Jinsi Ya Kujitayarisha Kuitwa Mama: Mambo Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Na Mimba

Jinsi Ya Kujitayarisha Kuitwa Mama: Mambo Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Na Mimba

Baada ya kuchagua majina utakayo waita watoto wako, safari ya kujitayarisha kuwa mama inaanza rasmi. Kuna baadhi ya wanawake ambao huwa na majina ya watoto kabla ya kupata mimba huku wengine wakitafuta majina ya watoto wao uchungu wa uzazi unapo anza. Haijalishi upande ulioko.

Jinsi Ya Kujitayarisha Kuwa Mama

Fanya mazoezi

kujitayarisha kuwa mama, mimba, mazoezi

Hakikisha kuwa una utayarisha mwili wako vilivyo kubeba mtoto na kujifungua, kuepuka matatizo yanayo andamana na kuto kuwa mzima wa afya unapo jifungua. Ukienda vipimo kabla ya kupata mimba, daktari wako atakushauri kuwa, ikiwa hauna uwezo wa kukimbia mbio za masafa marefu, hauko tayari kubeba mimba. Hakikisha kuwa una fanya mazoezi ili uwe na uzani unao faa na afya nzuri kabla ya kutunga mimba. Baada ya kutunga mimba, endelea kufanya mazoezi na wala usilegee. Jipe angalau dakika 30 kila siku za kufanya mazoezi ama ujiunge na darasa za wanawake wenye mimba. Kufanya mazoezi kuna kusaidia kuto choka ovyo unapokuwa na mimba na kufanya mchakato wa kujifungua kuwa rahisi.

Kula vyema

Jinsi Ya Kujitayarisha Kuitwa Mama: Mambo Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Na Mimba

Katika mimba, utakuwa na matamanio ya kula vyakula tofauti, hasa vyenye sukari kama vile ice cream, huku ukichukia vyakula vingine. Hakikisha kuwa unakula vyakula vyenye afya, protini, iron na kalisi ya kutosha na folic acid ni muhimu sana kwa mtoto wako. Nunua matunda, njugu, maziwa ya bururu kwa wingi. Virutubisho ni muhimu sana katika kipindi hiki, na vitasaidia katika ukuaji wa mtoto wako. Punguza ulaji na unywaji wa vibanzi na soda.

Punguza kiwango cha kafeini

Jinsi Ya Kujitayarisha Kuitwa Mama: Mambo Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Na Mimba

Wataalum wa afya katika ujauzito wana washauri wamama wenye mimba, na wanao jaribu kupata mimba kupunguza kiwango chao cha kafeini hadi miligramu 200 kwa siku. Kwa wale walio na uraibu wa kuchukua kahawa kila siku kabla ya kuanza siku yao, endelea lakini hakikisha kuwa unapunguza kiwango chako.

Koma kuvuta sigara

Utumiaji wa sigara hufanya iwe vigumu kwa mama kutunga mimba, lakini unapo bahatika na kupata mimba, unashauriwa kukoma kuzitumia punde tu unapo fahamu kuwa unatarajia. Kutumia sigara ukiwa na mimba kunakuweka katika hatari ya kujifungua kabla ya wakati, kupata mtoto mwenye uzani wa chini ama hata kuharibika kwa mimba.

Koma kutumia vileo

Jinsi Ya Kujitayarisha Kuitwa Mama: Mambo Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Na Mimba

Unapaswa kukoma kutumia vileo kabla ya kupata mimba, unapo anza juhudi za kutunga mimba. Kunywa pombe na vileo vingine ukiwa na mimba kuna muweka mtoto wako katika hatari ya kuzaliwa akiwa na matatizo ya kiafya, ya kusoma akiwa mkubwa ama kuzaliwa akiwa na uzito mdogo.

Chukua folic acid

faida za scent leaf unapokuwa na mimba

Folic acid ni muhimu sana katika kuhakikisha kuwa mtoto hazaliwi na changamoto zozote za kiafya. Unapo tunga mimba, hakikisha kuwa unachukua kipimo unacho shauriwa kila siku. Vyakula kama mboga za kijani, maharagwe na matunda huwa na viwango vya folic acid, lakini ni vyema kuchukua tembe ili kufikisha kiwango kinacho hitajika.

Fanya vipimo mara kwa mara

Baada ya kufanya kipimo cha mimba na kudhihirisha kuwa una tarajia mtoto, wasiliana na daktari wako ama utembelee kituo cha afya kilichoko karibu nawe. Utaanza vipimo vyako kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa na afya yako pia haina tatizo. Unapaswa kuendeleza vipimo hivi ili daktari afuatilie ukuaji wa mimba yako hadi mwezi wa mwisho kabla ya kujifungua.

Mtembelee daktari wako wa meno

Jinsi Ya Kujitayarisha Kuitwa Mama: Mambo Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Na Mimba

Ikiwa hupendi kumtembelea daktari wako wa meno mara kwa mara, huu ndio wakati bora kwako kumfanya rafiki yako. Mimba huongeza nafasi zako za kupata maradhi ya ufizi, tatizo la kiafya ambalo huenda likamfanya mama kushuhudia uchungu wa uzazi usio komaa. Hakikisha kuwa unaenda kuangaliwa meno mara kwa mara, yana safishwa ipasavyo na kusuguliwa baada ya kila mlo.

Kuwa mwangalifu wa uzito wako

kujitayarisha kuwa mama, mazoezi

Kuwa mnene sana ama mwembamba sana kuta fanya iwe vigumu kwako kupata mimba. Pamoja na kufanya iwe rahisi kwako kupata magonjwa kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu. Fanya mazoezi ili kuwa na uzito wa wastani, kwa njia hii, safari yako ya mimba itakuwa rahisi na pia uchungu wako wa uzazi hautakuwa mrefu. Daktari wako ata kushauri zaidi jinsi ya kutunza uzito wako.

Panga matumizi ya mtoto wako

Jinsi Ya Kujitayarisha Kuitwa Mama: Mambo Muhimu Ya Kufanya Ukiwa Na Mimba

Jambo ambalo wanandoa wengi hukosea ni kupata mtoto kabla ya kujipanga vyema kifedha. Anza kwa kununua mavazi ya mtoto wako. Ikiwa hujafanya ultrasound ya kukusaidia kufahamu jinsia ya mtoto unaye tarajia, nunua mavazi ambayo yanaweza valiwa na watoto wa jinsia zote mbili. Panga pesa utakazo hitajika kutumia kwenda kumtembelea daktari wako kila mara. Kununua bidhaa kama chupa za kumlishia mtoto na mahitaji mengine kabla ya kuzaliwa.

Punguza kazi unazo fanya

Kulingana na kazi unayo fanya, ni vyema kufahamu kuwa kazi nyingi katika mimba sio salama kwa afya yako na ya mtoto. Punguza kazi unazo fanya, unashauriwa kutafuta mtu wa kukusaidia na kazi zako za kinyumbani huku ukizidi kujitayarisha kuwa mama. Kwa wamama wanao amua kufanya kazi hadi siku ya mwisho, ni vyema kuhakikisha kuwa hawana fikira nyingi kwani zita hatarisha mimba yao. Ukihisi kuwa umelemewa na kazi na una tatizika kusimama kwa muda mrefu unapokuwa kazini, wasiliana na daktari wako ili upate mapumziko. Pumzika uwezavyo hasa katika trimesta yako ya mwisho. Utahitaji nguvu nyingi katika uchungu wa uzazi, kujifungua na baada ya kujifungua.

Soma PiaVitamu Tamu Vitano Wakati Wa Ujauzito

Written by

Risper Nyakio