Safari ya mimba ni mojawapo ya wakati muhimu katika maisha mwa wanandoa. Mwanamke huwa na hamu nyingi ya kula chakula tofauti katika kipindi hiki. Na jambo hili huenda likamfanya ashuhudie ongezeko la uzito. Hata hivyo, mtoto anaye zidi kukua tumboni atachangia katika ongezeko lake la uzani wa mwili. Ni kawaida kwa wanawake kuwa na shaka kuhusu kudhibiti ongezeko la uzito katika mimba.
Uzito Katika Mimba

Kuna baadhi ya wanawake ambao huwa na uzani wa juu ama wa kupindukia hata kabla ya kupata mimba. Huku wengine wakiongeza uzani kwa kasi katika mimba. Sio jambo la busara kwa mwanamke kujinyima chakula ili kupunguza uzito wa mwili akiwa na mimba. Kuto pata chakula tosha kuta athiri afya ya mtoto anaye kua tumboni.
Kuna njia ambazo mwanamke anaweza fuata ili kudhibiti ongezeko la uzani wa mwili.
Jinsi ya kudhibiti ongezeko la uzito katika mimba
Lishe katika kipindi hiki inachangia pakubwa katika afya na uzito wa mama. Hata ingawa mama atakuwa na hamu ya kula vitamu tamu visivyo kuwa na manufaa yoyote ya kiafya. Anastahili kujisitiri na kula vitu vyenye afya. Huenda akajipata akila vyakula vyenye ufuta mwingi vitakavyo mfanya aongeze uzito.
Kuna vyakula freshi na vyenye afya. Matunda yana manufaa mengi kwa afya yake. Kuongeza vitamini na pia zinapunguza kichefu chefu. Kula mboga hasa za kijani kwa wingi. Zina vitamini nyingi ambazo ni muhimu katika kipindi hiki.
Punguza ama ujitenge na vyakula hivi:
- Vinywaji vyenye sukari nyingi kama vile soda.
- Vibanzi vya viazi
- Vyakula vilivyo kaangwa kwa mafuta nyingi
- Keki na biskuti
Punguza unywaji wa kaffeini. Badala ya kununua chakula nje, jaribu kujitayarishia chakula chako. Kwa njia hii, utahakikisha kuwa una tumia mafuta kidogo kupika. Hakikisha kuwa unachukua maji kiwango tosha.

Mazoezi ni muhimu sana ili kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja na michakato tofauti mwilini. Hata hivyo, mama mjamzito anapaswa kuhakikisha kuwa hajishinikizi anapo fanya mazoezi. Fanya mazoezi mepesi kama vile kutembea kwa dakika kama 30. Kutembea ama kupanda ngazi za nyumba.
Unapo hisi kuwa miguu imechoka ama unahema sana, pumzika. Kufanya mazoezi ukiwa na mimba kunasaida kupunguza uzito kwa kasi baada ya kujifungua.
Kufanya mazoezi na kuwa makini kula lishe yenye afya ni njia bora za kudhibiti ongezeko la uzito wa mwili katika mimba!
Chanzo: healthline
Soma Pia:Dalili Za Mapema Katika Ujauzito Unazo Paswa Kufahamu!