Jinsi Ya Kukabiliana Na Hamu Ya Ngono Kabla Ya Ndoa

Jinsi Ya Kukabiliana Na Hamu Ya Ngono Kabla Ya Ndoa

Hamu ya kufanya mapenzi ni asili kwetu sote iwapo una mchumba, umeoleka ama bado, wavulana kwa wasichana. Ni hisia asili kwetu sote ambazo kwa bahati mbaya ama nzuri hatuwezi epuka. Ni rahisi kwa wanandoa kutosheleza hamu zao za kufanya mapenzi ila inapofika kwa watu ambao bado hawajafunga pingu za maisha, ni hadithi tofauti sana. Kulingana na imani na itikadi zako huenda ukawa na mtazamo hasi ama chanya wa hisia hizi za kutaka kufanya ngono. Ila je, ni vibaya kuwa na hisia hizi hata kama huna chumba? Cha muhimu zaidi kukumbuka ni kuwa hisia hizi ni za kibiolojia. Makala haya yana angazia jinsi ya kukabiliana na hamu ya ngono kabla ya ndoa.

Kukabiliana Na Hamu Ya Ngono Kabla Ya Ndoa

hamu ya ngono kablya ya ndoa

Picha:pixabay

Umri wa kuanza kuhisi hamu ya ngono

Kama tulivyo sema hapo awali, hamu ya kutaka kufanya ngono ni asili na kawaida kwa kila mtu kufuatia biolojia yetu. Ni hamu hii ambayo huwafanya watu walioko kwenye ndoa kupata watoto kama vile ambavyo bibilia inatuhimiza kufanya. Umri wa wa vijana kuanza kuhisi hamu ya juu ya kufanya mapenzi huanza wanapokuwa umri wa miaka 18. Kwa wanawake, umri wa kuanza kuhisi hamu ya juu ya kufanya ngono huwa juu kidogo. Kutoka wanapokuwa miaka iliyo kati ya umri 20 na 30 na huzidi kuongezeka kadri miaka inavyozidi kupita. Katika umri huu kwa wanawake, vitu vidogo huamsha hamu yao ya kufanya mapenzi. Kuna sababu nyingi zinazo amsha hamu hii ni kama vile watu wa jinsia tofauti, wakati wa mchana, mzunguko wa kipindi cha hedhi, hisia zake na picha ama video anazo tazama.

Hamu hizi zisipo thibitiwa, huenda zikamfanya mtu afanye mambo mengi yasiyo sawa na hapo baadaye kujazwa na majuto baadaye. Kwa sababu hii, ni muhimu kwa kila mmoja wetu, haijalishi ama una mchumba ama la, kujua jinsi ya kuthibiti hamu zake za kutaka kufanya ngono. Kujua kuthibiti hisia zako za kimapenzi ni muhimu sana kwani utakapo olewa ama kuoleka utajua jinsi ya kuwa mwaminifu kwa mchumba wako. Je, njia za kudhibiti na kukabiliana na hisia za kufanya ngono kabla ya ndoa ni kama zipi?

Kujitenga na vitu vinavyo amsha hamu ya ngono

Baadhi ya vitu hivi ni kama video na picha za ngono, ama makala inayo ongelelea kuhusu ngono. Ni muhimu kwa kila mtu kuelewa mambo yanayo amsha hamu yake ya ngono. Kwenye dunia ambapo kuna mengi sana kwenye mitandao, ni muhimu sana kwa watu wasio na wachumba kujiepusha na vifaa ambavyo vita amsha hamu yao ya kufanya mapenzi. Bila shaka, unapojielewa, utajua kujikinga kutokana na vifaa hivyo ili kuyarahisisha maisha yako. Iwapo unajipata wakati mwingi ukifikiria kuhusu ngono unapokuwa peke yako, hakikisha kuwa uko miongoni mwa watu wakati mwingi ili kuepuka kuwa na mawazo mabaya.

Jinsi Ya Kukabiliana Na Hamu Ya Ngono Kabla Ya Ndoa

Picha:Shutterstock

Kuzikinga fikira zako

Hamu ya kutaka kufanya ngono hutoka akilini kwani huko ndiko homoni za hisia hizi zinatoka. Ni muhimu kwako kulinda fikira ulizo nazo kichwani, kwa kuepuka kufikiria mawazo ya kufanya mapenzi. Ikiwa unajipata una mawazo haya unapokuwa umekaa kitini peke yako ukiwa nyumbani ama unapokuwa kitandani muda tu kabla ya kulala, ni vyema utafute shughuli ya kufanya wakati huo. Kama vile kusoma kitabu ama kutazama kipindi unacho kipenda zaidi wakati huo. Hakikisha kuwa hauna fikira hasi ila kwa wakati wote una fikira chanya ambazo zinaendeleza maisha yako vyema.

Kufanya mazoezi

Njia bora zaidi ya kukabiliana na hamu ya ngono kabla ya ndoa ni kufanya mazoezi.  Hii ni njia iliyo dhibitika kuwa shwari kukabiliana na tatizo hili. Unapo pata hisia hizi, fanya mazoezi mepesi hata unapokuwa nyumbani. Kwa njia hii, utakuwa makini kwenye jambo unalofanya na kukufanya usahau fikira ulizo kuwa nazo za kufanya mapenzi. Mazoezi yamedhibitika kuwa na faida nyingi sana kwa mwili. Mbali na kupunguza hamu ya kufanya ngono, utabaki ukihisi vyema zaidi na pia kupunguza mkwazo wa fikira. Hakikisha kuwa una ratibisha mazoezi kwa ratiba yako ya kila wiki.

Jitenge na marafiki wabaya

Usipo kuwa makini, huenda ukakuwa mtumwa wa mawazo mabaya ama wa kufanya ngono. Marafiki unao kuwa nao wana amua pakubwa maisha utakayo ishi. Iwapo una marafiki wengi ambao wana amini sana katika ngono, hatakua na budi ila kufuata mkondo wao na kuwa kama wao. Lakini iwapo marafiki wako wana mwelekeo maishani na wanajua wanacho taka, watakusaidia kuwa na mwelekeo pia na utapata kuwa wakati mwingi unatumia wakati wako vyema ila si kwa kuwa na mawazo ambayo haikusaidii maishani. Wateme marafiki ambao wana uraibu huu ili kuhakikisha kuwa haufuati nyayo zao.

Jinsi Ya Kukabiliana Na Hamu Ya Ngono Kabla Ya Ndoa

Picha: Shutterstock

Epuka madawa ya kulevya na vileo

Kwa mara nyingi, watu wanao jihusisha katika matendo ya ngono kabla ya ndoa huwa na uraibu wa kutumia madawa ya kulevya. Kuhakikisha kuwa unajichunga na kuwa na maisha bora yenye mwelekeo, epuka kutumia mvinyo na madawa kwani huenda vitu hivi vikakufanya ukose kuwa na  uamuzi shwari na hivi kufanya ufanye matendo ambayo utakuja kujuta baadaye. Kwa hivyo kabla ya ndoa, epuka kutumia madawa yoyote yale na pia baada ya kuoleka ama kuoana kwani madawa haya huwa na athari hasi kwenye maisha yako.

Fuata vidokezo tulivyo orodhesha ili kukabiliana na hamu ya ngono kabla ya ndoa.

Vyanzo: webmd.com

 

Written by

Risper Nyakio