Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Ya Mapacha

Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Ya Mapacha

Iwapo hakuna njia hususan ya kupata mapacha, kuna njia za kuongeza nafasi zako za kupata mapacha.

Kupata mimba kwa mapacha huenda kukawa changamoto kwa wanawake wengi, hasa kama hauna historia ya familia ya kuwa na ujauzito wa mtoto zaidi ya mmoja. Hakuna njia dhahiri za kuonyesha jinsi ya kupata mapacha, ila kuna njia za kuongeza nafasi zako za kukaribisha mtoto zaidi ya mmoja kwa familia yako inayo zidi kukua.

Jinsi ya kupata mapacha: Hatua za kuongeza nafasi zako

Tuangalie kwa kina kwanza jinsi mapacha wana tungwa.

Kwa mapacha wasio fanana, lazima kuwe na kupevuka kwa yai zaidi ya moja wakati wa ngono. Inapotendeka, mayai yote mawili ama zaidi yana tungwa.

Kwa mapacha wanao fanana, yai moja linaachiliwa kisha kupasuliwa mara mbili. Hata bila ya madawa ya uzazi, mapacha wasio fanana na wanao fanana wanaweza tungwa kwa njia asili.

 Je, aina za ngono zinaweza saidia kupata mapacha kwa urahisi?

getting pregnant with twins

Mbali na kuangalia matibabu ya uzazi na kuwa na familia iliyo na historia ya mapacha, aina za ngono za kupata mapacha huenda pia zitaongeza nafasi zako.

Kitu cha maana zaidi ni kuwachilia manii karibu sana na uke iwezekanavyo.

Hii ndiyo maana watu wengi wanajaribu kutumia aina fulani za ngono, kama vile:

  • Upande kwa upande. Katika aina hii, mwanamke huinama mbele na kisha mchumba wake kumwingia kutoka upande wa nyuma.
  • Njia ya missionary. Hii ndiyo iliyo rahisi zaidi na ni kawaida sana sio kufuatia kustarehe kwake tu, ila kwa sababu pia inakubalisha manii kupata yai bila matatizo.
  • Njia ya kusimama. Kuna aina moja inayo julikana kama 'door jam' inayo husisha kuangaliana na kupeana nguvu kana kwamba mlango. Upande mmoja ukiegemeza mgongo wako, weka mguu mmoja juu huku bwanako aki kuingia. Unahisi mapenzi zaidi na kumsaidia kukuingia zaidi ambayo inaweza boresha nafasi ya mimba ya mapacha.

Iwapo hakuna sayansi inayo unga mkono mojawapo ya aina hizi za ngono, ni rahisi kuona kwa nini watu wengi huamini hivi. Kuimarisha kuingia kwa urahisi kwa manii kwenye uke.

Ila, ni muhimu kuto sahau kuwa kupevuka kwa mayai mengi ndiko suluhu kwa kutunga mimba ya mapacha!

Sababu zingine zinazo athiri kutunga kwa mapacha

jinsi ya kupata mapacha

Utafiti wa mapema uligundua kwamba lishe ya mama huathiri uwezo wake wa kutunga mapacha. Kulingana na watafiti, wanawake walio kula lishe iliyo na bidhaa za wanyama, kama vile maziwa, walikuwa na nafasi mara tano ya kupata mimba ya mapacha.

Bila shaka, kupitishwa ama historia ya kifamilia ya mimba zaidi ya moja pia ni sababu.

Kilicho cha kufurahisha pia ni kuwa waliokatika miaka yao ya 30 ya mwisho wana nafasi zaidi za kupata mimba zaidi ya moja. Mbona? Wanawake kwa mara nyingi huwachilia mayai mengi wakati wa kupevuka kwa mayai wanapo zidi kuzeeka.

Jinsi Ya Kuongeza Nafasi Zako Za Kupata Mimba Ya Mapacha

Utafiti mwingine wa kusisimua, uliochapishwa katika Makala ya Reproductive Medicine unasema kuwa wanawake wanao kuwa warefu wako na nafasi zaidi za kupata mapacha.

Ila, usikate moyo iwapo umeamua kabisa kuwa unataka mtoto zaidi ya mmoja!

Katika ushuhuda wangu kama mwuguzi, nimepata kuwa wanawake wengi hutunga mimba ya mtoto zaidi ya mmoja bila mojawapo ya sababu zilizo tajwa hapa juu.

Kumbuka tu kuwa kinacho jalisha ni kuwa ufanye juhudi zote kuhakikisha kuwa unapata mimba yenye afya, haijalishi ni watoto wangapi ungetaka kuleta kwa hii dunia!

Vyanzo: Science Daily, Healthline, WebMD, VeryWell

Soma Pia: You Are Having Twins, According To These Telltale Signs

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Abigail kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio