Ikiwa unatatizika na kulala na kushangaa jinsi ya kupata usingizi kwa haraka, tuna kudokezea siri zitakazokusaidia. Kupata usingizi tosha ni muhimu katika utendaji kazi wa mwili wa kila siku. Kulingana na Sayansi, unapaswa kupumzika kwa masaa manane kila usiku. Lakini kufuatia mabadiliko ya kimaisha na haja ya kufanya kazi ili kukimu mahitaji ya kimaisha, inakuwa vigumu kulala kwa masaa haya yote. Hata hivyo, kutolala vya kutosha kuna athari hasi kwa mwili. Ikiwa unatatizika kulala, tazama vidokezo hivi.
Jinsi ya kupata usingizi kwa haraka

- Tumia godoro na mto bora
Watu wengi hupuuza umuhimu wa kutumia godoro na mto bora, na kusema kuwa hakuna haja ya kununua godoro ya kikliniki, na kuwa ina bei ghali. Ni muhimu kubadilisha mto na godoro baada ya muda. Kulalia godoro iliyozeeka huumiza mgongo na shingo na huenda ikafanya usingizi kupotea usiku. Huenda ukagundua kuwa unalala kama mtoto unapokuwa kwenye hoteli ila mambo yanakuwa tofauti ukiwa kwako. Hii ndiyo sababu. Badilisha godoro na mto unaotumia, nunua kwenye chapa zinazoaminika.
2. Tazama na usikilize vitu vinavyopuzisha akili usiku
Kusikiliza na kutazama vitu vinavyopumzisha akilini jioni ni muhimu, ili kuiweka akili katika mazingira ya kutulia tayari kulala. Tofauti na kusikiliza muziki wenye sauti ya juu na filamu za kutisha ambazo zinahusisha akili kufikiria. Kusoma kitabu kinacholiwaza na kuburudisha kunaituliza akili.
3. Tengeneza chumba cha kulala

Chumba chako cha kulala kinaathiri uwezo wako wa kulala kwa kasi ama kukosa usingizi. Paka rangi isiyo shouting sana. Hakikisha kuwa unatengeneza kitanda chako kwa kutumia matandiko safi. Punguza mwanga unaoingia chumbani chako usiku, epuka kutumia radio na runinga chumbani cha kulala. Hakikisha pia chumba chako kinapata hewa safi na tosha.
4. Punguza mwanga wa buluu usiku
Mwanga wa buluu hutokana na vifaa vya kielektroniki kama vile simu, runinga na tarakilishi. Kulingana na utafiti, mwanga wa buluu hupunguza utoaji wa kichocheo cha melatonin mwilini kinachotufanya tulale. Epuka kutumia mitandao ya kijamii usiku, badala yake, soma kitabu.
5. Kuwa na ratiba maalum ya kulala
Kuzingatia ratiba maalum ya kulala na kuamka kunasaidia kuizoesha akili yako kuwa wakati fulani unapaswa kuwa ukilala, huku ukiamka wasaa fulani. Zingatia ratiba hii na baada ya muda utafahamu kuwa hautatiziki kuamka wala kulala. Kubadilisha ratiba yako ya kulala huenda kukaathiri usingizi wako.
Soma Pia: Faida 7 Za Kufanya Yoga Kwa Afya Yako