Jinsi Ya Kufunga Kwa Vipindi.

Jinsi Ya Kufunga Kwa Vipindi.

Intermittent fasting is an effective way to lose weight and improve health. Learn how to do intermittent fasting using these methods.

Kufunga kwa kipindi  kumekuwa mojawapo ya mitindo ya miaka ya hivi karibuni.  Kuna umaarufu kwa sababu ya kupunguza uzito, kuboresha hali ya metaboli na labda pia kurefusha maisha yako. Si jambo la kushangaza ukizingatia umaarufu wake, mitindo mingi ya kufunga kwa vipindi imefumbuliwa. Tunaenda kukuonyesha jinsi ya kufunga kwa vipindi. Bora ata zaidi, tutakuonyesha njia tano. Hivyo, utaweza kuchagua ni njia ipi inafaa mtindo wako wa maisha.  Njia zote zina ufanisi tosha, lakini ile inakufaa vyema italingana nawe.

Jinsi ya kufunga kwa vipindi: Mbinu 5 maarufu zaidi

Jinsi Ya Kufunga Kwa Vipindi.

Njia ya 16/8: Funga kwa masaa 16 kila siku.

Njia hii ya 16/8 huhusisha kufunga kwa masaa 14-16 kila siku na kupunguza mwanya wako wa kula hadi masaa 8-10 kila siku. Katika mwanya huo wa kula, unaweza kuongeza milo mbili au tatu zaidi.  Huu mtindo ni wa Leangains protocol na ulifanyika maarufu kupitia kwa gwiji wa mazoezi Martin Berkhan.

Mtindo huu ni rahisi tu kama vile kujiepusha na kula chakula chochote baada ya chajio na kutokula kiamsha kinywa.  Kwa mfano, unamaliza chakula cha jioni saa 8 usiku na usile tena mpaka saa sita mchana siku inayofuatia.  Hivyo utakuwa unafunga kwa masaa kumi na sita katikati ya milo.  Wataalam hupendekeza wanawake kufunga kati ya masaa kumi na nne na kumi na tano pekee kwa vile wao huonekana kufanya vyema wakifunga kwa masaa machache.

Unaweza kunywa maji, kahawa, vinywaji vingine visivyo vya kulewesha wakati wa kufunga. Hii inaweza kupunguza kuhisi njaa.  Ni muhimu kula vyakula vilivyo kamili katika huo mwanya wako wa kula,. Huu mtindo hautafanya kazi iwapo utakula chakula kisichofaa au chenye kalori kupita kiasi.

 Lishe ya 5:2 : Kufunga kwa siku mbili kila wiki.

kufunga kwa kipindi

Huu mtindo huhusisha kula kwa kawaida kwa siku tano katika wiki huku ukijiepusha na kalori 500-600 kwa siku mbili kila wiki. Hii lishe pia ni mtindo wa kufunga na ulipata umaarufu kupitia kwa mwanahabari  wa Britain na daktari Michael Mosley.

Kwa siku unazofunga,  wataalam hupendekeza wanawake kula kalori 500 na wanaume kula kalori 600. Kwa mfano, unaweza kula kwa kawaida siku zile zote zingine ila tu jumatatu na alhamisi.  Hizi ndizo siku unakula chakula kidogo zaidi( kalori 250 kwa kila chakula kwa wanawake na kalori 300 kwa wanaume). Kama wakosoaji  wanavyosema hakuna utafiti uliofanyika juu ya lishe la 5:2 lakini kuna utafiti mwingi juu ya manufaa ya kufunga kwa vipindi.

Kula-koma-kula: Funga kwa masaa 24 mara moja au mbili kwa wiki.

Kula- koma -kula huhusisha kufunga kwa masaa 24 aidha mara moja au mbili kwa wiki. Huu mtindo ulipata umaarufu kupitia kwa gwiji wa mazoezi Brad Pilon na umetamba sana kwa miaka michache iliyopita. Kwa kufunga kutoka chajio moja hadi inayofuatia hio siku nyingine itakamilisha kufunga kwa masaa 24.

Kwa mfano, ukimaliza chajio jumatatu saa moja jioni usile tena hadi chajio siku inayafuata saa moja usiku na hivyo utakuwa umemaliza kufunga kwa kipindi cha masaa 24. Bado unaweza kufunga kutoka kiamsha kinywa hadi kiamsha kinywa chingine ama kutoka chakula cha mchana hadi kinachofuatia. Matokeo huwa ni sawia. Maji, kahawa na vinywaji vingine visivyo na vileo huruhusiwa lakini hakuna kula chakula kigumu.

Kama unafanya hivi kupunguza uzito, azima ukule vipimo vya kutosha wakati wa mwanya wa kula. Kama vile, kula vipimo sawai na wakati haufungi.

Shida iliopo kwa huu mtindo ni kuwa kufunga kwa masaa 24 ni ngumu sana kwa watu wengi, lakini si lazima uanze kwa haya masaa mara ya kwanza. Unaweza kuanza na kati ya masaa 14 -16 kisha uongeze kwenda mbele.

Kuvuka milo kwa hiari: vuka milo unapopata fursa.

kufunga kwa kipindi

Hauhitaji kufuatilia mtindo wowote ule wa kufunga kwa vipindi ili kupata matokeo mazuri. Njia nyingine mwafaka ni kuvuka milo mara kwa mara. Kwa mfano, iwapo hauhisi njaa au una kazi nyingi isiyo kuruhus kula au kupika. Ni hadithi za kiasili kuwa lazima watu wale baada ya masaa machache ama watakuwa wenye njaa kupita kiasi ama watapoteza misuli. Mwili wa binadamu umeumbika kwenda kwa vipindi virefu bila chakula sembuse mlo mmoja au mbili mara kwa mara. Kwa hivyo kama hauna njaa siku moja, vuka kiamsha kinywa na ule chakula cha mchana na chajio kamili. Au kama unasafiri na huwezi kupata kitu cha chakula funga kwa kipindi kifupi.

Kuvuka mlo mmoja au mbili unapojihisi hivyo hujulikana kama kufunga kusio kwa hiari. Hakikisha tu umekula chakula kamili wakati utakapokuwa  unakula.

Mlo wa shujaa: Funga mchana kula chakula kingi usiku.

Huu mtindo wa kufunga ulipata umaarufu kupitia kwa gwiji wa mazoezi  Ori Hofmekler. Huhusisha  kula vipimo vidogo vya matunda mbichi na mboga mchana alafu kula chakula kingi  jioni. Kwa ufupi, unafunga mchana wote kisha unakula chakula kingi usiku katika mwanya wa masaa manne.

Mlo wa kishujaa ni mojawapo ya mbinu za kwanza zilizohusisha mfumo wa kufunga kwa vipindi.

Jinsi ya kufunga kwa kipindi: Umuhimu wake

 • Kupunguza uzito
 • Shinikizo la damu lililo chini
 • Kuenda chini kwa uvimbe
 • Matokeo bora kwa waliopona kuharusi
 • Kupunguza kiwango cha kolesteroli
 • Kuboresha utendaji wa ubongo
 • Kinga kutokana na saratani
 • Ongezeko la kaunti ya seli
 • Kupunguza ukinzani wa insulini
 • Shida za moyo zilizo punguka
 • Kurefusha maisha
 • Kuwa na usingizi mzuri unapolala

Medical News Today

Also read: How To Identify Blood Sugar Levels And Keep Diabetes At Bay

Written by

Risper Nyakio