Siri Ya Kumfanya Mtoto Alale Imefichuliwa!

Siri Ya Kumfanya Mtoto Alale Imefichuliwa!

Ni kawaida kwa wazazi kukwazwa kimawazo watoto wao wanapo tatizika kulala. Makala haya yana kushauri jinsi ya kutatua shida hii.

Ikiwa tayari wewe kama mzazi una fikira nyingi, na ungependa kujua jinsi ya kumfanya mtoto alale, ili wewe pia upate wakati wa kupumzika. Tulia na upumue. Kuna njia zilizo jaribiwa na kudhibitishwa zinazo kuonyesha jinsi ya kumfanya mtoto wako alale, na baada ya hayo, unaweza pumzika pia.

Kwa nini mtoto wako halali vizuri?

kumfanya mtoto alale

Kuna sababu nyingi kwa nini mtoto wako halali. Unapo gundua kinacho mtatiza kulala, jinsi ya kumfanya mtoto alale itakuwa rahisi sana.

  • Wakati wa kulala usio kawaida

Mtoto anaweza tatizika na kuto pata usingizi usipo ratibishwa wakati haswa wake wa kulala. Kwa watoto wasio na wakati dhabiti wa kulala huwa vigumu sana kwao kulala kwa urahisi. Kwa sababu hii, huenda wakawa hawana usingizi wakati anapo paswa kuwa akilala.

  • Mazingira ya kulala yasiyo faa

Unapaswa kuhakikisha kuwa chumba cha kulala cha mtoto wako kinafaa. Mazingira yanaweza athiri mtindo wa mtoto wako wa kulala kiasi cha kumfanya kukosa kulala. Kila kitu kutoka kwa rangi ya kuta hadi kwa kelele chumbani hicho. Kagua chumba kuhakikisha kuwa hakuna mbu na wadudu wengine. Pia, hakikisha kuwa chumba hakina joto ama baridi sana.

  • Maradhi ya mwili ama kukosa starehe

Kukosa usingizi kwa mwanao huenda kukawa ni kufuatia aina yoyote ya kuto starehe. Ikiwa ungependa kujua jinsi ya kumfanya mtoto alale, unapaswa kuhakikisha kuwa hana tatizo la sleep apnea. Sababu zingine ambazo huenda zika athiri usingizi wake ni asthma, matatizo ya ngozi, homa, kuumwa meno yanapo kua, ama kuumwa na masikio.

  • Matatizo ya kihisia na kisaikolojia

Inapofika kwa mtoto kukosa kulala, huwezi puuza sababu kuwa hofu mnapo tengana ama ndoto mbaya. Matibabu yanayo tumika kusuluhisha tatizo hili pia huenda yakamfanya mtoto kukosa kulala.

Jinsi ya kumfanya mtoto alale

kumfanya mtoto alale

Kama tulivyo taja hapo awali, unapaswa kujua kinacho mfanya mtoto kukosa kulala ili ufahamu jinsi ya kumfanya alale. Huku kuna maana kuwa suluhu halitakuwa bora kwa watoto wa kila mtu. Walakini, unaweza tafuta chanzo cha kukosa usingizi na ujaribu kupata suluhu inayo tatua kila kesi.

Hapa kuna njia ambazo unaweza tatua tatizo la mtoto wako kuto lala:

1. Kuwa na utaratibu wa kulala

Utahitajika kutengeneza ratiba ya kulala na kuhakikisha kuwa mtoto wako ana lala wakati fulani kila siku. Kutafanya apate uraibu wa kufanya hivyo, lakini usimlazimishe. Usikate tamaa unapo mpeleka mtoto kitandani kulala kisha wana kufuata unapo toka. Warudishe kwa upole. Baada ya wakati, miili yao itazoea.

2. Hakikisha chumba cha mwanao kina starehe tosha

Joto ya chumba hicho inapaswa kuwa sawa. Pia, unaweza badilisha godoro lake ili kuhakikisha kuwa hivyo sio vyanzo vya kuto lala kwa mwanao. Tafuta neti na uhakikishe mwanao analala chini ya neti asikuliwe na mbu.

3. Usimlishe chakula kingi karibu na wakati wake wa kulala

Chakula kingi akiwa karibu kulala kitamfanya mtoto akose starehe. Chajio inapaswa kuwa nyepesi. Pia, vinywaji kama chai sio wazo nzuri akiwa karibu kulala. Kwa watoto wanao kojoa kitandani, punguza vinywaji baada ya chamcha.

4. Katisha tamaa vitendo vitakavyo mfanya kuwa makini karibu na masaa ya kulala

Zima televisheni na uchukue vifaa kama rununu usiku. Ikiwa unataka kufahamu jinsi ya kumfanya mtoto kulala, unapaswa kuchukua vidoli na vitu vya kucheza vitakavyo mfanya kuwa makini wakati anao paswa kuwa akilala.

Mtoto anapo kosa kulala mzazi hufilisika kimawazo. Ikiwa ungependa kujua jinsi ya kumfanya mtoto alale, unaweza suluhisha tatizo lake la kuto lala na kuboresha utendaji kazi wa kawaida wa mwili wake.

Vyanzo: NHS

Soma pia:Orodha Ya Matibabu Bora Ya Kinyumbani Ya Homa Katika Mtoto Aliyezaliwa

Written by

Risper Nyakio