Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Siri 3 Za Jinsi Ya Kupata Mtoto Wa Kiume (Vidokezo Muhimu Kwa Wanandoa)

3 min read
Siri 3 Za Jinsi Ya Kupata Mtoto Wa Kiume (Vidokezo Muhimu Kwa Wanandoa)Siri 3 Za Jinsi Ya Kupata Mtoto Wa Kiume (Vidokezo Muhimu Kwa Wanandoa)

Kuna matibabu ambayo yanaweza wasaidia wanandoa kutunga mimba ya jinsia wanayo tamani. Kufuatia hatari zinazo andamana na mbinu hizi, hazi shauriwi kwa sana.

Baada ya kuwa katika ndoa kwa miaka miwili, Zara na bwanake walikuwa tayari kuwa wazazi. Akilini, Zara alikuwa na picha ya familia ambayo angependa kuwa nayo. Familia ya watu watatu, yeye, bwanake na mtoto mmoja wa kiume. Walianza juhudi za kutunga mimba, baada ya kuhakikisha kuwa wamefanya mipango kabambe kuwa na mtoto kwenye familia yao. Kwa bahati nzuri, walifanikiwa na baada ya muda mdogo, Zara aliweza kutunga mimba.

Alizidi kuomba usiku na mchana kuwa mtoto aliyekuwa tumboni mwake awe kijana. Kwani hilo ndilo lililo kuwa ndoto lake. Miezi tisa ilipita na hata ingawa ilikuwa na misuko suko yake, walijazwa na furaha tele alipo jifungua. Mtoto ni baraka haijalishi jinsia yake! Alipo mshika mtoto huyu mchanga mikononi mwake, alijiona kwenye sura ya mtoto huyu. Na hata kama azimio lake halikutimia, alifurahi kuwa alijifungua mtoto wa kike mwenye kupendeza na mwenye afya bora. Je, kwa wanandoa kama Zara na mchumba wake, kuna uwezekano wa kupata mtoto wa jinsia unayo tamani? Soma zaidi kuhusu jinsi ya kupata mtoto wa kiume.

Vidokezo muhimu vya jinsi ya kupata mtoto wa kiume

jinsi ya kupata mtoto wa kiume

Hakuna njia dhibiti ya kupata mtoto wa jinsia moja. Kwani kinacho dhibiti jinsia ya mtoto atakaye zaliwa ni chromosome inayo achiliwa na baba na kurutubisha yai la mwanamke. Ila kuna njia ambazo wanandoa wanaweza kutumia kuongeza nafasi zao za kutunga mimba ya mtoto wa kiume.

  1. Wakati wa kufanya tendo la ndoa

Ikiwa wanandoa wangependa kuongeza nafasi zao za kujifungua mtoto wa kiume, wana shauriwa kufanya ngono siku ya kupevuka kwa yai la mwanamke. Na sio wakati wowote kabla ya masaa 24 kabla ya siku hii. Kwa sababu hii, ni muhimu sana kwa mwanamke kufahamu chati yake ya mzunguko wa hedhi na siku ya kupevuka kwa yai.

Ni vyema pia kwa mwanamke kufika kilele, tofauti na pale ambapo wanandoa wanatafuta mtoto wa kike. Ambapo mama hashauriwi kufika kilele katika tendo la wanandoa. Kabla ya tendo la mapenzi, wanandoa wanaweza kunywa kikombe cha kaffeini ama kula chokleti.

2. Lishe

jinsi ya kupata mtoto wa kiume

Lishe ni muhimu sana kwa mama anaye taka kutunga mimba. Na lishe inayo faa huenda ikaongeza nafasi za kupata mtoto wa kiume. Kulingana na utafiti uliofanyika mwaka wa 2008, ilidhihirika kuwa wanawake walio kula wanga zaidi waliongeza nafasi za kujifungua mtoto wa kiume.

Sio kumaanisha kuwa mama anapaswa kuongeza kiwango cha wanga kwenye lishe yake kwa idadi kubwa. Anajihatarisha kuongeza uzito mwingi wa mwili. Lishe yake inapaswa kuwa ya wanga yenye afya. Vyakula vyake vinapaswa kumsaidia kuongeza kiwango cha alkaline kwenye mwili.

3. Usaidizi wa kimatibabu

Kuna matibabu ambayo yanaweza wasaidia wanandoa kutunga mimba ya jinsia wanayo tamani. Kufuatia hatari zinazo andamana na mbinu hizi, hazi shauriwi kwa sana. Mama ako katika hatari ya kufanyiwa upasuaji ama kuharibika kwa mimba.

Mchakato wa kimatibabu unao fahamika kama preimplantation genetic diagnosis (PGD) ina saidia kutengeneza viinitete, kupima jinsia yake na kupandikiza kiinitete chenye jinsia inayo kusudiwa kwenye kuta za uterasi. Na mama atajifungua mtoto wa jinsia aliyo tamani.

Ikiwa shaka yenu kuu kama wanandoa ni jinsi ya kupata mtoto wa kiume, ni matumaini yetu kuwa makala haya yatawasaidia kuamua njia itakayo wafaa zaidi ya kutimiza matamanio yenu.

Chanzo: healthline

Soma Pia: Matayarisho Ya Mwisho Kabla Ya Mama Kujifungua

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Trying To Conceive
  • /
  • Siri 3 Za Jinsi Ya Kupata Mtoto Wa Kiume (Vidokezo Muhimu Kwa Wanandoa)
Share:
  • Siri 5 Za Jinsi Ya Kupata Mtoto Wa Kike

    Siri 5 Za Jinsi Ya Kupata Mtoto Wa Kike

  • Orodha Ya Vyakula Bora Vya Kukusaidia Kupata Mtoto Kirahisi

    Orodha Ya Vyakula Bora Vya Kukusaidia Kupata Mtoto Kirahisi

  • Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

    Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

  • Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

    Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

  • Siri 5 Za Jinsi Ya Kupata Mtoto Wa Kike

    Siri 5 Za Jinsi Ya Kupata Mtoto Wa Kike

  • Orodha Ya Vyakula Bora Vya Kukusaidia Kupata Mtoto Kirahisi

    Orodha Ya Vyakula Bora Vya Kukusaidia Kupata Mtoto Kirahisi

  • Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

    Vidokezo Vya Jinsi Ya Kupata Mtoto Mrembo Na Mwenye Busara

  • Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

    Uandalizi Muhimu Maishani Kabla Ya Kupata Mimba

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it