Wanawake ambao wanataka kuzuia mimba wanaweza kufanya maamuzi bora iwapo watakuwa na fursa ya kuchagua kati ya njia mbalimbali. Wanahitaji taarifa sahihi juu ya maelezo na ufanisi wa kila njia. Kuna jinsi ya kuepuka mimba kwa njia asili kama ifuatavyo.
Jinsi Ya Kuepuka Mimba Kwa Njia Asili

Kupanga uzazi kwa njia asili ina maana mbinu za kuzuia mimba isipatikane katika tendo la ndoa ambazo hufuata maumbile tu. Njia asili hazihusishi vifaa wala kemikali. Zinategemea ufahamu wa uwezo wa mwanamke kupata au kutopata mimba wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Wanawake ambao wananyonyesha na wanapenda kukwepa mimba wanaweza kufanya tendo la ndoa kwa kutegemea kukatizwa kwa hedhi wakati wa kunyonyesha. Mbali na huo ujuzi wa jumla, uzazi unaweza kupangwa kwa kutofanya tendo la ndoa siku 13.Hizi ni siku ambazo katika mzunguko wa hedhi kuna uwezekano wa kupata mimba.
Kinyume chake wanandoa wanaweza kulenga kwa uhakika uzazi kwa kufanya tendo la ndoa katika siku za rutuba za mwanamke. Vilevile wanaweza kuchagua jinsia ya mtoto mtarajiwa kwa kufanya tendo la ndoa siku ambapo kwa kawaida mbegu ya jinsia hiyo ndiyo inayowahi kuungana na yai la mwanamke katika tumbo la uzazi.
Ujuzi Wa Kisayansi
Utafiti umeonyesha kuwa mizunguko mingi ya hedhi huwa na siku kadhaa za mwanzo ambapo mimba haiwezi kupatikana. Halafu kuna siku ambazo mimba inaweza kutungika(siku za rutuba). Kisha siku kadhaa tu kabla ya hedhi ambazo mimba haiwezi kutungika. Siku ya kwanza ya kuvuja damu inahesabiwa kuwa siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi. Ujuzi wa kisayansi umeongeza idadi na hasa usahihi wa njia asili za kuzuia mimba.

Mbinu Zinazotegemea Dalili
Mbinu kadhaa hutegemea uchunguzi wa mabadiliko yanayoashiria uwezekano wa kutunga mimba. Hii ni kwa kufuatilia mzunguko wote wa hedhi ili kubaini siku za rutuba. Dalili tatu za msingi huwa ongezeko la joto msingi la mwili, ute wa uke na mkao wa mlango wa kizazi. Wanawake wengi hungamua dalili zingine za ziada kulingana na mzunguko wa hedhi kama vile maumivu na uzito tumboni, maumivu mgongoni, ulaini wa matiti na maumivu ya kuachilia yai.
Mbinu Zinazotegemea Kalenda
Mbinu hizi hufuatilia mzunguko wa hedhi na kwa kuzingatia urefu wake. Kuna wanawake walio na mizunguko halisi(regular) na wengine inayobabdilika. Walio na mizunguko halisi wana ufanisi mkuu wanapozingatia hii mbinu. Siku ya kwanza ya hedhi hujulikana kama siku ya kwanza ya mzunguko. Kwa kawaida yai la mwanamke huachiliwa baada ya siku kumi na nne ama katikati ya mzunguko. Hivyo huwa bora kujiepusha na mapenzi siku chache kabla na baada ya kipindi hiki.
Sifa Za Njia Asilia Za Kuepuka Mimba
- Zinaweza kutumika katika kudhibiti afya ya uzazi
- Zinaweza kutumiwa na wanawake wote katika kipindi chote cha uzazi
- Huongeza ufahamu wa jinsi mwili wa mwanamke unavyofanya kazi na unamwezesha kudhibiti zaidi uzazi wake binafsi
- Hazina madhara yoyote
- Hazina gharama au ni nafuu sana ikilinganishwa na mbinu zingine
- Ni tofauti na mbinu ambazo zina athari za muda mrefu
Watu wengi huzingatia upangaji uzazi kwa kutumia dawa za kupanga uzazi ila wengi hawafahamu jinsi ya kuepuka mimba kwa njia asili. Ila sifa zake ni wazi hii njia ni mwafaka kabisa.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Hatari Na Faida Za Kushika Mimba Baada Ya Miaka 35