Mwongozo Kwa Wanandoa Wanao Jaribu Kupata Mimba Haraka

Mwongozo Kwa Wanandoa Wanao Jaribu Kupata Mimba Haraka

Wasiliana na daktari wako akushauri zaidi kuhusu jinsi ya kusawasisha homoni zako kwa kasi kama ungependa kupata mimba haraka.

Kuna sababu nyingi ambazo huenda zikawafanya wanandoa wafanye ushawishi wa kupata mimba kwa kasi. Huenda ikawa wakati wa mwanamke wa saa yake ya kibiolojia una wadia na hataki kukumbana na matatizo yanayo andamana na kupata mtoto baada ya umri wa miaka 35. Huenda ikawa kuwa mngetaka watoto wenu waandamane na wasiwe na tofauti ya miaka mingi. Pia kwa wanawake wanao kuwa na biashara zao ama kazi, wangependa kumalizana na kupata watoto ili warejelee kazi zao. Ama hata kama mchumba wako ni mwana jeshi na ungependa kutunga mimba kabla arudi kazini. Soma zaidi upate maarifa kuhusu jinsi ya kupata mimba haraka.

Vidokezo vya jinsi ya kupata mimba haraka

jinsi ya kupata mimba haraka

  1. Kufanya tendo la mapenzi bila kinga mara kwa mara, angalau mara tatu na zaidi kwa wiki.
  2. Fuata kalenda yako ya kupevuka kwa yai (ovulation), siku unayo ovuleti una dirisha kubwa ya kutunga mimba. Fanya ngono siku mbili ama tatu kabla siku yako ya kuovuleti. Mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu hadi siku tatu ama tano. Kwa hivyo yai linapo achiliwa kutoka kwa mirija ya uzazi na mbegu yenye afya kupatana nalo, mwanamke anatunga mimba.
  3. Ikiwa mzunguko wa kipindi chako cha hedhi sio cha kawaida (siku 28), huenda ikawa vigumu kwako kutumia kalenda ya kutabiri siku ya kuengua yai. Hesabu siku 14 kabla ya kipindi chako kijacho cha hedhi, ama siku 14 ya mzunguko wako wa hedhi. Na hiyo ndiyo siku uliyo na nafasi zaidi za kutunga mimba.
  4. Ishi mtindo wa maisha wenye afya. Puuza unywaji wa pombe, uvutaji wa sigara na dawa za kulevya. Mbali na hayo, hakikisha kuwa una kula vyakula vyenye afya. Ongeza kiwango cha protini kwenye chakula chako na ule matunda na mboga kwa wingi. Una shauriwa kuhakikisha kuwa unapata usingizi tosha kila siku, angalau masaa manane kila siku.
  5. Zingatia uzani wenye afya, ikiwa una uzito mwingi wa mwili, anza kufanya mazoezi. Kwani watu wanene huchukua muda mrefu kutunga mimba ikilinganishwa na watu wenye uzito wa kawaida.
  6. Punguza fikira nyingi. Tatua matatizo uliyo nayo yanayo kufanya kuwa na mawazo mengi.
  7. Ukiwa na lengo la kupata mimba, usijipe fikira nyingi sana kuhusu kufanya ngono kila mara. Wacha liwe tendo unalo furahia na linalo kuja kwa njia asili, wala usitengeneze ratiba ya kitengo hiki, kwani utajikwaza tu.
  8. Fanya mapenzi kwa mtindo ambao utakuwa rahisi kwa mbegu za kiume kuogelea kwa urahisi hadi kwenye uke wa mwanamke. Kama vile mtindo ambapo msichana ana lala chini na mwanamme kuwa juu ama mtindo ambapo mwanamme anamwingia msichana kutoka upande wa nyuma.

kukoma kupanga uzazi

Kumbuka kuwa lazima kwa wanandoa waache udhibiti wa uzazi wanao utumia ili watunge mimba. Kulingana na njia ambayo mlikuwa mnatumia, ni vyema kufahamu kuwa hautapata mimba punde tu unapo koma kuitumia, kwani mwili wako utachukua muda kusawasisha homoni. Wasiliana na daktari wako akushauri zaidi kuhusu jinsi ya kusawasisha homoni zako kwa kasi. Kufahamu siku yako ya uenguaji wa yai ni muhimu katika kukusaidia kujua wakati ambapo una ratiba zaidi na ambapo ni rahisi kwako kutunga.

Kama una matatizo yoyote ya kiafya, hakikisha kuwa yametibiwa, kwani huenda yaka changia katika kuchelewa kupata mimba. Ni vyema pia kufanyiwa vipimo vya kiafya na kutibiwa maambukizi ya kingono ambayo huenda ukawa nayo.

Soma Pia:Vidokezo 5 Muhimu Kwa Wanawake Wanao Jaribu Kupata Mimba

Written by

Risper Nyakio