Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Ushauri Wa Kimapenzi Kwa Wanaume: Jinsi Ya Kumpenda Mwanamke

2 min read
Ushauri Wa Kimapenzi Kwa Wanaume: Jinsi Ya Kumpenda MwanamkeUshauri Wa Kimapenzi Kwa Wanaume: Jinsi Ya Kumpenda Mwanamke

Mwanamme anayejua lugha ya kimapenzi ya mke wake ana nafasi zaidi za kuelewa anachotaka. Lakini sio wanaume wengi wanaokuwa makini kufahamu lugha ya mapenzi ya wake zao.

Wanaume wengi huhisi kuwa hawaelewi jinsi wake zao wanavyotaka kupendwa. Sio jambo gumu kumpata mwanamme akisema kuwa wanawake ni viumbe vigumu visivyoeleweka. Baada ya kumfanyia kitu kimoja, atazidi kukasirika na kuitisha kingine. Huenda wakati mwingine wakahisi kuwa hawajui jinsi ya kuzungumza na wake ama wenzi zao. Inapofika kwa kupenda wanawake, wanaume wengi huhisi kuwa kuna siri ambayo haijavumbuliwa bado. Katika makala haya, tunaangazia jinsi ya kumpenda mwanamke na vitu ambavyo wanawake wanatarajia na wasivyo tarajia kutoka kwa waume zao.

Jinsi Ya Kumpenda Mwanamke

jinsi ya kumpenda mwanamke

Wanaume wengi wanapenda kulegea na kutotia juhudi katika kuwaonyesha wake zao kuwa wanawapenda. Na kusema kuwa wao si weledi wa vitendo vya kimapenzi. Matendo ya kimapenzi yanachangia pakubwa katika mahusiano yetu kuwa na afya. Punde tu baada ya kufunga ndoa, wanaume wengi hutupilia mbali matendo ya kimapenzi. Haifai kuwa hivi. Vitendo hivi vinapaswa kuzidi hata katika ndoa.

Kuzidisha kumwonyesha mke wako mapenzi hata baada ya ndoa ni muhimu katika kuhakikisha kuwa ndoa yenu inafuzu. Kunamdhihirishia mwanamke kuwa ungali unampenda, na utazidi kumtunza. Matendo hayana faida kwa mwanamke tu, mbali kwa mwanamme pia. Mwanamke mwenye furaha anahakikisha kuwa nyumba yake ina furaha pia.

Mambo ya kimapenzi ya kumfanyia mke wako

  • Mnunulie maua mara kwa mara. Usingoje siku ya Valentine's peke yake ili umnunulie maua. Fanya hivi hata asipotarajia.
  • Mnunulie vitu anavyopenda. Ikiwa anapenda chokleti, usingoje hadi anapokuwa ana sherehekea siku yake ya kuzaliwa ili kumnunulia vitu hivi.
  • Usimwulize zawadi anayotaka. Sikiliza kwa makini anapoongea kuhusu vitu anavyovitamani kisha umnunulie. Kufanya hivi kunamwonyesha kuwa unamjali na uko makini na vitu anavyovipenda.

Mambo ambayo kila mwanamke anatarajia kutoka kwa mume wake bila kuuliza

jinsi ya kumpenda mwanamke

  • Kuenda likizo mara kwa mara. Kupumzika baada ya kuitunza familia na kukwazwa kimawazo na kazi
  • Kupikiwa mara kwa mara. Sio jukumu la mwanamke kupika wakati wote, mwanamme anaweza chukua jukumu hili mara kwa mara.
  • Kumsaidia na kazi za kinyumbani. Kama vile, kuwalaza watoto, kuwasaidia na kazi za ziada na hata kusafisha vyombo mara kwa mara.

Mwanamme anayejua lugha ya kimapenzi ya mke wake ana nafasi zaidi za kuelewa anachotaka. Lakini sio wanaume wengi wanaokuwa makini kufahamu lugha ya mapenzi ya wake zao. Lugha ya mapenzi ni nini hasa? Hii ni njia ama vitu ambayo vinamfanya mwanamke huhisi kuwa anapendwa. Huenda ikawa ni zawadi, kumpa wakati wako, kumsaidia na kazi, kumshika ama maneno matamu.

Soma Pia: Kwa Nini Watu Wasio Na Usawa Hawawezi Kuwa Na Uhusiano Wa Kimapenzi?

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Relationship & Sex
  • /
  • Ushauri Wa Kimapenzi Kwa Wanaume: Jinsi Ya Kumpenda Mwanamke
Share:
  • Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

    Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

  • Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

    Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

  • Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

    Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

  • Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

    Imani za Kuchumbiana Zisizo za Kweli Unazostahili Kujua

  • Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

    Koma kufanya Hivi Ili Kuboresha Maisha Yako ya Kingono

  • Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

    Sababu 3 Kwa Nini Unapaswa Kuongeza Mara Unazofanya Mapenzi Kwa Siku

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it