Siri 5 Kuu Za Kuongeza Maziwa Ya Mama Kwa Mama Anaye Nyonyesha

Siri 5 Kuu Za Kuongeza Maziwa Ya Mama Kwa Mama Anaye Nyonyesha

Kila mtoto wako anapo nyonya chuchu zako, homoni spesheli zinatolewa na maziwa ya mama zaidi yanatolewa.

Sio jambo rahisi kwa mama mpya hasa wa mara ya kwanza kufahamu ratiba bora ya kumlisha mtoto. Wiki za kwanza sita ni muhimu sana kupata ratiba. Una tarajiwa kumnyonyesha mwanao baada ya angalau kila masaa mawili ama matatu kwa siku. Kwa hivyo kupata maziwa tosha ya mwanao huenda kukawa tatizo baadhi ya wakati. Makala haya yana kuelimisha jinsi ya kuongeza maziwa ya mama.

Jinsi ya kuchakata na kuongeza maziwa zaidi ya mama

Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza changia kupunguka kwa maziwa ya mama. Kama vile kula chakula kidogo ama kunywa maji yasiyo fika kiwango. Kuwa na mawazo mengi na kumlisha mtoto kwa kipindi kifupi. Hapa chini kuna baadhi ya njia za kuongeza maziwa ya mama kwa njia asili.

  • Kula lishe bora na yenye afya

jinsi ya kuongeza maziwa ya mama

Kama mama aliye jifungua na anaye nyonyesha, hakikisha kuwa wakati wote unakula lishe bora. Kufanya hivi kutakusaidia kuboresha maziwa ya mama. Unahitaji kula kalori kati ya 300-500 kila siku. Kiwango hiki kina athiriwa na utendaji wako wa kazi kwa siku.

  • Mlishe mtoto wako zaidi

Usiwe na shaka kuwa hautapata maziwa tosha ya kumlisha mtoto wako kila mara. Kila mtoto wako anapo nyonya chuchu zako, homoni spesheli zinatolewa na maziwa ya mama zaidi yanatolewa. Mnyonyeshe mtoto kati ya mara 8 ama 12 kwa siku ili kutengeneza ratiba spesheli ya kuongeza kiwango cha maziwa mwilini.

  • Mlishe mtoto pande zote mbili

jinsi ya kuongeza maziwa ya mama

Kuna manufaa ya kumnyonyesha mtoto kutoka kwa chuchu za pande zote mbili. Mtoto anapo nyonya chuchu, mwili unatoa maziwa zaidi ya mama. Kwa hivyo unapo nyonyesha mtoto kutoka kwa pande zote mbili, utaongeza nafasi zako za kuwa na maziwa zaidi.

  • Chechemua chuchu zako

Unapo chechemua chuchu zako, unaongeza maziwa. Huenda baadhi ya wakati, kuchechemuliwa na mtoto wako kukuwa sio tosha. Kwa hivyo unastahili kufanya hivi kwa kutumia mkono wako. Utachukua muda kusoma na kuzoea mbinu hii. Faida ya mbinu hii ni kuwa ni asili na haina gharama zozote zile.

  • Kunywa maji na viowevu tosha

Kunywa viowevu tosha kutausaidia mwili wako kuchakata maziwa zaidi ya mama. Mwili wako unatumia maji mengi kufanya majukumu tofauti mwilini. Kama vile kuchakata maziwa ya mama. Unastahili kunywa angalau vikombe 13 vya viowevu kwa siku. Kiwango hiki kina lingana na shughuli zako za kila siku na hali ya anga ilivyo.

Kama mama anaye nyonyesha mtoto, jaribu kadri uwezavyo kuutuliza mwili wako ipasavyo. Punguza mawazo mengi kwani yanachangia katika kupunguka kwa maziwa ya mama. Jaribu vidokezo tulivyo angazia vya jinsi ya kuongeza maziwa ya mama unayo toa.

Chanzo: Healthline

Soma PiaVyakula 5 Vinavyo Boresha Kuongezeka Kwa Maziwa Ya Mama

Written by

Risper Nyakio