Jinsi Ya Kumwanzishia Mtoto Wako Chakula Kigumu

Jinsi Ya Kumwanzishia Mtoto Wako Chakula Kigumu

Wataalum wa afya ya watoto wanashauri kuwa watoto wanapaswa kunyonya maziwa ya mama kwa miezi ya kwanza 6. Na kisha uanze kuwalisha vyakula vingine.

Baada ya miezi 6 ya kunyonyesha (peke yake bila chakula), ni wakati wa kumwanzishia mtoto wako chakula kigumu. Katika wakati huu, swali lililo kawaida sana ni jinsi ya kumwanzishia mtoto wako chakula kigumu. Huenda maswala mengine yakawa kiwango ambacho mtoto wako anapaswa kunywa, wakati bora wa kuanza mchakato wa kula na vyakula unavyo paswa kumlisha.

how to wean a baby in Nigeria

Hakuna umri hasa ama spesheli wa kumwanzishia mtoto chakula.  Cha muhimu ni kuhakikisha kuwa wewe na mtoto wako mna furaha, unaweza endelea kumnyonyesha hadi kwa wakati wa miaka miwili. Pia ni muhimu kujua kuwa wanapo patiwa wakati tosha, watoto huanza kula chakula wenyewe; na kupunguza wakati ambao wana nyonya na kuongeza idadi ya chakula kigumu wanacho kula; hadi mwishowe wanapo acha kunyonya. Tazama vidokezo hivi vya kufuata:

Vidokezo 10 Vya Jinsi ya Kumwanzishia Mtoto Chakula Kigumu

 Chagua wakati bora zaidi

Jinsi Ya Kumwanzishia Mtoto Wako Chakula Kigumu

The American Academy of Pediatrics (AAP) inashauri kuwa kwa miezi ya kwanza sita ya maisha ya mtoto wako, anahitajika kunyonya maziwa ya mama tu. Baada ya hapo kuchanganyishiwa vyakula vigumu na maziwa hadi pale anapo timiza mwaka mmoja. Ila, bila shaka kuanza kumlisha mtoto wako chakula ni hiari ya kipekee na inapaswa kuwa kulingana na hiari iliyo bora zaidi kwa familia. Huenda ukawa unarudi kazini na unahitaji kuanza kumlisha kwa kutumia chupa kwa mfano.

Kuwa mwangalifu kwa ishara za kuwa tayari

Ishara zinazo aminika kuwa mtoto wako mdogo ako tayari ni kama zipi? Mtoto wako anapaswa kuwa na uwezo wa kufanya yafuatayo:

  • Kukishikilia kichwa chake imara
  • Kuketi anapo saidiwa
  • Kuonyesha hamu ya chakula chako

Anzisha ratiba

Angalia kalenda yako: Chagua siku hasa unapo taka kumwanzishia mtoto wako chakula kigumu kunaweza saidia kupanga vyema. Kisha ujikubalishe mwezi mzima wa kumaliza kumpa chakula kigumu. Huku kuna saidia kumpatia mtoto wako nawe nafasi ya kupumzika ukikabiliana na matatizo kwenye safari hii.

Anzisha utaratibu

Kuzoea utaratibu wa kuanza kula chakula kwako na kwa mtoto wako kutasaidia. Kwa mfano, unaweza kosa kumnyonyesha mara moja kwa wiki; wakati ambao ni sawa kwako na ambapo mtoto wako hana hamu ya kunyonya. Na baadaye, punguza hisia hadi pale ambapo anatumia chupa ama vikombe ama kula vyakula vigumu.

Mwache mtoto wako aaongoze

jinsi ya kumwanzishia mtoto chakula kigumu

Baadhi ya watoto hufuzu wanapokuwa akitawala. Iwapo uko sawa na kumwacha mtoto wako atawale, itumie mbinu ya jaribio na ukweli "usimpe, asikatae". Kwa hitimisho, unam lisha anapo thibitisha hamu ya kutaka kula, ila itoke kwake. Sio mbinu ya kuanzisha chakula ya mbio zaidi, ila ina hakikisha kuwa mahitaji ya mtoto wako yanatimika.

Badilisha ratiba mara kwa mara

jinsi ya kumwanzishia mtoto chakula kigumu

Mwache baba, nyanya ama yoyote yule anaye kusaidia kuchukua jukumu hili la kumwanzishia mtoto chakula kigumu. Mtoto wako akikataa chupa kutoka kwako, La Leche League International ina shauri kuona iwapo mtoto wako atakubali chupa kutoka kwa mtu mwingine aliye kwenye chumba hicho. Ama iwapo wewe ndiye unampa chupa ile, kubadili ratiba hiyo kwa muda. Unaweza mshika vitofauti uone iwapo atakubali. Iwapo hii haitafanya kazi, rudia ratiba yako ya hapo awali kisha ujaribu tena baada ya wiki chache.

Kwa watoto wazee

Iwapo mtoto wako ni wa miezi tisa ama zaidi, ni vyema kujaribu kumwanzishia chakula kwa kumlisha kutoka kwa bakuli ama sahani ili usikumbane na tatizo la kumwachisha chupa baada ya siku chache. Na iwapo mtoto wako ana  zaidi ya mwaka mmoja, valia nguo ambazo zitamtatiza; kama vile rinda lililo na nyororo upande wa nyuma ama shati iliyo na vifungo hadi juu. Ili kupunguza nafasi za mtoto kujaribu kunyonya mara kwa mara na badala yake kujaribu kula chakula.

Epuka kufura

Sababu ingine ya kuanza polepole: kuanzisha chakula kwa mbio kuna weza sababisha kufura. Kwa nini? Mishipa yako ya maziwa haikujua kuwa inapaswa kupunguza utoaji wa maziwa. Na maziwa yote hayo hayana popote pa kuenda. Iwapo una fura, tuliza uchungu kwa kutumia vipande vya barafu ama acetaminophen. Ama ufikie pampu yako ya maziwa. Unaweza mpa mtoto wako maziwa hayo kwa kutumia chupa ama uchanganye na nafaka.

Elewa hisia zako

Sio mtoto wako peke yake ambaye anapaswa kubadilika anapo anza kula vyakula vigumu. Utakubaliana na hisia nyingi- baadhi ya wamama hutaka mili yao irudi kawaida; wengine wana hisi kana kwamba umetupiliwa nje mtoto wao anapo acha kunyonya. Hata ingawa huenda ukawa na furaha kuacha kunyonyesha na huenda mara na mara ukawa na fikira na hisia nyingi kufuatia kuzeeka kwa mtoto wako. Kumbatia uhuru wake, na ufahamu kuwa kumwanzishia chakula ni shuhudio la kihisia na uongee na wamama wengine wanao nyonyesha ambao wataelewa.

Pakua virutubisho

jinsi ya kumwanzishia mtoto chakula kigumu

Kuwaanzishia watoto vyakula vigumu kwa mara ya kwanza, wazazi wengi huwa anzishia watoto wao na pap Nigeria na uji Kenya. Baadhi yao huongeza nafaka kijiko kimoja kama vile cha wali na kuchanganya na maziwa ya ng'ombe hata ya mama. Anapo zoea uji na wali, unaweza ongeza maji ya sharubati ya mboga, matunda na nyama laini.

AAP inashauri kujaribu aina moja ya chakula kila mara na kungoja kwa angalau siku 2-3 kabla ya kuanza aina nyingine ili kuona iwapo mtoto ana shuhudia mzio. Anapo fikisha miezi 9-12 ya umri, mtoto wako anaweza anza kula viwango vidogo vya chakula kilicho kunwa.

Kumwanzishia mtoto chakula ni kawaida sana kupata watu wengi wakianza na uji unao tengenezwa kwa kutumia mahindi yaliyo siagwa ama unga spesheli wa uji.

Pap

Pia angalia orodha hii Nigerian foods that are great for weaning babies.

Mummy's Yum

American Academy of Paediatrics

Soma pia: 5 Practical Steps To Produce More Breastmilk

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha na kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

 

Written by

Risper Nyakio