Wazazi wanajukumu kubwa katika maisha ya watoto wao. Jinsi wazazi wanavyolinda watoto wakiwa wachanga kunachangia pakubwa katika kiwango cha maisha wanachoishi katika siku za usoni. Mambo wanayoamini, nidhamu na heshima yao.
Jinsi wazazi wanavyolinda watoto

- Zingatia vipindi ambavyo watoto wako wana tazama
Katika utamaduni wetu wa kisasa, karibu kila familia ina vifaa vya kiteknolojia vya mazungumzo na maburudisho. Kupitia kwa vifaa hivi, watoto wanaweza kupata habari na vipindi vingi. Njia ya kumlinda mtoto ni kwa kudhibitisha kuwa mtoto anatazama vipindi bora vya umri wake. Mzazi anaweza weka vidhibiti vya mzazi ili kudhibiti vitu ambavyo mtoto anatazama.
2. Kuhimiza watoto kuwa na urafiki wenye afya
Kuna usemi maarufu kuwa, 'mtoto umleavyo ndivyo akuavyo'. Ni muhimu kuanza kufunza na kuzungumza na watoto kuhusu urafiki wa maana, jinsi ya kuwa na marafiki bora na kudumisha urafiki huu. Unapowafunza watoto jinsi ya kuchagua marafiki wazuri na kuwa marafiki wazuri wenyewe, watakua wakizingirwa na watu wanaowasaidia maishani.
3. Sisitiza heshima nyumbani
Ili kulea watoto wenye heshima na nidhamu, kuwa makini na vitu unavyokubalisha nyumbani mwako. Mtoto anapokua akijua kuwa anaweza wazungumzia watu kwa njia yoyote, anakosa nidhamu. Ila, mtoto anapokua akijua kuwa hapaswi kuwazungumzia watu kwa njia yoyote ile, anakuwa na nidhamu maishani na kuwaheshimu watu.
4. Kuwa mfano wa kuigwa
Watoto hawafuati unachowaambia, mbali wanafuata mfano wako. Ikiwa ungependa kuwa na watoto wenye heshima na wanaokusikiliza, hakikisha kuwa hufanyi vitu hasi na visivyo vya heshima mbele yao. Kabla ya kuwaambia wasifanye chochote, hakikisha kuwa wewe mwenye hufanyi jambo hilo, kwani watafuata matendo yako zaidi ikilinganishwa na maneno yako.

5. Usibishane na mchumba wako mbele ya watoto
Watoto huathiriwa pakubwa na uhusiano kati ya wazazi wao. Wazazi wanapoheshimiana mbele ya watoto, watoto hukua wakiwaheshimu watu wote. Ila, watoto wanapokua katika nyumba ambapo wazazi wanavurugana kila mara, huenda wakageuka na kuwa watukutu.
6. Kuwa thabiti katika ulezi wako
Watoto hupenda ulezi thabiti na wenye uaminifu. Hasa katika nyanja za nidhamu na matarajio. Ni vyema kwa wazazi kuzungumza kwa uwazi matarajio yao kutoka kwa wazazi wao.
7. Omba na watoto wako
Kuwapa watoto wako msingi wa imani ni muhimu katika kujenga maisha yao ya usoni. Kunawasaidia kufahamu kuwa hata mambo yanapokuwa magumu, maombi husaidia na wanaweza kumtazamia Maulana mambo yasipoenda wanavyotarajia. Pia kunawasaidia kutojihusisha na vikundi vya watu wapotovu.
Soma Pia: Corazon Kwamboka: Jinsi Ya Kuwa Mzazi Bora Wa Kipekee