Jinsi Ya Kuficha Mimba Kwa Muda Mrefu Iweze Kanavyo

Jinsi Ya Kuficha Mimba Kwa Muda Mrefu Iweze Kanavyo

Huenda daktari wako aka kushauri kuweka habari za mimba yako fiche hasa katika trimesta yako ya kwanza. Tuna kupa vidokezo muhimu vya kutimiza jambo hili.

Mwanamke anapo kuwa na mimba, huwa na swali moja muhimu. Kujulisha watu ama kuficha habari hizi? Punde tu anapo gundua kuwa anatarajia mtoto, huenda akafikiria kuweka habari hizi fiche ama kuwajuza marafiki na wanafamilia wa karibu. Kwa nini wanawake huwa na fikira za kuficha mimba? Kuna sababu chache ambazo huenda zikawafanya wasiwajulishe watu wengi. Wanawake wengi huamua kuweka habari hizi fiche katika trimesta yao ya kwanza kwa sababu ya hatari ama changamoto kazini. Baadhi ya wakati, iwapo ni mimba iliyo na hatari nyingi, daktari wako ata kushauri kuweka habari hizi fiche kwanza. Kwa sababu zozote zile, ni sawa. Tuangazie jinsi ya kuficha mimba hadi wakati ambapo itakapo anza kuonekana.

Vidokezo vya kuficha mimba

  • Usivalie nguo za uzazi

Jinsi Ya Kuficha Mimba Kwa Muda Mrefu Iweze Kanavyo

Mavazi ya uzazi huwa yameundwa kuonyesha mimba inayo kua. Na kuwajulisha watu kuwa una tarajia. Iwapo hauta badilisha mitindo yako ya mavazi kwa kasi sana, watu huenda hawatagundua mabadiliko katika nguo zako. Wazo ni kununua nguo ambazo ni saizi mbili kubwa kuliko saizi yako ya kawaida. Hii ni hiari njema kwa visa ambavyo una itwa kwa mahojiano ya kikazi.

  • Valia mapambo yote unayo yafurahi

Jinsi Ya Kuficha Mimba Kwa Muda Mrefu Iweze Kanavyo

 

Mapambo ni njia nzuri ya kuwafanya watu waangalie sehemu fulani na kutoa macho yao mbali na tumbo yako. Tumia mapambo kutoa macho ya watu kwenye tumbo lako linalo endelea kukua. Unaweza fanya hivi kwa kutumia mikufu ya dhahabu, na herini ama kwa kuvalia mavazi ya rangi nyeusi. Kwa wakati huu kabla tumbo yako iwe kubwa sana, hakuna atakaye gundua kuwa una kiumbe kinacho kua ndani yako.

  • Tumia sababu ya kumwona daktari wa meno

Jinsi Ya Kuficha Mimba Kwa Muda Mrefu Iweze Kanavyo

 

Kliniki za mimba na za madaktari wa mimba huendana kama rangi nyeupe kwenye mchele. Iwapo una scan ambayo unapaswa kuenda na unapaswa kuendea matibabu ya utunzi kabla ya kujifungua, huenda watu hawata gundua chochote kazini. Tumia sababu ya kumwona daktari wa meno! Unaweza mwambia mkubwa wako kazini kuwa unaenda hospitalini kuangaliwa meno. Ama hata kung'olewa meno.

  • Tumia jisababu la kudetox

Jinsi Ya Kuficha Mimba Kwa Muda Mrefu Iweze Kanavyo

Jisababu nyingine yenye afya ni kusema kuwa una detox. Unaweza itumia kuepuka kula vyakula na vinywaji ambavyo havikubaliki katika mimba. Badala ya kusema kuwa huwezi kunywa vileo ama divai, sema kuwa huwezi kunywa vinywaji hivyo pamoja na kahawa kwa sababu una detox. Hakuna atakaye jua unacho kificha. Pia ni sababu nzuri ya kuto kula nyama ambayo haija iva vizuri.

  • Mikono mbali na tumbo

Jinsi Ya Kuficha Mimba Kwa Muda Mrefu Iweze Kanavyo

Wanawake wengi walio na mimba hugusa tumbo zao, mara kwa mara. Huenda ikawa ni hisia za kuwa mama zinazo ingia polepole. Hakikisha kuwa hufanyi hivi ukiwa mbele ya watu ambao hungependa wajue kuwa una mimba. Kumbuka kuiweka mikono yako mbali na tumbo yako, ili usiwafanye watu waangalie tumbo yako.

  • Play The Doctor's Orders Card

kuficha mimba

 

Unataka kufanya kitu ambacho ni kizuri kwa mtoto anaye kua ndani ya tumbo yako, kwa hivyo lazima ufanye mabadiliko ya lishe na mitindo na kukaa mbali na vileo na kahawa. Tatizo ni kuwa jambo hili huenda likawajuza wengine unacho jaribu kuficha. Marafiki wako wanapo kualika kunywa kahawa ama vileo, waambie kuwa unatatizika kupata usingizi usiku. Daktari wako alikushauri kuto kunywa chai kwa siku chache. Unaweza beba chupa na ujaze na maji na hakuna atakaye jua.

  • Valia nguo zisizo kubana

Jinsi Ya Kuficha Mimba Kwa Muda Mrefu Iweze Kanavyo

 

Rinda kubwa ni njia kubwa ya kuficha tumbo yako inayo endelea kukua. Unaweza enda kwenye maduka uanze kununua marinda makubwa. Nunua mavazi ambayo yata pendeza kwa mwili wako. Iwapo rinda litakuwa pana sana, huenda watu wakajua unacho kificha. Huenda pia ukavalia blausi ama shati pana ili kuficha tumbo yako. Kwa kufanya hivi, sio lazima uvalie blausi kubwa wakati wote kwani watu huenda wakaanza kujua kuna kitu unaficha. Pia kuna mitindo ya mavazi ambayo huwa pana kwenye kiuno chako, hizi ni hiari nzuri katika lengo lako la kuficha mimba.

  • Begi na mikoba mikubwa inapaswa kuwa rafiki yako

kuficha mimba

Unapaswa kununua begi moja ama mbili kubwa ili zikusaidie katika lengo lako kubwa. Mkoba huu unapaswa kuwa mkubwa kiasi cha kuficha tumbo yako inayo endelea kukua. Weka begi mahali pazuri ili ifiche mkoba wako. Beba begi hili mbele ya tumbo yako na hakuna atakaye jua siri yako. Pia unaweza weka mapambo kwenye begi yako kama vile skafu. Hii itakusaidia katika jambo unalo kusudia kutimiza.

Soma pia: Jinsi Ya Kumwambia Mchumba Wako Kuwa Una Mimba Kwa Njia Ya Kipekee

 

Written by

Risper Nyakio