Jinsi Ambavyo Tende Huongeza Idadi Ya Manii Na Faida Zake Kwa Wanaume

Jinsi Ambavyo Tende Huongeza Idadi Ya Manii Na Faida Zake Kwa Wanaume

Viwango vya chini vya manii vimehusishwa na kukosa zinc ama vitamini muhimu. Kwa hivyo kufanya mabadiliko ya chakula na kuongeza tende katika lishe yako ni njia nzuri ya kuongeza viwango vyako vya manii mwilini.

Bila shaka tende ni mojawapo ya matunda yaliyo kauka yenye ladha zaidi na yanayo patikana mwaka wote. Zina wingi wa virutubisho, watu wanakula matunda yaliyo kauka mara nyingi ili kupata nishati. Hii ndiyo sababu kwa nini wakati wa Ramadan, waislamu huvunja kipindi chao cha kutokula na tende. Kwa sababu kuto kula hunyima mwili wako nguvu, kula tende kuna saidia kuimarisha nishati yako mwilini. Zina uwezo wa kuboresha zaidi ya viwango vyako vya nishati, Sayansi ina shauri kuwa tende zinaweza boresha hamu yako ya kufanya mapenzi; kuboresha ubora wa manii na kuilinda ndoa yako. Utafiti umedhihirisha kuwa maarifa ya kale yame kuwa yakisema hivi wakati huu wote. Tende zina boresha maisha yako ya mapenzi kwa kuongeza hamu yako ya kufanya mapenzi na kuboresha uwezo wako wa kufanya matendo ya kitandani. Pia, kulingana na Sayansi, tende zina ongeza viwango vya manii, na hii ni sababu ingine kwa nini wanaume wanapaswa kula tende mara kwa mara.

Je, tende zinaongeza vipi viwango vya manii? Tazama utafiti uliofanyiwa na wataalum hapa chini.

Jinsi tende zinavyo ongeza kiwango cha manii

dates increase sperm count

Madaktari wa hapo awali walitumia pollen ya tende kutengeneza dawa za kuponya kukosa watoto. Kutumia ujuzi huo, wataalum na watafiti walifanya uchunguzi zaidi kuhusu tende.

Kulikuwa na utafiti wa majaribio ulio ongozwa na Bahmanpour et al. mwaka wa 2006. Watafiti waligundua kuwa tende zilikuwa na athari kwa mfumo wa uzalishaji wa panya nzima, walio tumika kwenye majaribio haya. Wana sayansi walitambua kuwa, kula tende kuliongeza viwango vya manii. Pia ziliongeza uzito wa testes na epididymis kwa sababu ya estradiol na flavanoid inayopatikana kwenye tende.

Pia, mwaka wa 2016 Novemba, wataalum wawili katika afya walishauri wanaume kula tende; na kusema kuwa ulaji wake unge boresha matendo ya kingono na kuongeza afya ya kufanya mapenzi.

Mwanamme huyo aliambia News Agency ya Nigeria (NAN) kuwa wanaume wanapo kula tende ipasavyp, wanaweza boresha hali zao za afya kwa njia nyingi. Pia inaweza ondoa aibu za kuto watosheleza wachumba wao kimapenzi, wataalum walisema.

Moja wa wanaume hao, Daktari. Aminu Kazeem, ambaye ni daktari wa mambo ya ngono anaye fanya kazi katika kliniki ya Lagos; alisema kuwa wanaume walio kuwa na matatizo ya kuwatosheleza wachumba wao kingono wanapaswa kula tende.

"Kula tende kuna boresha ubora na wingi wa manii kwani ni mojawapo ya matunda asili bora zaidi yanayo tumika kuboresha uzazi wa kiume. Pia zinaongeza saizi ya kibofu cha mwanamme na saizi ya chuchu za mwanamke. Kula matunda haya yana wezakusaidia kutibu changamoto za kingono."

Alizidi kudhihirisha kuwa tende zina viwango vya juu vya estradiol na flavonoid ambayo ina saidia manii kuongezeka na kuwa na kuboresha mwendo wake.

Tende zinaongeza hamu yako ya kufanya mapenzi na vitu vingine

tende zina ongeza manii

Tende zina ongeza manii mwilini. Ni nzuri kwa afya yako. Hapa kuna baadhi ya faida za kiafya za tende, soma zaidi:

Viwango vya damu vinakuwa sawa:

Je, ungependa kutosheleza hamu yako ya sukari? Badala ya kula vitamu tamu vilivyo jazwa na sukari, kula tende chache ama switi zilizo tengenezwa kutokana na tende ili kutosheleza hamu yako ya kula sukari. Ni mbadala mwema wa sukari nyeupe isiyo kuwa na cholestrol, ufuta na sodium. Ila, ni vyema kukumbuka kuwa zina kalori nyingi ikilinganishwa na matunda mengine na kuzila kwa wingi huenda kukasababisha kuongezeka kwa uzito.

Inasaidia kuchakata chakula

Tende zina uwingi wa fibre, ina maana kuwa ni nzuri kwa mfumo wako wa utumbo na mwendo wa tumbo. Ina maana kuwa pia ina epusha kupata viwango vya juu vya cholesterol; ambayo inaweza weka moyo wako katika hatari ya kuongeza vyanzo vya kupata maradhi ya moyo na kadhalika.

Kuepuka kukosa damu mwilini

tende zina ongeza manii

Iron ina virutubisho muhimu ambavyo mwili wako una hitaji kuepuka kukosa maji tosha mwilini. Inasaidia seli nyekundu kubeba oxygeni kwa sehemu tofauti za mwili na kuzisaidia kufanya kazi vizuri. Kukosa iron mwilini huenda kukakufanya kuhisi uchovu baada ya kufanya kazi ndogo. Kula tende kutasaidia kukumbana na uchache huu.

Ina punguza nafasi za kuugua maradhi ya moyo

Tende zina 656 mg ya potassium na kuzifanya zijulikane kwa uwingi wa potassium. Kulingana na mwongozo wa WHO, mtu mzima anapaswa kula miligramu 3,510 kila siku. Idadi za chini za potassium zinaweza kufanya upate maradhi kama shinikizo la juu la damu na kadhalika.

Ina imarisha afya kwa ujumla

Mbali na wema wote tulio orodhesha, tende zina wingi wa virutubisho muhimu kama kalisi, magnesium na vitamini B6. Mwili unahitaji magnesium na kalisi ili kuboresha ukuaji wa mifupa yenye nguvu; vitamini B6 inahitajika ili protini iweze kutumika mwilini na pia mfumo wa neva uweze kufanya kazi vyema.

Healthline

Soma pia: You Can Increase Your Sperm Count By Eating These Foods

Written by

Risper Nyakio