Jinsi Ya Kulea Wasichana Shupavu Wenye Maarifa Wasio Jua Maana Ya 'Siwezi'

Jinsi Ya Kulea Wasichana Shupavu Wenye Maarifa Wasio Jua Maana Ya 'Siwezi'

Vidokezo hivi muhimu vitawafaidi wavulana wako pia!

Sote tunafahamu jinsi watoto wanavyo penda teknolojia. Wanaipenda jinsi wadudu wanavyo penda mwangaza kutoka wakiwa na umri wa chini, mtoto anajua jinsi ya kutumia simu. Vidole vyao vidogo vinapo ibonyeza simu, vinafungua dunia mpya yenye nafasi nyingi. Walakini, wasichana bado wana ambiwa kuwa tasnia ya teknolojia sio yao na jambo hili hunisumbua sana. Ni muhimu kulea wasichana shupavu wasio na uwoga.

Huenda ikawa ni kwa sababu kama mwanamke aliye kwenye tasnia ya teknolojia bado nafikiria kuhusu riwaya iliyo andikwa na mhandisi wa kampuni ya Google (ambaye alipigwa kalamu) iliyo sema, mwanya wa jinsia ya wanawake kwenye kazi za teknolojia ni kwa sababu ya tofauti za kibailojia. Kwa mfano, imani isiyo ya kweli kuwa wanawake hawana hamu kubwa ya kazi zinazo wakwaza sana kwa sababu wana ogopa sana. Yote hayo sio kweli!

Hii ilinifanya nifikirie jinsi sisi kama wazazi, tunaweza panda mbegu kwenye watoto wetu zitakazo kua kuwapa wasichana kibali na kuwahimiza kuhusika kwenye majukumu ya kiteknolojia, na kwa wavulana kutarajia wasichana kuchangia kiasi sawa nao. Jibu nililo pata ni kuanza mapema.

Fikiria kulihusu

Ni vigumu kutupilia mbali tabia za kitambo. Baadhi ya jumbe tulizo sikia tukiwa wadogo hujirudia hadi wa leo zinaweza fanya tuamini imani zisizo za kweli za kijinsia na kuthibiti vitu ambavyo watoto wetu wana amini kuwa vinawezekana. Ni muhimu kujua ni jumbe gani tuna jaza kwa watoto wetu kuhusu jinsia hii.

raising strong and confident daughters

Kwa mfano, iwapo kompyuta ya nyumbani itaharibika na inahitaji mtu anayefanya kazi kwenye duka kuitengeneza, hii si kwa sababu kutengeneza ni 'kazi ya mwanamme', ila kwa sababu (ambaye huenda akawa ni mwanamme) amekuza maarifa yake katika nyanja hiyo.

Mhimize kuuliza maswali

Najua unajiuliza - "wao huuliza 'kwa nini' mara nyingi sana!" Ninacho maanisha ni kuwa wana paswa kusoma jinsi ya kufikiria peke yao na kuwa sawa na kufanya hivyo.

Kuuliza 'kwa nini na jinsi' kutawafanya wapate hamu ya kukuza na kutaka kujua mambo na iwapo kuna njia bora za kufanya mambo. Huenda mtoto wako aka ibua vitu ama kuwa mwanzilishaji, mwana biashara ama kitu chochote ambacho angependa kuwa lakini jambo hili hutendeka wanapo fahamu jinsi ya kufikiria peke yao. Hii ni njia bora ya kulea wasichana shupavu wasio na uwoga hata kwenye umati wa watu.

raising strong and confident daughters

Wape mtazamo wa kuto kata tamaa

Wahamasishe wanao kujaribu kujiuliza maswali kuhusu vitu na kuto puuza maswali yao. Iwapo kuna kitu ambacho hawawezi fanya, wakumbushe kuwa hawashindwi kwa sababu wao sio wazuri katika nyanja hiyo.

Ila, ni kwa sababu bado hawajapata maarifa ya kufanya jambo hilo. Wahimize kusoma zaidi kuhusu jambo hilo, omba usaidizi na kuendelea kufanya majaribio tena na tena.

Amuru na tarajia heshima

Kupuuza hata aina kidogo ya kuto heshimiwa hutuma ujumbe wenye nguvu -  kuwa aina yoyote ya kuto heshimiwa ni hatari.

Kuwacheka wasichana kwa sababu ya wanavyo kaa ama kutumia jinsia kama tusi, 'usirushe kama msichana' ama 'wavulana hawalii' kuna endeleza ubaguzi wa kijinsia na kufanya watu wasikuheshimu. Kijana wangu atakua akifahamu kuwa nafanya kazi za teknolojia kama msichana, na hilo ni jambo nzuri!

Mawingu ndiyo mwisho

Soma jinsi na usherehekea wanawake wanao ongoza kwenye tasnia zao na watoto wao, hasa wanao heshimika na kufahamika. Wanawake kama Hedy Lemarr aliye ibua teknlojia ya mazungumzo inayo kuwa kwenye WiFi, GPS, Bluetooth na karibu kwenye kila kifaa cha mazungumzo cha siku hizi!

Ukweli ni kuwa, tunahitaji wanawake zaidi kwenye tasnia kama ya teknlojia. Sio kwa sababu tunataka tu kusawasisha usawa kati ya wake kwa waume, mbali kwa sababu tuna mengi ya kuchangia kwenye nyanja hii!

Wasichana wetu wanaweza fanya mengi zaidi kuliko kutuonyesha jinsi ya kutumia kifaa cha kubadilisha programu kwenye televisheni (iwapo bado hawaja fanya hivi). Tunapo wahamasisha wasichana wetu na kuwatia imani kuwa wanaweza fanya kazi kwenye nyanja yoyote wanayo taka, naamini kuwa tuta nufaisha jamii yote, hata wavulana wetu.

Makala haya yaliandikwa mara ya kwanza na

Christie Whitehill (mwana biashara na mentor kwenye nyanja ya teknolojia Australia)

Makala haya yali chapishwa tena na idhini kutoka kwa Kidspot

Soma pia: Study: Ishara Tatu Zinazokuonyesha Kuwa Ni Wakati Wa Kuacha Kufanya Kazi Katika Ujauzito

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio