Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Lockdown Kufuatia Homa Ya Corona: Mazoezi Ya Kufanyia Nyumbani

3masomo ya dakika
Lockdown Kufuatia Homa Ya Corona: Mazoezi Ya Kufanyia NyumbaniLockdown Kufuatia Homa Ya Corona: Mazoezi Ya Kufanyia Nyumbani

Huenda janga hili la corona huenda likawa liliweka kizuizi kwa mazoezi yako ya wikendi kama vile zumba ama kwenda mahala pa kufanya mazoezi, ila hilo halimaanishi kuwa usahau kuhusu uzima wako wa afya, endelea. Chinwe Obinwanne, mama wa watoto watatu wanaopendeza na aliye anza Naijafitmoms Fitness Empire, anawaeleza watu jinsi ya kufanya mazoezi nyumbani na hata kushughulisha watoto katika lockdown hii ya Covid-19.

how to exercise at home

Jinsi Ya Kufanya Mazoezi Nyumbani Na Watoto Wako

Tumekuwa tuki sakata densi kwa wingi na watoto wetu, kuruka kamba ana kuhusika katika njia tofauti za usawa wa afya kwa kutumia vifaa vya uzito wa mwili na wakati mwingine applications za usawa wa mwili. Haupaswi kuwa na shaka kuhusu nafasi, ikiwa una nafasi tosha ya kugeuka bila kugonga kitu chochote, hilo ni sawa, na kufanya mazoezi ya mkeka kwa urahisi.

Kufanya watoto wafuate utaratibu wa usawa wa mwili nyumbani kunahitaji upole na kujitolea kwingi ili mchakato huu uwe wa  kuburudisha. Hapa ni baadhi ya mawazo ambayo unaweza jaribu:

  • Kusaata densi ni moja wapo ya njia mwafaka za kufanya mazoezi na wewe na watoto wako mtafurahia pia, kwa hivyo, weka muziki na usakate densi na wanao.
  • Kulingana na umri wa watoto wako, mnaweza ruka kamba kwa watu wawili kama tulivyo fanya hapo awali tukiwa wadogo ambapo watu wawili wangeshika kamba na mmoja angekuwa anaruka hapo katikati. Niamini; utafurahikia jambo hili na pia kuyeyusha mafuta yaliyo mwilini.
  • Iwapo una nafasi kubwa kwenye uwanja wako, kimbieni na watoto wako na atakaye shinda atuzwe.
  • Jambo lingine la kufurahisha la kufanya ni kukimbia kwa magunia iwapo una gunia kadhaa nyumbani, zitumie kufanya hivi.
  • Pia unaweza jaribu kurusha madondi kwenye hewa. Kurusha madondi huku, kunaweza saidia watoto wako kuwa washindi wabunifu wanapo rusha ngumi na kuwashinda watu wasio onekana. Unaweza sema, turushe ngumi 150 kupambana na watu hawa wabaya kisha uanze kuhesabu. Ni mazoezi mwafaka ya mikono na ukiifanya kwa nguvu, unapaswa kumwaga jasho.

jinsi ya kufanya mazoezi nyumbani

Mazoezi ya kuhimiza kutangamana kwa wanandoa

  • Wanandoa wanaweza sakata densi.
  • Kufanya mapenzi zaidi (naam, ni mazoezi ya kifizikia)
  • Kufanya mazoezi kama vile kuchuchumaa, planks, jacks, kukaa kwa ukuta na mazoezi mengineyo kwa pamoja. Kufanya hivi kuta tia mwingine moyo huku mkihimiza utangamano ulioko kati yenu.
how to exercise at home

Kibuyu cha maji cha kufanya dumbbells Picha:pixabay

Mawazo jinsi ya kuwa mbunifu ikifika wakati wa vifaa
  • Kwa dumbbells nyepesi, unaweza tumia vibuyu vya maji.
  • Iwapo unataka dumbbells nzito, unaweza tumia vibuyu vilivyo jazwa na maji.
  • Iwapo unatafuta uzito zaidi wa kufanya mazoezi kama vile kuchuchumaa, unaweza tumia vibuyu vya maji vya lita 5-10.
  • Pia una mkoba wa shule uliojazwa na vitabu, kikapu kidogo kilicho jazwa na nguo na zinginezo, inategemea na kiwango chako cha ubunifu unacho tarajia kutimiza.

Vidokezo vya afya vya kukumbuka unapo fanya mazoezi nyumbani

Ikifika ni wakati wa kufanya mazoezi, wazazi wanapaswa kuwa makini kuzingatia utaratibu wanapofanya mazoezi ya kila siku kwani kukosa kufanya hivi huenda kukasababisha maumivu.

Pia, ni lazima wazazi wasikize miili yao wanapofanya mazoezi na wasifanye zaidi ya vile ambavyo mili yao inakubalisha.

Kunywa maji tosha ni muhimu unapofanya mazoezi, hakikisha una maji karibu.

Nyoosha mwili kabla ya kuanza mazoezi na baada ya kumaliza mazoezi yako ili kuepuka kuumwa na sehemu za mwili.

 

Soma pia: Exercise For Pregnant Women: Simple Routines To Keep You Fit

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Syreeta Akinyede kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

img
Yaliandikwa na

Risper Nyakio

  • Nyumbani
  • /
  • Parent's Guide
  • /
  • Lockdown Kufuatia Homa Ya Corona: Mazoezi Ya Kufanyia Nyumbani
Gawa:
  • Mambo 5 Muhimu Unayo Paswa Kufanya Kabla Ya Kufanya Mazoezi

    Mambo 5 Muhimu Unayo Paswa Kufanya Kabla Ya Kufanya Mazoezi

  • Fanya Mazoezi Nyumbani Kwa Kutumia Karatasi Shashi!

    Fanya Mazoezi Nyumbani Kwa Kutumia Karatasi Shashi!

  • Ujauzito Na Mazoezi: Ni Salama Kufanya Mazoezi Katika Kipindi Hiki?

    Ujauzito Na Mazoezi: Ni Salama Kufanya Mazoezi Katika Kipindi Hiki?

  • Mazoezi Ya Mama Mjamzito: Utaratibu Wa Rahisi Wa Kukusaidia Kuwa Na Afya

    Mazoezi Ya Mama Mjamzito: Utaratibu Wa Rahisi Wa Kukusaidia Kuwa Na Afya

  • Mambo 5 Muhimu Unayo Paswa Kufanya Kabla Ya Kufanya Mazoezi

    Mambo 5 Muhimu Unayo Paswa Kufanya Kabla Ya Kufanya Mazoezi

  • Fanya Mazoezi Nyumbani Kwa Kutumia Karatasi Shashi!

    Fanya Mazoezi Nyumbani Kwa Kutumia Karatasi Shashi!

  • Ujauzito Na Mazoezi: Ni Salama Kufanya Mazoezi Katika Kipindi Hiki?

    Ujauzito Na Mazoezi: Ni Salama Kufanya Mazoezi Katika Kipindi Hiki?

  • Mazoezi Ya Mama Mjamzito: Utaratibu Wa Rahisi Wa Kukusaidia Kuwa Na Afya

    Mazoezi Ya Mama Mjamzito: Utaratibu Wa Rahisi Wa Kukusaidia Kuwa Na Afya

Pata ushauri wa mara kwa mara kuhusu ujauzito wako na mtoto wako anayekua!
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • Zaidi
    • TAP Jamii
    • Tangaza Nasi
    • Wasiliana Nasi
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
Kutuhusu|Timu|Sera ya Faragha|Masharti ya kutumia |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it