Ushauri Kutoka Kwa Wataalum Kuhusu Jinsi Ya Kunyonyesha Mtoto Mchanga!

Ushauri Kutoka Kwa Wataalum Kuhusu Jinsi Ya Kunyonyesha Mtoto Mchanga!

Ili mtoto anyonye vizuri, ana paswa kushikwa vizuri kwa njia ambayo hata shinikizwa. Mshike mwili wote na wala sio kwa kichwa ama mabega tu.

Hata baada ya mama kuwa amejitayarisha vilivyo anapo kuwa na mimba. Kuna baadhi ya mambo ambayo hata ng'amua hadi pale ambapo jifungua. Kama vile jinsi ya kunyonyesha mtoto mchanga.

Ni kawaida kumpata mama mjamzito akisoma vitabu vingi kuhusu ulezi na maisha baada ya kujifungua. Makala haya yana mpa mama mawaidha kabambe kuhusu jinsi anavyo paswa kunyonyesha mtoto wake.

jinsi ya kumnyonyesha mtoto mchanga

jinsi ya kunyonyesha mtoto mchanga

 • Unashauriwa kumnyonyesha mwanao lisaa limoja baada ya kujifungua
 • Mnyonyeshe mtoto pekee miezi ya kwanza sita bila kumpa chakula kingine
 • Maziwa ya kwanza yanayo fahamika kama colustrum yana faida sana kwa mtoto. Usiyamwage kwani yana kinga mwili na protini muhimu kwa mtoto mchanga
 • Mshike mtoto vizuri unapo mnyonyesha
 • Kuwa mwangalifu na uhakikishe kuwa mtoto wako anashika chuchu vizuri anapo nyonyesha
 • Mpe mtoto chuchu zote mbili

Je, mtoto anapaswa kushikwa vipi akinyonyeshwa

Kunyonyesha ni wakati muhimu sana kwa mama na mtoto. Ili mtoto anyonye vizuri, ana paswa kushikwa vizuri kwa njia ambayo hata shinikizwa. Jambo la kwanza ni mama kuhakikisha kuwa ameketi vizuri na ana starehe zake.

 • Hakikisha kuwa kichwa na mwili cha mwanao ni laini
 • Mshike mtoto karibu na chuchu na atazame chuchu yako
 • Mwili wa mtoto na mama ikirabiane
 • Mpakate mtoto, mwili wote na wala sio shingo ama mabega pekee

Ishara za uhusiano mzuri

jinsi ya kunyonyesha mtoto mchanga

Baada ya kumshika mtoto inavyofaa, hakikisha kuwa unamfunza jinsi ya kufikia chuchu. Kwa kufanya haya:

 • Kumguzisha mtoto kichwa na chuchu zake
 • Ngoja hadi mtoto anapo kifungua kinywa chake wazi
 • Kisha umsongeshe kwenye titi

Mtoto anapo fanya haya, utagundua kuwa mna uhusiano mzuri:

 • Kukifungua kinywa chake wazi
 • Kidevu cha mtoto kiguze chuchu
 • Kukiinua kinywa cha chini kiwe juu

Kwa mama wa mara ya kwanza, uta funzwa jinsi ya kumshika na kumnyonyesha mtoto hospitalini baada ya kujifungua. Kwa hivyo usiwe na shaka. Na usipo elezewa yote unayo stahili kujua, usiwe na shaka kwani haya yana elimu yote unayo stahili kujua kuhusu jinsi ya kunyonyesha mtoto mchanga!

Chanzo: healthline

Soma PiaSababu Za Kuona Damu Kwenye Maziwa Ya Mama

Written by

Risper Nyakio