Wanandoa wanapo lenga kupata mimba, kufanya mapenzi sio jambo la furaha ama la kuwapumzisha baada ya kuwa na siku ndefu tu. Wana jaribu kufanya vyote wawezavyo ili kuongeza nafasi zao za kutunga mimba. Hata hivyo ni muhimu kwa wanandoa kuto jifilisisha kimawazo bidii zao za kutunga mimba zisipo faulu. Zidi kujaribu na bila shaka lengo lenu la kuwa wazazi litatimia siku moja. Tazama jinsi ya kupata mimba kirahisi.
Licha ya hayo, ni muhimu kwa wanandoa kufanya kazi na daktari wa masuala ya uzazi. Hivyo, atawashauri kuhusu mnavyo stahili kufanya na kuzingatia maendeleo yenu.
Tazama mbinu 3 kuu za jinsi ya kupata mimba kirahisi

- Kuzingatia siku za rutuba za mwanamke
Mwanamke huwa na siku ambapo ana rutuba zaidi katika kila mzunguko wake wa hedhi. Katika kipindi hiki ana nafasi za juu za kutunga mimba. Siku yenye rutuba zaidi inayo fahamika kama siku ya kupevuka kwa yai ama ovulation huwa siku bora zaidi ya kufanya mapenzi. Kwa wanandoa wanao lenga kuwa wazazi. Hii huwa siku ya 14 baada ya kuanza kipindi cha hedhi. Siku tano kabla ya siku hii na siku mbili baada yake.
Mwanamke anaweza fahamu siku hii kwa kuangalia mabadiliko yanayo fanyika mwilini mwake. Kama joto mwilini kuzidi, idadi ya ute unao toka kwenye kizazi kuongezeka, kuhisi hamu ya kufanya mapenzi na zinginezo.

- Mazoea ya kufanya tendo la ndoa
Ili mwanamke ashike mimba, lazima mwanamme amwage mbegu zake kwenye kizazi chake. Na tendo la ndoa ni lazima. Ili kuongeza nafasi za kushika mimba, wanandoa wana hitajika kufanya tendo hili mara nyingi. Hata hivyo ni muhimu kuto jichosha kwani kitendo hiki kina hitaji nishati, fanya mara ambapo nyote mtahisi mnaweza.
Kuna utafiti unao dokeza kuwa staili hasa za kufanya ngono zina ongeza nafasi za wanandoa kushika mimba.
Kulingana na utafiti, watu wanao kuwa na matatizo haya ya kiafya hutatizika kushika mimba. Juhudi zao za kufanikisha hili huchukua muda zaidi. Uzito zaidi ama uzani mdogo zaidi wa mwili. Mwanamke anaye taka kupata mimba ana shauriwa kuangazia lishe yake na kuhakikisha kuwa ana kula vyakula bora. Punguza unywaji wa kaffeini na bidhaa zilizo na kaffeini. Punguza unywaji wa vileo na uvutaji wa sigara.
Soma Pia: Njia Tofauti Ambazo Wanandoa Wanaweza Kufurahia Ngono Katika Mimba!