Jinsi ya kujua jinsia ambayo mama anatarajia. Kuna njia tofauti ambazo wanandoa wanaweza kutumia kufahamu jinsia ya mtoto wanayetarajia muda kabla ya kufanya ultrasound.
Jinsi ya kujua jinsia
Mapigo ya moyo

Ili kufahamu jinsia ya mtoto, mama anaweza kuzingatia jinsi moyo unavyopiga. Mwanamke mjamzito hufajiriwa na mapigo ya moyo ya mtoto na mbali na hayo, anaweza kufahamu jinsia ya mtoto wake. Ikiwa mtoto anapiga mapigo zaidi ya mara 120 kwa dakika, ni wa kike, na ikiwa anapiga mara chache, atakuwa wa kike. Kumbuka kuwa hakuna utafiti wa Kisayansi unaoegemeza hili mbali ni imani tu.
Ugonjwa wa asubuhi

Ugonjwa wa asubuhi na kichefuchefu ni baadhi ya dalili za mapema za mimba. Kuna baadhi ya wanawake wasiopata ugonjwa wa asubuhi huku wengine wakitatizika na hali hii hadi muhula wa mwisho. Kichefuchefu kinaweza msaidia mama kufahamu iwapo anatarajia mtoto wa kike ama wa kiume. Kwa wanawake wanaokuwa na mimba ya kike, hutatizika kwa sana na kichefuchefu kikali na kisichoisha, huku wanawake wanaotarajia watoto wa kiume hawatatiziki sana na ugonjwa wa asubuhi.
Sukari na shubiri
Mbinu ya tamu na chungu ama sukari na chumvi hutumika kubaini jinsia ya mtoto mjamzito anayotarajia. Mama mjamzito huwa na hamu ya kula vyakula tofauti katika kipindi cha ujauzito. Huku akipenda vyakula vingine, anavichukia vingine. Ikiwa mama anapata hamu ya kula vyakula vitamu tamu kama chokleti na switi, anatarajia mtoto wa kike. Na iwapo ana hamu ya kula vyakula chachu, atapata mtoto wa kiume.
Kuwa na chunusi usoni

Kwa muda mrefu, watu wameamini kuwa uso wa mama wakati wa ujuazito unazungumza kuhusu jinsia ya mtoto anayetarajia.
Ikiwa mama anapopata mimba uso wake unapata chunusi, kuna imani kuwa ana mimba ya kike na kuwa mtoto amechukua urembo wake. Ikiwa uso wa mama una ng'aa katika mimba, nafasi kubwa ni kuwa ana mimba ya kiume.
Bicarbonate
Bicarbonate imetumika kwa muda mrefu kubaini jinsia ya mtoto. Ikiwa baada ya kuchanganya bicarbonate na mkojo, inatoa mapovu, mama anatarajia mtoto wa kike, isipotoa mapovu, ana mimba ya kiume.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Lishe Ya Kupata Mtoto Wa Kike: Uhusiano Kati Ya Lishe Na Jinsia Ya Mtoto Katika Mimba