Jinsi Ya Kufungua Chuchu Za Mama Zilizo Ziba

Jinsi Ya Kufungua Chuchu Za Mama Zilizo Ziba

Iwapo unashangaa jinsi ya kufungua chuchu zilizo ziba, uko mahali panapo faa. Mama anaye nyonyesha anaye tatizika na kiwango cha maziwa kinacho toka kwa chuchu zake anaweza kueleza jinsi anavyo hisi kukata moyo. Baada ya kugundua kuwa mtoto hali ipasavyo. Chuchu zinaweza kuwa laini na kufura kwa sababu maziwa yame zibwa na hayana njia dhabiti ya kutoka.

how to clear clogged milk ducts

Kwa bahati nzuri, unaweza tatua tatizo la maziwa yaliyo ziba kwa kufuata mbinu hizi zilizo jaribiwa na kufuzu za kufungua chuchu.

Chuchu za mama zilizo ziba ni nini hasa?

Chuchu zina maziwa yanayo tumika kumlisha mtoto baada ya kuzaliwa. Iwapo chuchu hizi zitaziba, huenda mama akawa na shida ya chuchu zilizo fura. Chuchu zilizo fura huzuia maziwa kutoka kwa urahisi.

Chuchu zinazo paswa kubeba maziwa zisipo fanya kazi yake, maziwa huenda yaka baki kwenye chuchu badala ya kutoka. Matokeo ya jambo hili huenda yaka fanya ukate tamaa na uhisi uchungu, na hii ndiyo sababu kwa nini unapaswa kufahamu jinsi ya kukabiliana na tatizo la chuchu za mama kubana na kufungana.

how to clear clogged milk ducts

Sababu za chuchu za maziwa kufungana

Maziwa nyingi ya mama

Iwapo unatoa maziwa mengi ya mama, huenda ukawa na tatizo la matiti kufungana. Utoaji mwingi wa maziwa ya mama huenda likawa tatizo iwapo mtoto wako hawezi maliza. Maziwa yanayo baki kwenye matiti huenda yaka ziba matiti.

Kufura kwa matiti

Kufura kwa matiti ni ishara na athari hasi ya kubana kwa chuchu za maziwa. Mfumo wa kutoa maziwa ukikosa, matiti yako yata fura na kuwa na uchungu unapo gusa.

Mtoto hali vizuri

Hii ni sababu kuu ya matiti kufura. Iwapo chuchu zako zinafura kwa mbio, unapaswa kuhakikisha kuwa mtoto wako ana nyonya ipasavyo.

Mtoto hanyonyi chuchu vizuri anapo kula

Mtoto anapo nyonya, mdomo wao unapaswa kufunika areola. Inapaswa kuwa ndani ya mdomo wake kuhakikisha kuwa mtoto ana nyonya vizuri. Iwapo kesi ni tofauti, mtoto hanyonyo vizuri na unapaswa kuwa na shaka.

Lazima uhakikishe kuwa mtoto wako anapata maziwa tosha kabla ugundue jinsi ya kufungua matiti yaliyo ziba.

Haushiki mtoto vizuri unapo mnyonyesha

Kumshika mtoto ipasavyo anapo nyonya kutasaidia kufungua chuchu zilizo fungana. Mkono mmoja wa mtoto wako unapaswa kuwa nyuma yako, kitovu chake kinapaswa kugusa tumbo yako, na kichwa chake kinapaswa kulala kwenye mkono wako, na mguu mmoja unapaswa kuinuka kidogo na mkono wako kuwa chini ya makalio yake. Iwapo hauwezi kumshika mtoto kwa njia hii, huenda akakosa kunyonya ipasavyo.

how to clear clogged milk ducts

Iwapo mtoto wako anakula kidogo, kulala sana, kunywa formula nyingi, kukosa lishe, kungoja sana kabla ya kula tena, unapaswa kufahamu jinsi ya kufungua chuchu zilizo fungana kwa sababu hiyo huenda ikawa sababu.

Kumwanzishia mtoto chakula

Hiki ni kitendo cha kuto mnyonyesha mtoto ili awache kunyonya. Athari hasi za kitendo hiki ni kuwa kumwanzishia mtoto chakula mbali na maziwa ya mama huenda kuka sababisha chuchu kubana.

Shinikizo kwenye chuchu

Kubeba vitu nzito, kuvalia sindiria zinazo kubana, kulala kwa upande mmoja usiku wote, kufanya mazoezi magumu kama vile kukimbia na kuruka ni sababu zinazo sababisha chuchu kufungana.

Ishara za chuchu za maziwa zilizo fungana

• Uchungu kwenye sehemu iliyo athiriwa
• Uvimbe laini
• Baridi
• Blebs za maziwa
• Chuchu nzito

kufungua chuchu zilizo ziba

Jinsi ya kufungua chuchu zilizo bana

Kuepuka ni bora kuliko kuponya. Jinsi ya kuponya chuchu zilizo ziba ni kuepuka sababu zinazo sababisha chuchu za maziwa kuziba. Unaweza fanya mambo haya kufanya maziwa yako yatiririke vyema:

a. Valia sindiria za kunyonyesha na nguo zisizo kubana, Usijali sana kuhusu shepu za chuchu zako unapo nyonyesha. Chuchu zako zina stahili kuwa kubwa unapo nyonyesha.

b. Mnyonyeshe mtoto wako mara nyingi iwezekanavyo. Hakikisha kuwa ana nyonyesha vyema na ubadili chuchu zote mbili. Unapokuwa na chuchu iliyo ziba, anza na chuchu hiyo. Ikiwezekana, ipe chuchu hiyo misa huku ukiendelea kumnyonyesha mtoto.

c. Lala kwa upande badala ya kulalia tumbo (kwa sababu kulala kwa tumbo hushinikiza chuchu zako. Badili pande zote mbili pia.

d. Piga misa sehemu iliyo athiriwa kwa kutumia maji moto. Pia unaweza weka chuchu zako kwa maji moto iwapo unaweza stahimili kuto hisi starehe. Iwapo huwezi, wekelea nguo yenye joto kwenye sehemu hiyo. Kuoga na maji moto kunasaidia pia.

e. Kunywa vinywaji vingi na upumzike kwa sana.

f. Pia, jinsi ya kuepuka kuwa na chuchu zilizo bana ni kuepuka vinywaji na vyakula vinavyo boresha utoaji wako wa maziwa. Kula matunda, mboga na njugu.

g. Wekelea mtoto kwenye kitanda, mwinamishe mtoto wako na umnyonyeshe. Hii inajulikana kama 'dangle feeding'.

h. Jinsi ya kutatiza chuchu zilizo fungana ni kwa kuweka baadhi ya vyakula vyenye virutubisho - viazi baridi, matawi ya kabichi moto, chai ya lavender -kwenye sindiria yako! Pia unaweza paka mafuta ya nazi na shea butter kwenye chuchu zako baada ya kupiga chuchu zako misa.

Ukifuata vidokezo hivi vya jinsi ya kufungua chuchu zilizo bana na baada ya siku tatu ishara zinaendelea kuwa mbaya zaidi, unapaswa kuenda hospitalini. Iwapo bado kuna ugumu kwa chuchu, huenda daktari wako akahitaji kukufanyia vipimo kudhibitisha hauna ugonjwa wowote.

Kumbukumbu: Medical News Today

Soma pia : Vyakula Vya Lactogeni Vya Kumsaidia Mama Kuongeza Maziwa

Written by

Risper Nyakio