Vidokezo 3 Muhimu Vya Jinsi Ya Kujifungua Mtoto Shupavu

Vidokezo 3 Muhimu Vya Jinsi Ya Kujifungua Mtoto Shupavu

Mama, unapo kula chakula cha watu wawili, kumbuka kuwa nyote wawili mnahitaji virutubisho vingi. Vya kuegemeza mabadiliko ya kasi yanayo tendeka.

Ushauri wa kimsingi na mkuu kuhusu jinsi ya kujifungua mtoto shupavu, ni kwa wazazi wote wawili. Wazazi wanashauriwa kujitenga na vileo, mvinyo, kafeini nyingi na sigara wanapo anza juhudi za kutunga mimba. Kulingana na profesa wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha California huko Long Beach, Stephen J. Schoenthaler.

Soma mambo muhimu ambayo wanandoa na mama mjamzito wanapaswa kuangazia ili kuongeza nafasi zao za kupata mtoto shupavu.

Jinsi Ya Kujifungua Mtoto Shupavu

jinsi ya kujifungua mtoto shupavu

Epuka hatari

Ni vyema kwa mama mwenye mimba kujitenga na vitu ambavyo vinaweza athiri ukuaji wa ubongo wa mtoto. Vitu kama vile rangi nzee ama kutengeneza mfumo wa maji kwenye nyumba. Ikiwa unaishi kwenye nyumba nzee, hakikisha kuwa vipimo dhabiti vimefanyika na mahali hapo ni sawa.

Kula vyakula vya baharini kutoka kwa maji machafu kunaweza athiri mtoto kufuatia wingi wa mercury na lead. Mama ana shauriwa kuwa makini sana na chakula anacho kula na vitu vinavyo mzingira.

Jinsi Ya Kujifungua Mtoto Shupavu: Kula Chakula Chenye Afya

Mama, unapo kula chakula cha watu wawili, kumbuka kuwa nyote wawili mnahitaji virutubisho vingi. Vya kuegemeza mabadiliko ya kasi yanayo tendeka. Mtoto wako anapo kuwa katika safari ya kubadilika kutoka seli moja hadi kuwa kiinitete, seli za ubongo zina hitaji virutubisho tosha. Hii ndiyo sababu kwa nini lishe ya utunzaji kabla ya kujifungua ni muhimu. Hakikisha kuwa unakula vyakula vinavyo faa kupata virutubisho muhimu na wala sio kuchukua tembe.

Mbali na vitamini vya utunzaji kabla ya kujifungua, mama mjamzito anapaswa kuhakikisha kuwa ana kula matunda na mboga kwa wingi katika kila lishe.

Ongeza mayai kwenye lishe yako

eggs and heart disease

Kulingana na utafiti kwenye wanyama wa hivi karibuni ulio fanyika kwenye Chuo Kikuu cha Duke huko Durham, bidhaa inayo patikana kwenye mayai kwa wingi ina athari kuu kwa watoto wanao kua.

Panya wenye mimba walipatiwa kiwango cha choline zaidi ya mara tatu kiwango wanacho chukua kwa siku, na watoto wao walifuzu katika mitihani inayo husika na kusoma na uwezo wa kukumbuka. Ubongo wao uli imarika na kuwasaidia kukumbuka na kusoma. Vivyo hivyo, panya walio kosa choline kwenye lishe zao wali shuhudia matatizo ya kusoma.

Kuna wanawake wanao pata viwango vya chini vya choline wakiwa na mimba. Utafiti zaidi bado unafanyika kudhihirisha athari za choline kwenye lishe kwa wajawazito na watoto wao, miaka mingi baada ya kujifungua. Lakini kabla ya matokeo kutolewa na kuchapishwa, hakuna athari hasi kwa mama mwenye mimba kula mayai zaidi, njugu, nyama na vyakula vinginevyo vyenye wingi wa choline. Lakini hakikisha kuwa una wasiliana na daktari wako kabla ya kufanya hivi ili kuepuka matatizo yoyote yale.

Ni jambo la kusisimua kufikiria kuwa lishe ya mama mjamzito inaweza athiri jinsi ya kujifungua mtoto shupavu. Mbali na hayo, utafiti ume dhihirisha kuwa, kula vyakula vyenye afya ukiwa na mimba kuna epusha matatizo yanayo husika na umri yanayo weza kuathiri uwezo wa kukumbuka kwa watoto.

Soma Pia: Kuumwa Na Miguu Katika Ujauzito Unapokuwa Umelala

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio