Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Njia Za Kulala Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba

3 min read
Njia Za Kulala Katika Trimesta Ya Kwanza Ya MimbaNjia Za Kulala Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba

Kulala ipasavyo katika mimba kunamsaidia mama kuwa na starehe na kuto shinikiza tumbo. Tazama jinsi ya kulala katika trimesta ya kwanza ya mimba.

Iwapo uko katika trimesta yoyote ile ya ujauzito, inaweza kuathiri pakubwa uwezo wako wa kulala. Mabadiliko ya homoni huweza kubadilisha hali ya usingizi ya mwanamke mjamzito. Ni vyema kuelewa jinsi ya kulala katika trimesta ya kwanza ya mimba. Hii ni pamoja na jukumu la homoni na uwezekano wa matatizo wakati wa kulala.

Jinsi Ya Kulala Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba

jinsi ya kulala katika trimesta ya kwanza ya mimba

Katika awamu ya kwanza ya ujauzito, mama anaweza kulala kwa njia au pande yoyote ile. Hii ni bila ya kusababisha dalili yote hasi. Hata kama mama ataamua kulala kwa tumbo lake, katika hatua za mwanzo za ujauzito huwa hakuna hasara yoyote ile. Hisia mbaya zinaweza kusababishwa na uvimbe wa tezi za matiti.

Kwa wanawake wengi,  ni mwanzo tu wa mimba kukua. Kama kulala kwa tumbo kunasababisha maumivu na kero katika kifua ni muhimu kubadilisha tabia. Matatizo ya usingizi yanayotokana na ujauzito yanaweza kuwa mbaya zaidi. Pia matatizo mapya yanaweza kujitokeza kwa kila awamu ya ujauzito na kuanzisha changamoto mpya.

Sababu Za Kukosa Usingizi Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba

jinsi ya kulala katika trimesta ya kwanza ya mimba

Katika hii awamu ya ujauzito, mabadiliko kuu yanahusu hisia ambazo mwanamke anafaa kukabiliana nazo. Hizi ni kama vile wasiwasi, hofu na furaha kubwa ya kuwa mama. Kwa sasa mabadiliko ya mwili bado yapo mbali ila yale ya homoni.

Ni wazi kuwa kila mwanamke huwa na mabadilliko mengi . Haya hutokana na kubadilika kwa homoni katika mwili wakati wa ujauzito. Katika hatua hii sababu kuu za Kukosa usingizi katika ujauzito huwa homoni na mchanganyiko wa hisia.

Sababu Za Homoni:

  • Kuongezeka kwa progesterone ambayo ni homoni muhimu katika kubeba mimba. Pia uterasi hujitayarisha kukubali kiinitete na hii husababisha kero kadhaa ambazo zinaweza kuingiliana na usingizi
  • Mwanamke huhisi uchovu mwingi wakati wa mchana. Mara nyingi hujiingiza katika usingizi mchana ambao husababisha ukosefu wa usingizi usiku.
  • Wakati wa usiku mama hulazimika kuamka mfululizo kukojoa inayosababishwa na ujauzito
  • Joto la mwili huongezeka ambalo linaweza kuathiri usingizi
  • Awamu ya usingizi mzito hupunguzwa kwa hivyo mapumziko hayafanyi kazi vizuri. Ni rahisi mama kujihisi mchovu asubuhi.
  • Kuwepo kwa kichefuchefu, asidi ni mambo ambayo hayasaidii katika kupumzika vizuri

Marekebisho ili Kupumzika Vizuri

  • Kupunguza usingizi alasiri kabla ya saa za jioni. Hii ni kwa kuwa kulala kwa muda mrefu zaidi ya wakati huu kunaweza kupunguza  hamu ya kulala jioni
  • Ikiwa una shida kulala usiku usisisitize. Ondoka  kitandani na usumbue akili yako kwa kusoma kitabu au gazeti. Hili husaidia katika kupumzika
  • Kutembea husaidia kupumzisha akili na kuhisi uchovu zaidi jioni
  • Kuwa na chakula cha jioni kidogo ili kupunguza usumbufu wa tumbo usiku
  • Kusikiliza nyimbo kabla ya kulala huwa na athari ya kutuliza
  • Kunywa chai ya mimea au limau ambayo husaidia kupumzisha misuli na kupunguza hali ya kichefuchefu na kutapika.

Njia za kulala katika trimesta ya kwanza ya mimba zinaweza kuwa nyingi na tofauti. Hii ni kwa kuwa mtoto bado hajaanza kuwa mkubwa. Ila Kadiri mimba inavyozidi kukua ndivyo njia za kulala zinavyozidi kuwa chache. Hili husababisha maumivu wakati wa kulala katika upande wowote ule.

Chanzo: healthline

Soma Pia: Sigara Katika Mimba Zina Madhara Gani Kwa Fetusi: Maswali Maarufu Katika Mimba

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Njia Za Kulala Katika Trimesta Ya Kwanza Ya Mimba
Share:
  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it