Michirizi ama alama za kunyoosha sio jambo geni kwa wanawake hasa baada ya kujifungua. Katika mimba, mwili wa mwanamke hupitia mabadiliko mengi. Kuongeza uzito hufanya mwili kupata alama za michirizi kufuatia mabadiliko ya kasi. Mara nyingi, sehemu zinazo athiriwa na alama za michirizi ni kwenye matiti, tumbo, mapaja na pia mikono. Ni vigumu kuondoa michirizi mwilini lakini kuna mbinu za kupunguza kuonekana kwake.
Jinsi ya kuondoa michirizi
Kuna njia asili za kupunguza kuonekana kwake kama vile kwa kutumia mafuta ya kupiga masi. Kuzingatia utaratibu wa kupaka mafuta haya muda kwa muda, michirizi hii itapungua baada ya muda.

Aloe vera imekuwa ikitumika kwa muda mrefu kurekebisha hali tofauti za ngozi. Kupaka aloe kwenye sehemu iliyoathiriwa na michirizi kunasaidia kupunguza kuonekana kwake. Paka kwenye ngozi kisha uwache ibaki kwa dakika 15 kabla ya kuisugua sehemu hiyo.

Kupaka na kisha kusugua mafuta kwenye sehemu zilizo na michirizi husaidia pakubwa na kupunguza kuonekana kwa michirizi mwilini na kuifanya ngozi ilainike.
Baadhi ya mafuta bora kufanya hivi ni kama vile mafuta ya olive na mafuta ya kupiga masi.
Utaratibu wa kufuata
- Weka mafuta kwenye mikono kisha usugue sehemu iliyoathirika
- Kisha uiwache kwa dakika 30
- Safisha sehemu hiyo kisha uokoge mwili
- Kuna baadhi ya watu wanaofanya uamuzi wa kupaka mafuta wanapolala
- Kumbuka kuwa jambo hili litachukua muda
Sharubati ya limau

Limau ina nguvu za kupunguza kuonekana kwa alama ya kidonda mwilini. Hivyo basi inatumika kupunguza michirizi mwilini.
Tia sharubati ya limau kwenye kontena. Kisha upake kwenye sehemu iliyo na michirizi. Iwache itulie kwa dakika 15. Baada ya hapo, safisha kwa kutumia maji ya vuguvugu. Zingatia utaratibu huu kila siku ili uone mabadiliko.

Asali ina uwezo wa kupunguza kuonekana kwa vidonda mwilini. Weka kiwango kidogo cha asali mkononi, kisha uwekelee kwenye sehemu iliyoathiriwa hadi ikauke. Unaweza amua kutumia kipande cha mavazi. Baada ya kukauka, safisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.
Mbali na mbinu hizi, mwanamke anaweza kutumia mchanganyiko wa sukari, maziwa na maji kuondoa michirizi mwilini. Sharubati la viazi hutumika kuondoa alama zinazo baki baada ya kidonda kupona na hutumika kupunguza kuonekana kwa sana kwa michirizi.
Ni vyema kwa wanawake kukumbuka kuwa mbinu hizi huchukua muda kabla ya matokeo kuanza kuonekana. Pia, wanapaswa kuzingatia utaratibu huu kwa muda bila kukoma. Mwili wako unapendeza kwa njia yoyote ile, haijalishi iwapo una michirizi sehemu nyingi mwilini. Upende mwili wako ulivyo huku ukichukua hatua kuufanya upendeze zaidi.
Chanzo: WebMD
Soma Pia: Jinsi Ya Kupunguza Uzani Wa Mwili Kwa Mama Aliye Jifungua