Jinsi Ya Kupika Kitoweo Cha Nyama Ya Mbuzi

Jinsi Ya Kupika Kitoweo Cha Nyama Ya Mbuzi

Wali na matoke ni vyakula vyema vya kupakua na kitoweo cha nyama ya mbuzi.

Katika karibia kila familia ya Ki Nigeria, kitoweo cha nyanya ni kawaida katika kila lishe. Tunaitumia kutengeneza Jollof ya ki Nigeria ambayo ni maarufu; pia tuna itumia kama kitoweo kwenye supu zingine kama vile okro ama ewedu. Kitoweo cha nyanya cha ki Nigeria ambacho kinatumika kula wali mweupe, mihogo ya kuchemsha, mkate na chakula kingine chochote! Hii ndiyo sababu tunafikiria kuwa kila mtu anapaswa kujua jinsi ya kupika kitoweo hiki.

Hatuwezi ishi bila kitoweo. Ni kweli kuwa huenda kitoweo kikawa kina unganisha mataifa. Kwa sababu haijalisha nchi unayo toka, unakula kitoweo sio? Pia, utapata viungo vya kitoweo mahali popote unapo ishi katika bara la Afrika; viungo ambavyo unaweza tumia haijalishi msimu.

Kupika kitoweo kizuri za nyanya sio jambo rahisi. Chemsha nyanya na mchanganyiko wa pili pili kwa muda mrefu na kitachomeka. Uki chemsha kwa wakati mfupi, kitoweo hiki huenda kikaonja kana kwamba hakija iva ama kiwe na ladha ya kuganda. Unajua jinsi ya kutayarisha kitoweo? Usiwe na shaka kwani tutakufunza.

Pata maagizo yaliyo kamilika.

Jinsi Ya Kupika Kitoweo Na Nyama Ya Mbuzi

Jinsi Ya Kupika Kitoweo Cha Nyama Ya Mbuzi

Kabla ya tuanze, ni jambo la busara kutayarisha kitoweo kwa kiwango kikubwa na kisha uhifadhi kwenye freezer hadi kwa mwezi mzima. Kumbuka, kinatumika kwa karibu vyakula vyote vya kinigeria vya familia yako ambayo itakuwa inakula. Na utaokoa muda mwingi iwapo umekitayarisha; yote unayo paswa kufanya ni kukipasha kwa microwave kwa kiwango unacho hitaji kila mara.

Viungo
 • 1.5 kilo ya nyanya zilizo mbichi (kwa kawaida katika Nigeria zinajulikana kama Jos tomatoes)
 • 600gramu za nyanya za kugandishwa maarufu kama tomato paste (ama Tomato Puree yenye unyevu nyevu: 1.2kilo)
 • Mafuta ya kupikia: kiwango kikubwa
 • 2kilo nyama ya mbuzi
 • 2-3 vitunguu vya saizi ya wastani
 • Pili pili ya Habanero na chumvi (kuongeza ladha)
 • 3 big stock cubes
 • 2 vijiko vya thyme
Kabla ya kupika kitoweo
 1. Osha na usiage nyanya zako mbichi za plum. Kumbuka kutoa mbegu iwapo hauna uhakika ama kifaa chako cha kusiaga kita zisiaga zote vyema.
 2. Iwapo unatumia tomato paste nene iliyo gandishwa ambayo ni maarufu sana Nigeria, ichanganye na maji baridi ili kupata mchanganyiko laini.
 3. Kata vitunguu viwe vipande vidogo.
 4.  Kata nyama yako ya mbuzi na upike na vitunguu vilivyo katwa nusu, weka viungo vya ladha na thyme. Kisha uongeze chumvi na uipe muda iive na mvuke kwa angalau dakika 5, kisha uipeleke kwa ungo utoe maji. Kaanga nyama yako. Hii sio lazima ila ni muhimu kwani chakula chako kina pata rangi ya kupendeza ya hudhurungi.

Vitu vya kujua kuhusu kupika nyama ya mbuzi:

Jinsi Ya Kupika Kitoweo Cha Nyama Ya Mbuzi

Ongeza maji hadi kwa kiwango cha viungo vya chungu unapo pika. Unapo pika nyama, jaribu usiongeze chumvi kwa nyama ambayo haija iva. Hii ni kwa sababu chumvi huziba mashimo ya nyama. Hii inazuia ladha ya asili ya nyama ya mbuzi kuto toka kwenye maji yaliyo karibu; na kuziba viungo vya ladha kuto ingia kwenye nyama na kuipa ladha. Matokeo yatakuwa kuwa nyama yako haitakuwa na wingi wa ladha ya asili. Itakuwa na ladha ya kuongezwa tu. Chumvi pia inaifanya nyama kuwa ngumu na hivi kuchukua muda mrefu kupikika. Kwa hivyo ongeza chumvi nyama ikiiva.

Jinsi ya kutayarisha kitoweo: maagizo

Jinsi Ya Kupika Kitoweo Cha Nyama Ya Mbuzi

  1.  Mwaga nyanya mbichi kwenye chungu na upike kwa moto wa juu hadi karibia maji yote yaishe. Iwapo una tomato puree iliyo kwenye kontena, ongeza hizi kwenye chungu chako kisha upunguze moto.
  2. Ongeza mafuta ya kupika, vitunguu vilivyo katwa katwa na tomato puree iliyo nene ambayo ulichanganya katika maagizo ya pili hapo juu (iwapo ni puree ndiyo unayo tumua) Changanya vyema.
  3. Kaanga kwa kutumia kiasi kidogo cha moto na uchanganye baada ya muda hadi pale ambapo mafuta yame achana na tomato puree. Tomato puree iliyo kaangwa vizuri na mafuta. Onja tomato puree iliyo kaangwa ili kuhakikisha kuwa nyanya mbichi zimeiva zote. Kwa muda na uzoefu, unaweza tofautisha tomato puree iliyo pikika vyema mbali na inavyo nukia.
  4. Wakati ambapo utakuwa na furaha na nyanya zako zilizo kwenye kitoweo chako cha nyanya kuwa zimepikika vyema, mwaga mafuta yaliyo zaidi.
  5. Weka chungu chako cha kitoweo cha nyanya kwenye moto na uongeze nyama yako (maji kutoka kwa upishi wako wa nyama ya mbuzi).  Kuna vipande vingi vya mifupa kwenye upande wa chini, kuwa makini usiviongeze.
  6.  Ongeza pili pili na nyama iliyo kaangwa. Changanya vyema na uongeze chumvi kama inatakikana. Pia unaweza ongeza maji kidogo katika hatua hii iwapo kitoweo chako ni chembamba sana.
  7. Funika chungu chako na upike kwenye moto wa wastani hadi viungo vyote kwenye chungu viive vyema na mvuke. Changanya vyema na chakula chako kitakuwa sawa.
Tazama video hii ya jinsi ya kupika:

Hii hapa ndiyo jinsi ya kupika kitoweo chako kwenye njia ya ki Naija. Kifurahie chakula chako!

AllNigerianRecipes

Soma pia: 3 Ways To Cook Tasty Chicken Wings

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Ayeesha kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio