale, hapa chini kuna baadhi ya hatua ambazo zinaweza boresha nafasi zako za kulala vyema.

  • Kunywa chai iliyo yenye asili

does sleep help a cold

Asali hufanya vyema na kupunguza kikohozi. Pia, inaweza tuliza koo inayo uma. Kwa hivyo, hakikisha kuwa unakunywa chai iliyo na asali na itakufaa katika kuponya homa, na kukusaidia kulala vyema. Joto kutoka kwa chai itakusaidia kusafisha mfumo wako wa mapua.

  • Ongeza mto wako

Kuongeza mito yako kuna kusaidia kuinua kichwa chako. Kufanya hivi kutakusaidia kuepusha kamasi kushikana na kusababisha koo kushikana.

  • Oga kwa maji moto

Kutumia maji moto kuoga kuna timiza mambo sawa na kunywa maji moto. Ina saidia kusafisha mfumo wako wa mapua na kukusaidia kupumua vyema. Mbali na kuponya homa, kuoga kabla ya kulala kuna ongeza nafasi zako za kulala vyema.

  • Tumia kisafisha hewa (humidifier)

Watu walio na homa hawafanyi vyema kupumua hewa iliyo kauka. Kifaa hiki kina weza tatua tatizo hili. Kifaa hiki kina ongeza unyevu nyevu kwenye hewa na kufanya hewa unayo nusa isiwe ime kauka sana. Lakini utakuwa una jihatarisha zaidi ikiwa kifaa chako ni kichafu. Kita ongeza vumbi zaidi na bakteria kwenye hewa. Kwa hivyo hakikisha kuwa wakati wote ni kisafi.

Hitimisho

Kwa watu ambao wanatumia dawa za kununua kwenye zahanati kuponya homa, dawa nyingi za homa ni nyingi. Kwa hivyo angalia zinazo angazia zaidi kwa ishara zako kabla ya kununua.

Soma Pia:Kulala Sana Kuna Athari Hasi Kwa Afya Yako

Written by

Risper Nyakio