Tembe za emergency contraception ni njia ya kuepuka mimba baada ya kufanya ngono bila kinga. Tembe hizi zina fahamika kwa majina tofauti kama vile tembe ya asubuhi baada ama ECPs. Zinapaswa kuchukuliwa kabla ya siku 5 baada ya kujihusisha katika tendo la ndoa. Kwa tembe zisizo na nguvu zaidi, zinapaswa kuchukuliwa kabla ya siku tatu. Tuna angazia njia zaidi za jinsi ya kukomesha mimba baada ya siku moja.
Kuna baadhi ya wanawake wanao amua kutumia IUD. Kifaa hiki cha homoni ama kisicho na homoni kinamkinga mama dhidi ya kupata mimba. Mama anapo amua kutumia kifaa hiki, anapaswa kuhakikisha kuwa kimewekwa kabla ya siku tatu kuisha.
Jinsi ambavyo tembe za emergency contraception zinavyo fanya kazi

Kwa kawaida tembe hizi husaidia kuepusha kupata mimba kwa kuzuia kurutubishwa kwa yai. Mwanamke ana shauriwa kutumia tembe hizi mapema iwezekanavyo. Kunywa dawa hizi baada ya yai kurutubishwa hakuta epusha mimba.
Utafiti umedhibitisha kuwa moja kati ya wanawake wawili wanao tumia tembe za kudhibiti mimba wata tunga ujauzito. Hata baada ya kuchukua tembe hizi kabla ya siku tatu kuisha kutoka wanapo fanya ngono bila kinga. Kumbuka zinachukuliwa baada ya tendo la ndoa na sio kabla. Kufanya hivi hakutakuwa na matokeo chanya.
Kuna uwezekano wa kupata mimba hata baada ya kuchukua tembe za kudhibiti uzazi. Kwa hivyo ni vyema kwa mama kuenda kumwona daktari baada ya kujihusisha katika kitendo cha ndoa bila kinga.
Athari hasi za tembe za emergency contraception

Binti ana shauriwa kuchukua tembe hizi mara mbili kwa mwaka. Kuchukua mara zaidi kuna athari hasi kwa afya ya mwanamke.
Athari hizi ni kama vile:
- Maumivu ya kichwa
- Chuchu kuwa laini
- Kutapika
- Kichefu chefu
- Kuhisi joto jingi mwilini
Baada ya kuchukua tembe hizi, mwanamke huenda akapata kipindi chake cha hedhi siku chache kabla ama baada ya siku anayo zitarajia. Huenda zika sababisha upele usoni mwa mwanamke kufuatia kulegeza viwango vya homoni mwilini mwake.
Wasiliana na daktari unapo ona ishara hizi:
- Kuhisi uchungu katika tendo la ndoa
- Uchungu kwenye kitovu ama pelviki
- Uta wenye harufu mbaya kutoka kwa uke wako
- Kuvuja damu nyingi na kwa muda mrefu
Kutumia tembe za emergency contraceptive ndiyo jinsi ya kukomesha mimba baada ya siku moja iliyo dhibiti zaidi. Hakikisha kuwa una fuata maagizo ya daktari ama kutembelea kituo cha afya unapo hisi kuwa kuna kitu kisicho kuwa sawa.
Chanzo: webmd
Soma pia:Kuna Uwezekano Wa Kutumia Maji Na Chumvi Kuzuia Mimba?