Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

Makala haya yanakusaidia kujua jinsi utakavyo pata mtoto mrembo na mwenye busara.

Ni jambo la kawaida kwa mama mwenye mimba kuwa na shaka kuhusu mtoto aliye tumboni mwake na wakati wote kutaka kuhakikisha kuwa mtoto yuko salama, ana afya na ana kua ipasavyo. Bila shaka, sote twafahamu kuwa kuishi maisha ya afya unapokuwa na mimba kutasaidia mtoto wako kuwa mkubwa na kuwa na nguvu. Ila, ulijua kuwa anaweza kuwa mrembo zaidi na mwerevu kulingana na maisha unayo ishi? Tuna angazia jinsi ya kupata mtoto mrembo.

Ni kweli kuwa chaguo unazo fanya kila siku zinaweza kusaidia kukuza akili ya mtoto wako. Hii ni iwapo unakula vyakula vyenye afya kama vile mboga za kijani ama kufanya mazoezi kwa dakika chache kila siku. Utakuwa na mtoto mrembo na mwenye busara.

jinsi ya kupata mtoto mrembo

Unacho fanya ukiwa na mimba kita athiri maisha ya mtoto wako, ukuaji na maendeleo yake na busara yake katika siku za usoni.

Vidokezo vya jinsi ya kupata mtoto mrembo

  • Kula vitamini vya kabla ya kujifungua

Unapokuwa na mimba, unapaswa kutembelea daktari wako na uhakikishe kuwa unapewa vitamini B na folic acids. Hizi ni muhimu katika kutengeneza seli za akili zenye afya. Pia wanawake wanao anza kutumia vitamini hizi mapema wiki nne hadi wiki nane wanapo pata mimba, wana asilimia 40 ya chini ya hatari ya kupata watoto wanao kuwa na matatizo wanapo zaliwa. Pia ni vyema kula omega-3 fatty acids na iron.

  • Kula matunda na mboga

Matunda na mboga ni muhimu hasa katika wiki za kwanza za mimba yako. Zina saidia kupunguza kichefu chefu. Ni vyema kula unapo amka na kuhakikisha kuwa sahani yako ina mboga nyingi.

  • Kufanya mazoezi

Mazoezi yatakusaidia hasa kuhakikisha kuwa safari yako ya ujauzito ni rahisi na wakati wa uchungu wa mama na kujifungua. Pia ni muhimu katika kuipa akili ya mtoto nguvu. Utafiti una thibitisha kuwa watoto wa mama wanao fanya mazoezi wanapokuwa wajawazito hufanya vyema katika mitahani yao ikilinganishwa na watoto wa wazazi ambao hawafanyi zoezi wanapokuwa wajawazito. Ni vyema kwa mama anaye tarajia kujifungua kuhakikisha kuwa anafanya mazoezi kwa angalau dakika 30 kila siku. Hakikisha kuwa unafanya kazi na mtaalum wa afya na pia usifanye mazoezi magumu ili kuhakikisha kuwa mwili wako hautaabiki.

jinsi ya kupata mtoto mrembo

  • Kuongea na mtoto

Kila mama anashauriwa kuchukua muda kila siku na kuongea na mtoto aliye tumboni mwake. Kuna saidia kuwa na utangamano kati ya wawili hawa. Na mtoto anapo zaliwa kulingana na alivyo kuwa akiongeleshwa na mama, anajua kuwa anapendwa. Mtoto anaye kuwa na amani na imani kuwa anapendwa na wazazi wake ana ujasiri anapo zaliwa na ushupavu huu unamfanya apendeze zaidi.

Kwa mama yeyote anaye tarajia kujifungua na anashangaa jinsi atakavyo jifungua mtoto anaye pendeza, orodha yetu ya vidokezo vya jinsi ya kupata mtoto mrembo vitakusaidia pakubwa.

Written by

Risper Nyakio