Jinsi Ya Kuwasaidia Watoto Waanze Kuongea Kwa Ufasaha

Jinsi Ya Kuwasaidia Watoto Waanze Kuongea Kwa Ufasaha

Watoto wengi huanza na majina kama vile "eeh", "ooh" wanapo anza safari yao ya matamshi na mazungumzo. Ila ni vyema kutia akilini kuwa safari ya mazungumzo huanza mapema wangali tumboni mwa mama yao. Kwa kusikiliza wazazi wao wanacho sema. Kwa wakati huu, wanaweza tofautisha kati ya sauti za wazazi wao na watu wengine. Mzazi huenda akapata shaka baada ya kugundua kuwa mtoto wake amechelewa kuanza kuzungumza. Tuna angazia kumsaidia mtoto kuongea kwa ufasaha.

when do babies say mama and really mean it

Lugha ya watoto

Hakuna ushuhuda unaonyesha wakati ambapo watoto huanza kutamka majina kwa ufasaha. Kuna baadhi ya watoto ambao huenda wakaanza kuzungumza mapema na wengine baadaye. Utafiti umedhihirisha kuwa utaratibu wa mazungumzo huanza mtoto anapokuwa tumboni mwa mamake. Na kwa sababu hii, wamama walio na mimba wana shauriwa kuanza kuwasomea watoto wao vitabu wangali wachanga.

Mtoto ana uwezo wa kutpfautisha sauti ya mamake na ya watu wengine angali tumboni mwa mamake.

Ni jambo la kawaida kwa wazazi wengi kushangaa umri ambapo watoto wataanza kuzungumza kwa ufasaha

Ukuaji wa watoto hukua tofauti. Wengine huanza kuongea wakiwa wachanga sana na wengine huenda waka kawia kidogo, hata kwa watoto kutoka kwa mzazi mmoja. Ila, hakuna kiwango cha kupima ukuaji wa watoto. Mazingira ambapo mtoto analelewa huathiri atakapo anza kuongea.  Wazazi wanashauriwa kuwa wasikilivu ili kujua mtoto wao anapo anza kuongea na kusema maneno yake ya kwanza. Kwa hivyo tuna angazia jinsi ya kumsaidia mtoto kuongea kwa ufasaha

 

when do babies say mama and really mean it

Jinsi Ya Kuwasaidia Watoto Kuboresha Uwezo Wao Wa Kuongea

Huenda ukagundua kuwa uwezo wa mtoto wako wa kuongea haukui kwa kiwango kinacho hitajika, na huenda ukawa unashangaa jinsi ya kumsaidia mtoto kuongea kwa ufasaha. Maswali mengine ambayo huenda ukawa nayo ni wakati ambapo ataanza kutamka majina kwa ufasaha, hasa majina ya kwanza kama vile mama. Lengo lako ni kuboresha uwezo wa mwanao wa lugha na mazungumzo.

Kuna baadhi ya hatua rahisi ambazo unaweza kuchukua kumsaidia mtoto wako kuongea. Hatua ya kwanza ni kuwa egemezo lake na kuhakikisha kuwa mazingira ni bora na yenye mapenzi. Hapa ni baadhi ya vitu ambavyo unaweza fanya:

1. Zungumza na mwanao

Hakikisha kuwa kila mara unamwongelesha mtoto wako. Kumwambia maneno kama "Unapendeza", "Wewe ni mrembo", na "Nakupenda". Waeleze jinsi siku yako ilivyo kuwa na mambo ambayo ungependa kutimiza maishani. Na unapofanya kitu mwanao akiwa karibu, hakikisha kuwa unamweleza unacho fanya. Mfunze kuhusu watu na vitu vinavyo mzingira. Mwimbie nyimbo za watoto na umfunze zilizo rahisi kwake.

Wataalum wa mazungumzo na lugha wana shauri lugha rahisi isiyo na ugumu wa kuelewa. Epuka kuongea kwa maneno magumu na mtoto wako. Kuongea kwa ufasaha na kutumia lugha rahisi kutamsaidia mtoto wako kuongea vizuri.

2. Kumsomea

Wataalum wa lugha ya watoto wanashauri wazazi kuanza kuwasomea watoto wao hadithi na mashairi wangali wachanga kwani kuna hamasisisha uwezo wao wa kuongea. Kulingana na watafiti, watoto wanapenda kusikia sauti ya wazazi wao. Mtoto wako atajua kutamka maneno unayo yasoma kutoka kwa vitabu.

Watoto wanafurahia matamshi ya mashahiri ya watoto ya kuliwaza. Ili kumsaidia mtoto wako kuongea kwa ufasaha, hakikisha kuwa unachukua muda wako kununua vitabu vizuri vya watoto, na utafurahia.

3. Kuwa makini na mtoto wako

Hakikisha kuwa haupuuzi mtoto wako anapo anza kutamka maneno kwa lugha ya kitoto. Huenda uka umiza hisia zao na kuwafanya wakate tamaa. Unapaswa kuwa makini na mtoto wako hasa anapo jaribu kuzungumza. Baada ya wakati mdogo, ataanza kutamka maneno ambayo yana eleweka.

Wazazi wote wangependa kuona watoto wao wakitimiza hatua muhimu maishani. Wamama wangependa kusikia watoto wao wakitamka jina mama na dada. Ni vyema kukumbuka kuwa watoto wote huwa tofauti na kila mtoto hufikisha hatua hizi katika wakati tofauti. Kuwa mpole na mtoto wako. Hatua rahisi kama vile kuongea na mtoto wako, kuwa sikiliza, kuwachezea muziki na kuwasomea vitabu kutawasaidia kuimarisha uwezo wao wa kuongea. Anza kufanya hivi na utaanza kushuhudia mabadiliko katika mtoto wako.

Kumbukumbu: BBC, The Telegraph

Soma pia: Tafadhali Nakuomba Usimbusu Mtoto Wangu

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio