Jinsi Ya Kujua Iwapo Mungu Amekutumia Mchumba. Fuata Vidokezo Hivi!

Jinsi Ya Kujua Iwapo Mungu Amekutumia Mchumba. Fuata Vidokezo Hivi!

Watu wengi wana ndoto na malengo ya kupatana na watu walio umbwa kwa ajili yao. Tuna angazia jinsi ya kujua iwapo Mungu amekutumia mchumba. Fahamu zaidi!

Mungu huwajulisha watu iwapo wana mtu anaye faa? Iwapo ni kweli, ni jinsi gani ya kujua iwapo Mungu amekutumia mchumba wako? Watu wengi huota kuhusu kupata na kumpenda mtu huyo mmoja, yule ambaye aliumbwa kwa ajili yao. Baada ya haya, matarajio ni kuishi pamoja kwa furaha hadi milele.

Jinsi ya kujua iwapo Mungu amekutumia mchumba

how do you know if god sent your mate

Kuwa makini na kazi zako

Kwenye bibilia, watu wengi walipata wachumba wao pahali wanafanya kazi. Adamu alimpata Eva baada ya kuwapa majina wanyama wote shambani. Mtumwa wa Ibrahimu aliye tumwa kumtafutia Isaka mke alimpata Rebekah alikuwa akiwapatia mifugo wa babake maji. Ruth alimpata Boaz alipo enda kumfanyia kazi.

Mifano hii yote inaonyesha kuwa watu hawa hawakuyasimamisha maisha yao ili kupata mchumba. Walikuwa nje wakifanya kazi wakati ambapo wachumba wao walitokea. Unapaswa kufuata mifano hii. Maliza masomo yako, fanya kazi kwa bidiii kazini mwako na ujitahidi kuyaweka maisha yako yawe sawa. Mchumba wako atatokea njiani.

Kwa hivyo kuna uwezekano kujua iwapo Mungu amekutumia mchumba?

Oa mtu anaye amini vitu sawa na wewe

Bibilia inasema kwamba hupaswi kuwa na mzigo usiokuwa sawa mgongoni, kumaanisha kuwa unapswa kutafuta mtu anaye mwamini Mungu kama wewe. Kuna wanandoa wengi duniani leo walio wa dini tofauti, ila sio jambo mbaya, sio jambo la busara kuoa mtu na kumlazimisha kubadili dini yao.

Unajuaje iwapo Mungu amekutumia mchumba iwapo hawana imani sawa na zako? Unapaswa kuangalia kwa kina sana katika sehemu hii.

Utajuaje iwapo Mungu amekutumia mchumba? Omba na uamini

Jinsi ya kujua iwapo Mungu alikutumia mtu  wakati ambapo umekuwa ukiomba kuwapata, bila shaka! Lengo sio kuomba kwa Mungu na kumwuliza aitikie chaguo lako la mchumba. Unamkubalisha kufanya matakwa yake kutoka hapo mwanzoni. Katika kesi ya Rebekah, mtumwa aliye patiwa kazi ya kutafutia Isaka bibi aliomba na kumwambia Mungu ampe ishara. Alitaka mwanamke huyo kujitolea kumpa maji ya kunywa. Punde tu alipofika hapo, alifanya hivyo.

Huku kulilipa vyema kwani Isaka alimpokea bibi kwa mikono mikunjufu alipo letewa yeye. Mtumwa aliomba, kuamini na kufuata alipotokea. Ange ghairi maombi yake ya hapo awali, ila alibaki nayo binti yule alipofika.

Utajuaje iwapo Mungu amekutumia mchumba? Kuwa mchumba afaaye

jinsi ya kujua iwapo Mungu amekutumia mchumba

Ni kitu kimoja kumwaminia Mungu mtu anayekufaa, ila wewe pia ni mtu anafaa? Hapa ndipo kuji tathmini ni muhimu sana. Huenda ukahitaji kujifanyia kazi. Unapo tengeneza vitu muhimu unavyo taka kutoka kwa mwenzi wako, tumia orodha hiyo kuangalia iwapo una vitu hivyo kabla ya kuvitarajia kutoka kwa mtu mwingine. Kwa hitimisho, fanyia utu wako kazi, mavazi na kila kitu kitakacho kufanya uwe mtu wa kufurahia kuwa naye.

Remember, someone somewhere is also praying to meet you so you should make sure they like what they see when you show up.

Kuwa tayari wakati mapenzi yanabadilika na kuwa kitu kingine

Watu wengi wanafikiria kuwa uhusiano wa kimapenzi unadumu, na wanaingia kwenye uhusiano na matarajio ya hisia hizi kudumu hadi milele. Muda tu baada ya vipepeo kwenye tumbo vinakufa, huenda hata wakafikiria kutoka kwa sababu vitu vimebadilika sana na hawakuwa tayari kwa mabadiliko haya.

Ukweli ni kuwa mapenzi ni chaguo. Unajuaje iwapo Mungu amekutumia mchumba? Unapo chagua kubaki na wao haijalishi mabadaliko. Unapaswa kuwa na msingi wa nguvu zaidi kuliko hisia za mapenzi tu. Jenga urafiki utakao dumu misimu yote ya maisha. Watu wengi wamesema kuwa iwapo watapata nafasi ya kurudia tena, hawawezi wachagua wachumba wao.

Kwa wale ambao wanataka kujua jinsi ya kujua iwapo Mungu amekutumia mchumba, unapaswa kwanza kujua kuwa mapenzi ni chaguo. Unapaswa kumchagua mchumba wako muda baada ya mwingine.

 Utajuaje iwapo Mungu amekutumia mchumba? Tafuta washauri

jinsi ya kujua iwapo Mungu amekutumia mchumba

Washauri wenu wa uhusiano huenda wakawa wazazi, wachungaji wenu ama yeyote anaye kuwa na uhusiano ama uhusiano ambao unatamani. Washauri wema watakuelezea mambo yanayo tendeka nyuma ya milango kwenye uhusiano, sio mambo ya kupendeza tu unayo yaona nje.

Tafuta amani yako

Iwapo unasoma kurasa za uhusiano za mtandao, utapata kuwa watu wengi wanataka wenzi wanao waletea amani. Amani sio ukosefu wa kuto sikizana. Nyinyi wawili ni watu wanao jaribu kuwa kitu kimoja, kwa hivyo mtabishana mara kwa mara. Walakini, haipaswi kuwa hivi wakati wote. Uhusiano wenu haupaswi kuwa kiwanja cha vita.

Kumbukumbu: Bibletools.org

Marriagemission.com

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio