Kuna imani kuwa mwanamke mwenye mimba anapaswa kula chakula cha watu wawili. Na wanawake wengi hujipata wakila vyakula visivyo na afya na kwa viwango vikubwa. Jambo linalo wafanya kuongeza uzito mwingi wa mwili kwa kasi. Kula kwa watu kuna maana kuwa mama anapaswa kula chakula chenye afya ili mwili wake pamoja na mtoto wapate virutubisho tosha. Kuna vitu ambavyo mwanamke anaweza kufanya ili kudumisha afya katika mimba. Tuna angazia baadhi ya vitu muhimu anavyo paswa kuangazia.
Chakula cha mama mwenye mimba kinapaswa kuwa na nini?

Chakula chenye afya ni muhimu hasa katika ujauzito. Kuhakikisha kuwa mtoto anapata virutubisho vyote na kwa viwango vinavyo faa.
Chakula kinapaswa kuwa na:
- Bidhaa za maziwa zisizo na ufuta mwingi
- Nafaka nzima
- Nyama laini
- Matunda
- Mboga
Kula lishe bora na iliyo sawasishwa kuna hakikisha kuwa mama anapata virutubisho vyote anavyo hitaji mwilini. Hata hivyo, ana shauriwa kuchukua tembe fulani ili kufikisha viwango vya virutubisho muhimu anavyo hitaji mwilini. Kama vile tembe za kalisi, iron na folic acid.
Kalisi
Kalisi ni muhimu kwa mwanamke mwenye mimba. Kuchukua viwango tosha vya kalisi kunasaidia kuepusha kutumika kwa kalisi kutoka kwa mifupa ya mama ili kutimiza mahitaji ya kalisi ya mtoto.
Vyanzo vya kalisi ni kama vile:
- Maharagwe iliyo kaushwa
- Bidhaa za maziwa kama vile, maziwa, maziwa ya bururu
- Mboga za kijani kama vile sukuma wiki, broccoli na mchicha
- Sharubati ya machungwa
Iron
Wanawake wenye mimba wana hitaji miligramu 30 za iron kila siku. Inasaidia katika kutengeneza damu na kubeba hewa kwa viungo tofauti mwilini. Ukosefu wa chuma mwilini husababisha ugonjwa wa kutokuwa na damu tosha mwilini.
Vyakula vilivyo na viwango vingi vya iron ni kama vile:
- Nyama nyekundu
- Nyama kutoka kwa ndege wa nyumbani
- Mayai
- Matunda yaliyo kaushwa
- Nafaka
Folic
Mwanamke mjamzito ana stahili kuchukua miligramu 0.4 za folic kila siku. Kuchukua tembe za folic mwezi moja kabla miezi mitatu baada ya kushika mimba kunamsaidia mtoto kutopata matatizo ya mfumo wa neural tubes. Daktari atamshauri mama kuhusu tembe bora zaidi anazo paswa kuchukua ili kudumisha afya katika mimba. Epuka kununua tembe zozote kwenye duka la madawa bila kupata ushauri wa daktari.
Viowevu

Viowevu kama vile maji ni muhimu sana katika mimba. Mwanamke anapoteza maji mengi katika ugonjwa wa asubuhi. Ni muhimu kuhakikisha kuwa ana maji tosha mwilini. Maji hayo yana tumika na mtoto pia.
Mazoezi

Jambo linalo puuzwa kwa sana wanawake wanapo shika mimba. Wengi wao wanalegea na kupuuza kufanya mazoezi. Mazoezi ni muhimu sana katika safari hii. Hata hivyo, kumbuka kufanya mazoezi mepesi ili usijishinikize. Mazoezi katika mimba yana manufaa mengi. Kama vile:
- Kudhibiti dhidi ya kuongeza uzito kwa kasi
- Kupunguza maumivu ya mgongo ama kuvimba
- Kupata usingizi kwa urahisi
- Kuboresha kuzunguka kwa damu mwilini
- Kupunguza uzito kwa kasi baada ya kujifungua
- Kuboresha hisia za mama
- Kuutayarisha mwili kwa uchungu wa uzazi
Soma Pia: Vyakula Visivyo Na Acid Vinavyo Paswa Kuwa Kwenye Lishe Yako Wakati Wote!