Jinsi Ya Kuepuka Kupata Virusi Vya Corona

Jinsi Ya Kuepuka Kupata Virusi Vya Corona

Fuata maagizo haya kuhakikisha kuwa hauambukizwi virusi vya corona unapo toka nje

Tangu kuibuka kwa virusi vya homa ya corona maarufu kama Covid-19, kumekuwa na habari nyingi kuhusu virusi hivi. Habari zingine za kuaminika na zingine za kupotosha watu. Ni vyema kuwa makini na kuzingatia ushauri kutoka kwa wizara ya afya nchini mwako na WHO. Ili kuhakikisha kuwa watu wako salama na wana fuata maagizo ya kukumbana na janga hili. Africa Parent imeona vyema kuwaelimisha watu jinsi ya kuepuka kupata virusi vya corona. Soma makala haya kufahamu mambo unayo paswa kufanya kuhakikisha kuwa uko salama kutokana na janga la Covid-19 na familia yako pia haipati maradhi haya.

jinsi ya kuepuka kupata virusi vya corona

Vidokezo Vya Jinsi Ya Kuepuka Kupata Virusi Vya Corona

  • Hakikisha kuwa una nawa mwikoni mara kwa mara. Angalau mara kumi kwa siku. Tumia angalau sekunde 20 unapo nawa mikono. Unapo nawa mikono, tumia vitakasio vilivyo na viwango vipasavyo vya vileo. Kunawa mikono kwa muda na kwa makini kuna saidia kuua virusi ambavyo huenda vikawa mikononi mwako.
  • Unapo enda mahali kunako kuwa na watu, zingatia umbali wa mita 1.5 na mtu aliye karibu zaidi nawe. Umbali huu unakusaidia kutopata chembechembe za unyevu mtu aliye karibu nawe anapo kohoa. Huenda mtu huyo akawa na virusi hivi hatari vya homa ya corona. Iwapo mna karibia sana, huenda ukapumua unyevu unao baki hewani anapo kohoa na ukapata maradhi yale.
  • Epuka kujigusa macho, mdomo na mapua. Virusi hivi vina ingia mwilini kupitia kwa sehemu hizo. Huenda mikono yako ikashika sehemu zilizo na virusi hivyo na baada ya kushika macho ama mdomo wako, virusi hivyo vikapata namna ya kuingia mwilini mwako.
  • Hakikisha kuwa watu walio kando yako wanazingatia masharti yaliyo wekwa. Kufunika midomo wanapo chemua na kukohoa. Na kuna mikono mara kwa mara kwa kutumia vitakasio.
  • Iwapo unahisi kuwa una ishara kama vile kuchemua, kukohoa, kuumwa na kichwa ama joto mwilini, jitenge na watu wengine hadi upone.

homa ya corona

  • Valia barakoa unapo toka nje kwenda mahali popote. Ili kujikinga na kukinga walio karibu nawe.
  • Kadri iwezekanavyo, epuka kwenda kwa umati wa watu ama mikutano. Baki nyumbani, hadi pale unapo hitajika kwenda kununua vitu vya lazima kama vile vyakula ama madawa. Unapokuwa katikati ya watu, uko katika hatari ya kukaribiana na watu walio wagonjwa na uka ambukizwa.
  • Iwapo una ugua kutokana na virusi vyovyote, hakikisha kuwa unakaa nyumbani na hutoki kwani kinga yako ya mwili ni duni na nafasi yako kuugua virusi vile viko juu.
  • Ukihisi kana kwamba uko mgonjwa. Hakikisha kuwa unaenda hospitalini, lakini una shauriwa kumpigia daktari wako simu kwanza kabla ya kutembea hospitalini.

Kila mtu ana shauriwa kufanya awezavyo kufuata ushauri kutoka kwa wizara ya afya nchini mwao. Hakikisha kuwa unafuatilia habari za Covid-19 nchini mwako.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio