Vidokezo Vya Kupata Mimba Na Vipindi Vya Hedhi Visivyo Vya Kawaida

Vidokezo Vya Kupata Mimba Na Vipindi Vya Hedhi Visivyo Vya Kawaida

Vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida hupunguza nafasi yako ya kupata mimba. Tuna angazia jinsi ya kupata mimba na hedhi na isiyo ya kawaida.

Kipindi cha hedhi kisicho cha kawaida si jambo mpya kwa wanawake. Kati ya asilimia 14% na 25% ya wanawake huwa na vipindi visivyo vya kawaida katika wakati mmoja maishani mwao. Vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida vinaweza kuathiri nafasi  zako za kuwa mjamzito. Kwa kweli, ndio chanzo cha visa asilimia kati ya 30 hadi 40 za utasa kwenye wanawake. Kwa hivyo kwa kina mama wanaotarajia katika hiki kifungo, lengo ni kujua jinsi ya kupata mimba na hedhi isiyo ya kawaida kwa haraka zaidi.

Ujauzito kwa wakati mwingi huwa juu ya wakati ata kwa wanawake walio na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida. Lazima kutungwa kwa yai kuambatane na kuachiliwa kwa yai. Wakati yai linapoachiliwa kutoka kwa ovari moja, hilo hujulikana kama ovulation. Huu ndio wakati mwili wako hujitayarisha kwa uwezekano wa ujauzito. Lakini iwapo huu wakati utapita bila ya yai kutungwa, basi lile tabaka la uterasi litatoka na kupitia kwa uke. Huo ndio mwanzo wa kipindi cha hedhi. Mara nyingi vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida hupunguza uwezekanao wa hili kutokea hivyo basi hupunguza nafasi za kuwa mjamzito.

Kuachiliwa kwa yai na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida: Hivi ni nini hasa?

Ovulation and irregular periods, what are they

 

  • Vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida: Iwapo vipindi vyako vya hedhi hutokea baada ya chini ya siku 21 ama huwa mara yote ni zaidi ya siku 36 una vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida. Njia moja ya kujua ni jinsi huwezi kutabiri kwa uhakika kipindi chako kinachofuatia.
  • Kuachiliwa kwa yai: Huwa uko katika hali nzuri ya uzazi kwa kipindi kinachokaribia kuachiliwa kwa yai. Kuachiliwa kwa yai ni wakati yai hutolewa na ovari ikingoja kutungwa.
Kwa nini ni vigumu kwa wanawake walio na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida kushika mimba?

Kila mwanamke huachilia yai siku kumi na nne kabla ya kipindi cha hedhi kinachofuatia. Kwa mwanamke aliye na kipindi cha hedhi kisicho cha kawaida ataachilia yai  siku ya 14 ikiwa ana mzunguko wa hedhi wa siku 28. Iwapo ana mzunguko wa siku 32 ataachilia yai siku ya 18. Kwa bahati mbaya, kwa wanawake ambao kwa mara nyingi huwa na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida , si rahisi kusema kwa uhakika ni siku ipi yai litaachiliwa. Hili hufanya kuwa mjamzito jambo ngumu  kwani hujui ni lini utahesabu siku kumi nne kutoka.

Kulingana na George Carson, OB/GYN  kutoka Regina, mwanamke mwenye mzunguko wa hedhi wa siku 28 huachilia yai mara 13 kwa mwaka.  Kwa hivyo kuna fursa 13 ambazo anaweza kushika mimba na anaweza kutambua ni lini. Lakini kama anaachilia yai mara sita kwa mwaka, bila shaka ana fursa  nusu kuwa ataweza kushika mimba.

Kwa kuongeza, wanawake wengine walio na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida huwa hawaachilii yai kabisa. Wanaweza kuvuja damu kwa wakati lakini kipindi cha hedhi huwa hakifuatii baada ya yai kuachiliwa. Hili hujulikana kama anovulatory.

Jinsi ya kupata mimba haraka na hedhi isiyo ya kawaida

how to get pregnant even with irregular periods

Vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida hupunguza uwezekano wako wa kuwa mjamzito, lakini kwa kuzingatia hizi vidokezo unaweza kurejesha vitu kwenye mkondo.

  • Ratibisha siku ya kuachilia kwa yai

Kalenda ya kipindi cha hedhi inaweza kukusaidia kufuatanisha siku zako za kuachiliwa kwa yai, ambao ndio mwanya wako wa nafasi bora zaidi ya uzazi. Hio app imebuniwa kukusaidia ili kukuwezesha kuweka habari na dalili zitakazokusaidia kuhesabu mzunguko wako wa hedhi. Pia kuweza kutabiri siku yako ya kuachiliwa kwa yai, unaweza kutazama makasi inayotokana kwenye uke na kiwango cha joto ukitumia kipimajoto mwilini.  Wakati wa kuachiliwa kwa yai, huwa kuna wingi wa homoni estrogen na progesterone, inayosababisha joto la mwili kuongezeka.  Na kipimajoto huweza kugundua ata mabadiliko kidogo kabisa kwenye joto hadi 1/100th ya digrii.

  • Fanya mapenzi zaidi

Manii yanaweza kukaa kwenye mwili hadi siku sita. Kwa hivyo, kufanya mapenzi kwa mara nyingi huongeza fursa yako ya kuwa mjamzito ata kama una vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida. Kufanya mapenzi kwa mara nyingi hurahisisha uwezekano wako wa kupata mwanya wako wa uzazi ulio bora.

Kwa kuongeza, kufikiria ni lini bora kufanya mapenzi, unaweza kutumia vifaa  vya kutabiri kupima mkojo.  Hili huweza kuwezekana kwani kabla ya kuachilia yai wanawake hutoa luteinizing hormones (LH). Hizi homoni hufanya yai kuachiliwa na ovari.

  • Kula vizuri

Iwapo vipindi vyako vya hedhi  ni visivyo vya kawaida, kula chakula cha kunawirisha na kilicho sawa. Jiepushe na chakula kilicho na mafuta mengi na kundi la vyakula la kabohidrati. Pia jiepushe na vyakula vya viwandani  na badala yake kula matunda kwa wingi, nafaka na pia mboga.

  • Zingatia uzito wa wastani

Hili linazungumzia kuwa na uzito wa juu sana ama wa chini sana. Ni muhimu kuzingatia uzito wa wastani kwani matatizo kwenye uzito husababisha usawaziko. Na wakati kuna usawaziko wa homoni inaweza kusababisha vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida na kuvuruga kuachiliwa kwa yai.  Na kama mwanamke aliye na vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida na aliyeamua anataka kuwa mjamzito, kuzingatia uzito wa wastani inaweza kuzuia haya matatizo. Na iwapo una shida kufikia uzito wa wastani inaweza kuwa shida inayotokana na usawaziko wa homoni. Kwa hivyo zungumza na daktari wako.

  • Punguza mkazo wa akili

Reduce Stress

Kupunguza mkazo wa akili kunaweza kusaidia sana iwapo unajaribu kuwa mjamzito haraka na una vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida. Wasiwasi na mkazo wa akili unaweza kuchelewesha kuachiliwa kwa yai ikipunguza nafasi zako za kuwa mjamzito. Jaribu kuzingatia mbinu za kupunguza mkazo wa akili mchana kwani pia kujaribu kuwa mjamzito peke yake inaweza kuwa ya kuongeza mkazo wa akili.

Vipindi vya hedhi visivyo vya kawaida huwa jambo la kawaida na kwa wakati mwingine husababishwa na matatizo yaliyofichika. Iwapo vipindi vyako vya hedhi si vya kawaida mtembelee daktari  wako kwa uchunguzi zaidi. Daktari atakufanyia uchunguzi , atadhibitisha viwango vyako vya homoni  na pia aangalie iwapo kuna tatizo ambalo halijatatuliwa.

Soma PiaEffective Home Remedies For Irregular Periods

Written by

Risper Nyakio