Tumia Vidokezo Hivi Unapokuwa Na Homa

Tumia Vidokezo Hivi Unapokuwa Na Homa

Homa ni mojawapo ya virusi vinavyo sumbua zaidi, makala haya yana kuelimisha jinsi ya kulala ukiwa na homa ili upate usingizi mwema zaidi.

Kulala ni mojawapo ya dawa bora zaidi inapofika kwa kupigana na homa. Ina saidia vyema na mfumo wako wa kinga, kuboresha uwezo wa mwili wa kupigana na virusi kabla vitambe zaidi mwilini. Na unapo gonjeka, usingizi tosha unakusaidia kulala vyema zaidi. Kwa hivyo, unapaswa kufanya nini uki kohoa ama unapo kuwa na homa na kufungana kunako kufanya uamke usiku? Mikakati hii rahisi inaweza kusaidia kudhibiti ishara za homa - ili upate usingizi unao hitaji. Jinsi ya kulala ukiwa na homa. Soma zaidi jinsi ya kulala ukiwa na homa.

Jinsi ya kulala ukiwa na homa: Vidokezo vitakavyo kusaidia

Je, utapata usingizi unaofaa vipi unapokuwa na mapua yaliyo fungana na kukohoa kunako kusumbua na kufanya iwe vigumu kwako kulala?

  • Jiinue kichwa

jinsi ya kulala ukiwa na homa

Shinikizo la sinus huwa bora kichwa chako kinapokuwa juu zaidi ya mwili wako. Unapo lala chini, postnatal drip yako inaweza fungana, na kufanya koo iliyo shikana kuanza kukohoa. Ongeza mito ili kuinua kichwa chako juu ya kitanda. Huenda uka pumua na kulala vyema.

  • Tumia kifaa cha vaporizer

Ishara za homa na kikohozi hufanya mfumo wako wa kupumua kukauka. Ongeza unyevu kwa hewa unayo pumua kwa kutumia kifaa cha vaporizer. Hakikisha kuwa kifaa chako ni kisafi wakati wote.

  • Kunywa na kula vitu moto

Tumia Vidokezo Hivi Unapokuwa Na Homa

Kupumua mvuke kutoka kwa vinywaji moto ama supu kunaweza kusaidia na mfumo wa kupumua ulio kauka na kufanya iwe rahisi zaidi kwako kupumua. Ongeza asali ili kutuliza koo yako na kusaidia unapo kohoa. Oga kwa maji moto kabla ya kulala.

  • Jaribu dawa za homa na kikohozi

Kuna dawa ambazo unaweza nunua kwenye zahanati za kusaidia na homa yako. Hakikisha kuwa una nunua dawa zinazo faa. Ikiwa hauna uhakika kuhusu ishara zako, uliza anaye kuuzia dawa hizo.

  • Usinywe vileo

Bila shaka itakufanya ulale, lakini itakufanya ukauke zaidi, kufurisha sinus zako na kuathiri vibaya homa yako. Ngoja hadi upone kisha uendelee na sherehe zako.

  • Fuata utaratibu wako wa usiku

Homa huenda ikafanya iwe vigumu kwako kuzingatia utaratibu wako wa usiku. Lakini ni vyema kuzingatia wakati unao enda kulala na kuamka hata ukiwa mgonjwa. Kufuata utaratibu wako wa kawaida, kuna fanya iwe rahisi kwako kulala na inaweza kusaidia kupigana dhidi ya homa. Soma moja lina shauri kuwa watu wasio pata usingizi tosha wana nafasi tatu zaidi za kupata homa ikilinganishwa na wanao lala masaa nane na zaidi kila usiku.

  • Kunywa kinywaji cha kukutuliza kabla ya kulala

jinsi ya kulala ukiwa na homa

Watu wengi hupoteza hamu yao ya kula wanapo kuwa na homa. Sio lazima uongeze idadi ya vinywaji unavyo kunywa unapokuwa mgonjwa, lakini lazima uhakikishe kuwa una maji tosha mwilini. Na vinywaji moto ni vizuri hasa wakati wa usiku.

  • Hakikisha unaoga kwa maji moto

Kuoga kwa maji moto ukiwa bafu kuna saidia kufungua mfumo wako wa kupumua, kupunguza kamasi iliyo shikana na kusafisha mfumo wako wa hewa. Pia ni njia nzuri ya kupumzika baada ya siku mrefu.

  • Lala peke yako

Unapo kuwa mgonjwa, ni vyema kulala mbali na mchumba wako. Kwa njia hiyo, unapunguza hatari za kusambaza ugonjwa. Na unaweza kohoa ama kuchemua bila kumwamsha mwingine.

Ikiwa una tatizika kulala, jaribu kusoma kitabu, kusikiliza muziki, ama kunywa chai moto. Kisha ujaribu kulala baada ya dakika 15-30.

Chanzo: WebMD

Soma Pia:Mwongozo Wa Vinywaji Vyenye Afya Vya Watoto Kuzuia Uzito Mwingi Kwa Watoto

Written by

Risper Nyakio