Ili mapenzi yafuzu na yanoge, wachumba wote wawili wana stahili kufanya juhudi ili uhusiano wao uwe wenye nguvu. Na sio kati ya wanandoa tu, mbali hata kwa mandugu, wazazi, marafiki na wafanya kazi. Utapatana na watu wengi, wengine ambao watakusaidia pakubwa maishani, huku wengine mkiwachana baada ya muda mfupi. Haijalishi ikiwa una mchumba ama bado hauja fanikiwa, kuna njia fulani za kuimarisha uhusiano huu na wale unao wapenda.
Njia 7 Za Kuimarisha Uhusiano Wako:

- Cheka nao sana
Fanya vitu vitakavyo wafanya mcheke kwa pamoja sana. Tengenezeni makumbusho ya ucheshi kwa muda wenu mlio pamoja, kufanya hivi kuta boresha utangamano wenu na uhusiano wenu utakuwa bora.
2. Kujadili masuala tata
Kosa moja ambalo watu wengi hufanya na ambalo huwa na athari hasi kwa uhusiano wa aina yoyote ile ni kuto jadili masuala yanayo wasumbua. Kwa kufanya hivi, chuki inaanza kukua na utengamano kuzidi. Baada ya muda, uhusiano wenu unakatika. Ikiwa kuna jambo linalo kutatiza, hakikisha kuwa unachukua muda na kuzungumza na mwenzi wako ama rafiki yako na kutatua suala hilo.
3. Ku safiri pamoja
Kuenda ziara pamoja na mtu unaye mpenda huwaleta pamoja na pia mnatengeneza nyakati za kupendeza za kukumbuka kwa muda mrefu, hasa kwa wanandoa. Mtahisi kuwa mmekaribiana zaidi baada ya ziara ya kupendeza.
4. Kuwa na wakati pamoja
Kutenga wakati wa kuwa na mtu unaye mpenda ni muhimu sana. Hampati muda wa kufanya mambo mnayo yapenda pamoja tu, mbali mnaweza kujuana zaidi. Na sio kwa walio na wachumba tu, mbali kwa marafiki na ndugu zako pia. Mnapo fanya hivi, uhusiano wenu una zidi kukua.
5. Mzawadi umpendaye

Kuelewa lugha ya mapenzi ya mwenzi wako ni muhimu sana. Utaweza kuelewa anacho hitaji ili kuona kuwa mapenzi yenu yanafuzu. Ikiwa ana penda zawadi, hakikisha kuwa unamzawadi mara kwa mara. Kwa kufanya hivi, pia ataona kuwa ana enziwa.
6. Mpongeze
Kumpongeza mwenzi wako mara kwa mara kutafanya ahisi kuwa unaona na kufurahia juhudi anazo tia maishani na pia kwenye uhusiano wenu.
7. Sherehekea ushindi wake
Kusherehekea mtu anaye mpenda anapo shinda ama kutimiza lengo fulani ni muhimu sana.
Soma Pia: Malengo 10 Ya Uhusiano Yatakayo Fanya Mapenzi Yenu Yakue