Njia Bora Zaidi Za Kumwadhibu Mtoto Kwa Kuiba Pesa

Njia Bora Zaidi Za Kumwadhibu Mtoto Kwa Kuiba Pesa

Ni jambo la kuhuzunisha kwa mzazi kufahamu kuwa mtoto wake ana iba. Tazama njia bora za kumwadhibu mtoto wako.

Baadhi ya wakati, huenda mtoto wako akachukua kitu kisicho cchake na kusahau kukirudisha kwa mwenyewe. Kisa hiki ni tofauti na mtoto wako anapo chukua kitu cha mtoto mwingine maksudi na kukosa kukirudisha na mathumuni ya kujiekea. Kisa cha mwisho ni kuiba. Huenda uka vunjika moyo kujua kuwa mtoto wako huiba na ukawa na hamu nyingi ya kutaka kumwadhibu mtoto kwa kuibapesa na vitu vingine.

kumwadhibu mtoto kwa kuiba

Ukitaka kukomesha tabia hii, makala haya yana angazia hatua unazo paswa kufuata iwapo ungependa kujua jinsi ya kumwadhibu mtoto wako kwa kuiba pesa.

Kuiba ni nini?

Kulingana na Leah Davies, M.Ed., kuiba ni pale ambapo mtoto anapo chukua kitu kisicho chake bila kuomba ruhusa kwanza. Mara nyingi, mtoto hutmani kitu hicho na kutaka kiwe chake kwa kukichukua tu.

Kutoka umri wa miaka mitano hadi saba, mtoto hufahamu kuwa kitendo hiki ni kibaya na hii ndiyo sababu kwa nini wana danganya kukihusu ama kuhakikisha kuwa hakuna atakaye wapata kwa kitendo hicho.

Kwa nini watoto huiba?

Inapo fika kwa kuiba katika watoto, maksudi yao huenda ikawa tofauti kwa kila mtoto. Baadhi ya sababu kwa nini watoto huchukua vitu visivyo vyao huwa:

• Wameona watu wazima wakifanya hivyo

Kabla ya kuanza kufanya utafiti jinsi ya kumwadhibu mtoto kwa kuibapesa, kwanza unapaswa kuhakikisha kuwa hakuna mwanajamii anaye fanya kitendo sawa. Watoto wanapenda kuiga tabia za watu wazima walio karibu nao. Kwa hivyo iwapo wazazi ama walezi wanafika nyumbani na bidhaa kutoka ofisini zao, mtoto atasoma kuwa ni sawa kuchukua kitu chochote wanacho taka.

• Wanapendelea hisia ya kuiba

Kuiba bila kupatikana huja na aina ya hisia, ambayo huenda ikawa ya kutamanisha. Mtoto wako anapo pata hisia hii, huenda ikazidisha tatizo kwenye hatua ya kuchukua vitu hata asivyo hitaji ili kutosheleza hisia zake alizo zoea.

• Watoto huiba wanapo taka pesa za kuiba vitu ambavyo wazazi wao hawata wapatia

Baadhi ya watoto wata iba pesa kutoka kwa mikoba ya wazazi iwapo iwapo wamekataa kuwapatia pesa za mchezo mpya, kununua baiskeli ama vitu vinginevyo. Wana hamu ya kupata kitu chochote wanacho kitaka kwa mbinu yoyote na kujaribu kupata pesa kununua kitu hicho wao wenyewe.

• Baadhi ya watoto huiba pesa ku adhibu yeyote yule wanaye muibia

Kulipiza kisasi ni sababu kuu ya kuiba. Hautaelewa vyema kumwadhibu mtoto kwa kuibaiwapo hauelewi kuwa mtoto anaweza amua kuiba ili kumwumiza mtu mzima kwa kuchukua kitu ambacho mtu huyo ana kidhamini.

• Marafiki wao huiba pia

Hakuna kupuuza shinikizo la wana rika kama mojawapo ya sababu kwa nini watu wachanga huenda wakaiba. Iwapo marafiki wake ni wezi, pia wao wata fikiria kuwa ni sawa kuiba.

• Unyanyasaji na kupuuzwa

Mazingira ya unyanyasaji huenda yakamfanya mtoto kuanza kuiba. Hili huenda likaja ama likakosa kuja na hisia za hofu, kupuuzwa na uchungu. Pia, mtoto anapo puuzwa kwa kiwango ambacho mahitaji yake ya kimsingi haya toshelezwi, huenda wakawa wana iba kama njia ya kupigana na jambo hili.

• Baadhi ya watoto huiba ili wapatiwe umakini

Mtoto anapo fahamu kuwa kufanya tabia mbaya kutampa umakini wako, huenda wakajaribu kuiba ili uwape umakini wanao utafuta.

kumwadhibu mtoto kwa kuiba

Jinsi ya kumwadhibu mtoto kwa kuibapesa na vitu vingine

Haijalishi sababu yao ya kuiba, hiki ni kitendo kibaya na unapaswa kukaa chini nao na uwe na mazungumzo ya ndani na mtoto wako. Ni muhimu sana kuwafanya kuona makosa katika matendo yao. Kama mzazi ama mlezi, haupaswi kujilaumu sana kwa tabia yao. Hapa ni baadhi ya hatua ambazo unaweza chukua kutatua tatizo hili:

1. Fanya utafiti wa maksudi yao ya kuiba

Mazungumzo tuliyo shauri hapo awali yata ibua kwa nini mtoto wako alifanya alicho fanya. Baada ya kujua, unaweza rekebisha kisa hicho na uhakikishe kuwa hakita ibuka tena katika siku za hapo usoni.

2. Mfanye mwanao arejeshe chochote kile alicho kichukua

Iwapo una uhakika ungependa kujua baadhi ya njia za kumwadhibu mtoto kwa kuibapesa, haupaswi kuangalia aibu ya kwenda pamoja na mtoto wako kurejesha kile walicho kichukua. Hakikisha kuwa wame regesha chochocte kile walicho chukua, ikiwa ni pesa ama bidhaa.

3. Wahimize wakifanyie kazi

Katika kesi ambapo walisha tumia pesa walizo iba, unaweza waambia wazifanyie kazi kwa kusaidia na kazi za nyumbani kwa muda fulani.

4. Tazama uone iwapo wata rudia tabia ile

Baadhi ya watoto wataacha kuiba ukiwapata mara ya kwanza. Kwa bahati mbaya, kuna watoto ambao watafanya kitendo hiki kiwe mtindo. Ukimchunguza mtoto na ufahamu kuwa wanaendeleza tabia ile, unapaswa kupata ushauri kutoka kwa wataalum.

Ni kawaida kuhisi kana kwamba utakata tamaa mtoto wako anapo iba. Kwa bahati nzuri, unaweza rekebisha tabia hii kwa kufuata vidokezo hivi.

Kumbukumbu: KellyBear.com

FamilyEducation.com 

Soma pia: Tofauti Kati Ya Wazazi Wa Afrika Na Umarekani Na Mbinu Zao Za Ulezi

Written by

Risper Nyakio