Baada ya kujifungua, baadhi ya mambo ambayo mama anafunzwa ni jinsi ya kunyonyesha mtoto mchanga, jinsi ya kuzuia maambukizi, uzazi wa mpango na lishe bora kwake.
Katika kliniki za kabla ya kujifungua, mama huelimishwa kuhusu ulishaji wa mtoto mchanga na kuendeleza baada ya kujifungua. Mama anaelimishwa kuhusu kuanzisha na kudumisha unyonyeshaji bora kwa mtoto.
Utaratibu wa kunyonyesha mtoto mchanga

- Mama anastahili kumnyonyesha mtoto katika lisaa limoja baada ya kujifungua
- Kolostrum, ambayo ni maziwa ya kwanza baada ya mama kujifungua hayapaswi kumwagwa, kwani yana wini wa protini
- Kwa miezi sita ya kwanza ya maisha ya mtoto, mama anastahili kumlisha maziwa ya mama pekee
- Mama anapaswa kukaa wima anaponyonyesha mtoto
Hakikisha kuwa mtoto anashika ziwa vizuri na mdomo wake ili kuzuia hewa kuingia anaponyonya
Mama anapaswa kukaa vipi?
- Mama anastahili kumshika mtoto kwa namna ambayo kichwa na mwili iko laini
- Mwili wa mtoto ukaribiane na ule wa mama
- Mtoto atazame ziwa la mama huku pua lake likiwa kinyume cha chuchu ya mama
- Mama anapaswa kushikilia mwili wote wa mtoto na wala sio shingo yake tu
- Kwa mama aliyefanyiwa upasuaji na kuifanya iwe vigumu kwake kumpakata mtoto ipasavyo, anaweza kutumia mto kumlazia mtoto. Atauweka mto juu ya magoti yake
Jinsi ya kunyonyesha mtoto mchanga

Mama anapofahamu jinsi anavyopaswa kukaa, hatua ya pili ni kufahamu anavyopaswa kumnyonyesha mtoto wake. Ili kunyonyesha vizuri, anapaswa:
- Kumguzisha mtoto chuchu kwenye kinywa chake
- Ngoja hadi mtoto anapofungua mdomo wake
- Mtoto anapofungua mdomo, mama anapaswa amsongeshe kwenye ziwa
- Kidevu cha mtoto kinapaswa kugusa ziwa la mama
Mama anashauriwa wakati wote kuhakikisha kuwa amemaliza maziwa kwenye titi moja kabla ya kumbadilisha mtoto kwenye upande huo mwingine. Mama anaweza kujua iwapo ananyonyesha ifaavyo mtoto anaponyonya kwa kawaida, polepole na kupumzika kidogo muda kwa muda na pia mama hahisi maumivu.
Mama anapogundua kuwa unyonyeshaji wake una hitilafu, kama vile kuhisi uchungu mtoto anaponyonya, mtoto kunyonya kwa kasi, ama mtoto kuwa njaa baada ya kunyonya, anashauriwa kuwasiliana na daktari wake atakayemshauri.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Kunyonyesha Kuna Faida Zipi Kwa Mama?