Jinsi Ya Kupika Wali Wa Nazi Kipwani!

Jinsi Ya Kupika Wali Wa Nazi Kipwani!

Wali wa nazi ni chakula kilicho maarufu sana hasa katika upande wa pwani. Ukitafuta jinsi ya kupika wali wa nazi kwenye mtandao, utapata matayarisho tofauti kutoka kwa wapishi duniani kote. Tafadhali fahamu kuwa matayarisho ya chakula hiki ya kipwani ni bora zaidi. Habari njema ni kuwa utasoma na kutia akilini matayarisho ya wali wa nazi.

jinsi ya kupika wali wa nazi

Chanzo: Sisiyemmie.com

Wali wa nazi ni nini hasa?

Kama jina linavyo ashiria, wali wa nazi kwa kifupi ni wali ulo tengenezwa kwa kutumia maziwa ya nazi. Matokeo ni walio ulio na ladha na harufu ya kuvutia. Iwapo unasoma jinsi ya kutayarisha wali wa nazi, unapaswa kujua kuwa matayarisho yana tofautiana na wali wa kukaanga ama ule wa jollof kwa sababu mbinu hizi zinahitaji kukaanga kwa sana na wali wa nazi hauhitaji hayo yote.

Wakati wa kupakua wali wa nazi

Kujua jinsi ya kupika wali wa nazi hakutakusaidia iwapo hautajua jinsi ya kuringa na chakula ulicho jua kukitayarisha. Unaweza wapikia jamii na familia wako chakula hiki wakati wa mchana ama hata usiku. Iwapo kuna sherehe ijayo, panga kupika wali wa jollof na wali wa nazi na upakue kando.

Viungo

3 vikombe vya mchele
2 nazi za wastani ama 400ml maziwa ya nazi
Kuku, nyama ya ng’ombe ama samaki wa barafu
2 vikombe vya supu ya nyama
I kitunguu kikubwa kilicho katwa
2 matawi ya bay (bay leaves)
2 nyanya zilizo katwa
3 vijiko vidogo vya poda ya crayfish
4 pilipili
Chumvi -ya ladha
2 viungo vya chumvi ama seasoning cubes
1 kijiko cha mafuta ya nazi

Jinsi ya kutayarisha wali wa nazi njia ya Kipwani

Hatua 1 – Kupika nyama na kutoa supu

• Pika kuku wako kwa kutumia vipande vya kuongeza ladha, pilipili na kitunguu kilicho katwa
• Pika nyama hadi iwe laini
• Kausha supu kutoka kwa nyama na uitenge kando
• Kaanga nyama kwenye mafuta ya nazi hadi iwe ya hudhurungi na uweke kando

Hatua 2 – Kutayarisha maziwa ya nazi(iwapo unatumia nazi freshi)

• Katanisha nazi yako kisha ukamue nyama yake
• Kata nyama ya nazi kwa vipande kisha uimwage kwenye kifaa cha kusiaga maarufu kama blender
• Pia unaweza kifaa cha kuwava ama grater iwapo hauna blender
• Mwaga nazi iliyo wavwa kwenye bakuli
• Ongeza vikombe viwili vya maji moto kwenye bakuli kisha uchanganye
• Chukua taulo ya jikoni iliyo safi kisha uitumie kutenga maziwa na mabaki ya nazi
• Ongeza kikombe kimoja cha maji ya na usuuze mabaki yale tena
• Weka maziwa kando kisha utupe mabaki yale

Hatua 3 – Jinsi ya kutayarisha wali wa nazi

• Mwaga mafuta ya nazi kwenye chungu kisha ukaange kwa dakika tatu
• Ongeza kitunguu kilicho katwa, kisha nyanya na upike hadi ziive
• Ongeza viungo vya ladha na chumvi
• Mwaga maziwa ya nazi kwenye chungu na uyape muda yatokote
• Ongeza mchele, crayfish na pilipili na upike hadi wali uwe tayari
•Hakikisha kuwa maji yote yana kauka
• Utajua kuwa wali wako uko tayari usipo shikana
• Pakua na ule na nyama

Iwapo unatafuta matayarishio mwafaka ya wali wa nazi wa kipwani, usitafute zaidi. Matayarisho haya yana kuongoza hatua baada ya nyingine hadi uwe gwiji wa mapishi haya.

Kumbukumbu: Healthline.com

Soma pia: Nigerian chicken pepper soup recipe

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio